Wamesema hawapunguzi nauli: Je, hiyo ruzuku ya mafuta ni kwa faida ya nani?

Wamesema hawapunguzi nauli: Je, hiyo ruzuku ya mafuta ni kwa faida ya nani?

sepema

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2019
Posts
591
Reaction score
1,001
Kumekucha wakuu,

Nipo siti yanyuma kwenye gari ya abiria. Nikiwa nimetulia zangu mara nastushwa na mtoza nauli akidai chake. Mara napata faraja baada yakukumbuka leo ni Juni2 ambapo bei ya mafuta imetangazwa kupungua toka Juni 1.

Nimempa nauli nilokua nimezoea kulipa kabla ya mafuta kupanda Ila amegoma anadai nauli hazijashuka na hazitashuka.

Hali ipoje huko kwenu?

Nakama hawapunguzi nauli,Ile ruzuku yamafuta nikwa faida ya nani hasa?

Mjenga nchi ni mwananchi!
 
Sipo Dsm mkuu...Labda huko Hali inaweza kuwa tofauti.
Kuna Sehemu nasikia wameongeza 1000 kutoka 1000 yaani jumla 2K huko mikoani watu wanajiongeza Sana huku dsm imeongezeka sh. 100 kila safari.
 
Nchi ya mazingaombwe hii, walishasema kuna wananchi na wenyenchi, wale walamba asali
 
Leo nampa konda mia5
Ananiuliza mia iko wapi? 😂😂
 
Leo nampa konda mia5
Ananiuliza mia iko wapi? [emoji23][emoji23]
Ukitaka angalau ku win hii vita na konda, nibora uwe na nauli yako mkononi unayohisi nihalali kulipa.Ukitoa pesa inayohitaji kurudishiwa chenji basi andika maumivu
 
Hii inchi ya hovyo Sana.

Hivi kwann wasimgesubiri suluhisho ndy wakatoa maamuzi?

Haijawahitokea nauli zipande halafu zikashuka.

Hili liitaleta taabu Sana kwa wanainchi.

Wanaohusika na viwango vya nauli wanapaswa watoke hadharani kukemea hili la nauli kugoma kushuka.
 
Hiyo ruzuku imeenda kuongeza faida kidogo kwa wasafirishaji, siyo kupunguza gharama kwa wadanganyika......hiyo bil. 100 ni bora ingeenda kuchimba visima vijijini.
 
Back
Top Bottom