Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Inashangaza sana ndugu zanguni. Unakutana na fremu ina tisheti 2 na jinzi moja lenye mitatuko, pembeni kuna kepu imening'inizwa. Fremu lenyewe la kioo halafu full kiyoyozi. Mhuni aliyepanga fremu hiyo amechili tu akiwa na smartphone yake anaperuzi, muda huo meno nje nje. Nje imepaki BMW
Unaamua kuvuta muda uone kama kuna mteja ataingia lakini wapi. Cha ajabu ukipita kesho unakuta fremu limefunguliwa huku bidhaa ni zilezile nne. Halafu bila aibu anafungua saa 5
Hivi nini hasa ni siri ya urembo?
Kwenye hizo t shirt 2 mnazoning'iniza mwezi mzima ndizo ambazo mnalipia kodi ya fremu?
Na hili nalo Mama akalitazame kwa kina
Naombeni siri ya urembo