DOKEZO Wamiliki vyuo vya afya vya City College acheni dhulma na unyonyaji

DOKEZO Wamiliki vyuo vya afya vya City College acheni dhulma na unyonyaji

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

GenZ_Haki

New Member
Joined
Jan 4, 2026
Posts
2
Reaction score
2
Awali, vyuo vya afya na tiba shirikishi vya City Colleges vilivo sajiliwa na NACTEVET kutoa kozi za afya kwa ngazi za astashahada na stashada ikiwemo Kigamboni campus, Temeke & Mikwambi csmpus, Mwanza na Arusha Campus, wamiliki wake ni makada wa ccm akiwemo Abubakari Ali(Boka aliyejitokeza kuchukua fomu ya ubunge Kigamboni) na kundi lake, wamiliki hawa wamekuwa wanyonyaji, wabinafsi na wadhulmati kwa wafanyakazi wa vyuo hivyo.

Pia Wamekuwa wakiendesha vyuo hivo kama Vicoba bila kufata misingi na sheria za uendeshaji wa taasisi za elimu (wanaendesha vyuo kama daycare kwa maslahi yao binafsi bila kujali haki na ustawi wa wanachuo na watumishi wao

1. HAWALIPI MISHAHARA - suala la kulipa mishahara pamoja na maslahi mengine ya wafanyakazi imekuwa sio kipaombele chao. Watumishi hao wamekuwa wakipitia kipindi kigumu sana maana wanaelekea zaidi ya miezi 4 bila kulipwa mishahara (imagine wanadai mishahara ya tokea mwezi wa 8, 9 , 10 , 11 ,12 , wa kitu pekee wanachofanya kuwawekea watumishi kiasi kidogo cha pesa ambacho hakikidhi mahitaji yao na lengo lao ni watumishi hao watakitumia kama nauli tu ili waendelee kuwatumikisha

2. WATUMISHI HAO HAWANA BIMA ZA AFYA - Takriban asilimia 98 ya watumishi wa vyuo hivyo hawana Bima za afya (nhif ) ambapo ni takwa la kisheria la nchi , watumishi hao hata wakiumwa hawana uhakika na matibabu na ukizingatia mishahara yenyewe hawalipwi kwa wakati

3. Vyuo hivi vinaingiza pesa nyingi sana (billions of money ) na wanachuo huwa hawaruhusiwi kufanya mitihani bila kulipa ada , kwahiyo chuo kina uhakika wa ada na kina maelfu ya wanachuo LAKINI CHA AJABU wamiliki wameweka centralized system ya pesa zote kwa vyuo vyote ili watumie pesa zote kwa maslahi yao binafsi bila kujali mustakabali na ustawi wa watumishi na wanachuo

4. Ndugu watanzania tafakari hivi vyuo janja ndio vimepewa dhamana ya kufundisha na kuwaandaa wataalamu wa afya , Je mkufunzi mwenye njaa ambae ana miezi kibao hajalipwa mentality na psychology yake ipoje? Anaweza kufundisha kwa ufasaha na umakini ilihali hana uhakika wa matibabu wala mshahara

5. Wanachuo hao wamekuwa hawaendi kufanya mafunzo kwa vitendo (clinical rotation/field ) kwa wakati licha ya kulipa ada kwa sababu tu misingi mibovu ya vyuo kwa kuhodhi pesa na kushindwa kuwalipia pesa za mafunzo na kuwasifirisha kwa wakati suala ambalo limekuwa likiathiri mafunzo ya vitendo kwa wanachuo

6. Taasisi na vyombo vya serikali vyenye Mamlaka ya kusimamia vyuo hivyo Nactevet, wizara ya elimu na afya , Je, mnasumamia nini Ilihali hamzingatii ubora wa vyuo na haki na maslahi ya wakufunzi na wanachuo? Nactevet mnakagua nini ilihali ukiangalia ratio wakufunzi na course haziendani? Wakufunzi wanakuwa overloaded na hawalipwi

7. Malalamiko na hoja hizi zimetolewa na kwa ujumla na ushirikiano wa watumishi takriban wote wa vyuo hivyo vya City college baada ya kuona shida ni wamiliki hao wamekuwa wabinafsi na hawana nia ya kuwajibika kutimiza haki zao za msingi, wamesisitiza kuwa huu ni mwezi 1 wanafamilia na watoto ambao kimsingi wanahitaji wawalipie ada na kutimiza mahitaji yao ya msingi hivyo wameazimia mambo yafuatayo.

1. WALIPWE MISHAHARA YAO YOTE KATI YA TAREHE KABLA YA TAREHE 9 JANUARY, failure ya kufanya hivo hawatashirika mitihani na shughuli zote za chuo ikiwemo mitihani itakayoanza tarehe 13 January na watachukua hatua zaidi

2. PILI WASIPOLIPWA EARLIER WATAKUJA NA PART 2 YENYE USHAHIDI WA NDANI NA MADUDU KIBAO YANAYOENDELEA CHUONI HAPO (Nactevet, social security funds, paye, contracts, taxes ) pia itaanzishwa movement social media zote
 
SIASA MKURUPUKO SABABU YA ANGUKO CITY COLLEGE TANZANIA
Wamiliki wa CITY COLLEGE TANZANIA(kigamboni,Temeke,Arusha, Mwanza na Dodoma ) ambao pia walikuwa watia Nia kwa nafasi ya ubunge na kushindwa kufanikiwa ( kigamboni) Abubakari Ally na ( Singida ) Baraka Erasto. Wamejikuta kwenye sintofahamu baada ya mambo kuwaendea kombo na kushindwa kuendesha vyuo vyao baada ya kuwekeza kwa Hali na Mali kwenye uchaguzi na kushindwa na kupelekea kushindwa kulipa gharama za uendeshaji na mishahara kwa wafanyakazi wao ( Miezi mitatu+) hivyo kupelekea huduma kusua sua na kudhorota
Tishio kwa taaluma na elimu kwa ujumla
 
Shida nyie wanafunzi huku mnalalamika mnafukuzwa kama hamjalipa ada sijui mnashituliwa mapema, sasa bila kulipa gharama za uendeshaji chuo wao wakalipe mishahala na NSSF kwa pesa zao mfukoni
 
Wamiliki ni makada wa mboga mboga na walijitokeza kuwania ubunge ndani ya chama, mbogamboga ni wanyonyaji
Hivyo vyuo mambo ni shagala bagala. Hata kama una kijana usimpeleke akasoma hapo.
 
Back
Top Bottom