Wamiliki wa lodge kuweni serious

Nchi ngumu Kila sehemu hii.
 
Ukichungulia uvunguni unakutana ndom mbichi ina mbegu
 
Lodge iwe na turn over ya 180 millions kwa mwaka ?

Hauko serious mkuu.
 
[emoji7][emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 

Hahahaha
 
Hiv hii kwann iki hiv???.. Yan hata kama nimeingia jana saa 8 usiku ila saa 4 mwisho, maana yake nini???
Kuna Lodge nyingine hata ufike saa11 asbh mwisho ni saa4 otherwise usubiri mpk saa4 ndio uchukue chumba, nimekutana nazo hizo Mkoa fulani maana tunasafiri masaa24 unajikuta umeingia huo Mkoa saa10 au 11 asbh sasa umechoka unasema ngoja nichukue room nipumzike unakutana na mwisho saa4
 
Kuna guest ilikuwa pale unaingia Kino studio kama unaelekea Hananasif
1. Chumba unaingia kwa kunyanyua mguu kama vile vizuizi vya mafuriko yasiingie mpaka ndani.
2. pazia halifungi hadi mwisho
3. Switch ya taa ndio ya feni hiyo hiyo. Hapo unachagua uwashe feni kwa hiari huku ukimulikwa kwa lazima na pazia likiwa na upenyo wa chabo, au uzime feni huku ukipata joto kali!

Sema ile guest tulikuwa tunaipenda masela ukichukua room unakabidhi muda kama uliochukua kama vifurushi vya ya kwako tu masaa 24.
 
Aisee umefanya nimecheka sana
 
Mwaka 2007 nilikwenda Korogwe, kulikua na send-off . Baada ya sherehe mishale ya saa sita jamaa yangu akani drop mbele ya Magoma guest house. Wakafungua na kunipa room. Aisee!! Shuka hazijafuliwa, Ile naendelea kuchunguza nikakutana na kunguni wenye njaa, mvunguni mende wametawala. Ilibidi nivue nguo zote ili nisije kubeba mbegu ya chawa wa CCM na kunguni.
Nikilala usingizi wa mang'ang'am haswa.
Kifupi Ni kwamba wasambaa hospitality industry waachieni wakinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…