Wameshaanza sasa ku-profitize na janga la Kariakoo

Kitu ninachojua ukisali ama usiposali, kama uko duniani haya majanga yanaweza kukukuta tu.Kwa hiyo mtu yeyote anayeniaminisha nikisali kwake au nikimrudia Mungu sitaumwa, sitakumbwa na majanga kama lile la Kariakoo ama shida yeyote simuamini (najua tuna uelewa tofauti, ila naamini niko sahihi).
We kama umeamua kumrudia Mungu (Jambo muhimu sana), mrudie, lakini usiwaze kuwa utabarikiwa zaidi kuliko wengine ambao hawana muda na haya mambo.
 
Hakika mkuu
 
Kikubwa wanaume mkeo akienda huko au mpenzi wako akitaka kwenda huko mkataze, akikaza fuvu muonye na akitoa mguu kwenda muambie abakie huko huko asirudi nyumbani na kama ni mpenzi piga chini haraka sana tena usipepese macho maana hawajamaa wanataka kutumia udhaifu wa wanawake zetu kujilimbikizia mali kwa sababu washajua wanawake ni fata upepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…