Wamiliki wa fremu Sinza zenye tisheti mbili tu na kiyoyozi, tunaombeni siri ya urembo

Kuna dada mmoja ana uzuri wake akiwa mjini na gari yake utadhani labda ana mwanaume anamtunza, ila huyu dada ukimkuta mwanza ziwani akigombana na wavuvi hutaamini, ananuka shombo hafai. Inasemekana ana tenda za samaki za mahoteli makubwa na ana wavuvi wake ziwani hivyo akiwa na tenda anasimamia mchakato wote kuanzia kuparua mpaka kuwapaki ila akiwa mjini hajulikanagi anafanya nini. Huyu ni mfano hai kabisa na ukimuona akiwa dar anaamka na kuendesha gari yake utakachohitimisha ni kuwa anadanga tu ila uhalisia ni dada ni jembe haswa kwenye kupiga kazi na kuchungulia fursa.

Tukiachana na madawa na ufreemason sijui kuuza mwili, pengine huyo mtu anachukua mabelo mjini hapo yanasafirishwa mikoani huko kwa jumla na ana wateja wake singida, iringa, njombe, makambako ambao akipakia mizigo inalipa frem ambayo ni ofisi tu pa kukutania na watu.

Tusikatishwe tamaa na mawazo negative, tuwe positive.
 
Labda TRA
 
Parachute oil is typing
 
Ji
Jichanganye ukaulize Kitu bei utakayoambiwa utakimbia🚶🚶🚶🚶
 
Hizo ni cover up, ni geresha, wana biashara nyingine behind the scene ambazo ni kinyume na sheria za nchi mara nyingi
Exactly!
Hizo kazi huwa ni geresha tu ili kuwazuga watu, wengi wao wanafanya kazi za udhalimu za kificho tofaufi kabisa na hizo wanazozionyesha kwa Watu hadharani.

Nchini Urusi kuhusiana na scenario za namna hii kwa kawaida huwa Wana msemo wao kwamba "an intelligence work is not your primary job in your life, it's a secondary one." Raia wa nchi za nje wanaozuru Urusi ambao hawajui maana ya msemo wao huu mara nyingi Sana huwa wanakuwa Waathirika WAKUBWA au wanakuwa Wahanga wakubwa Sana kwa kupuuzia msemo huu. Wengi wao wahamiaji hao wamekuwa wakirudishwa nchini mwao walikotokea aidha wakiwa wagonjwa, wakiwa madishi yao yameyumba au wakiwa kwenye masanduku baada ya 'kujichanganya hovyo' nchini Urusi.
 
Bro unamaanisha nini katika huo msemo!? Tafadhali nitafunie zaidi 🙏🏾
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…