Wamiliki wa Mabasi waomba Mabasi yaruhusiwe kusafiri kwa Spidi 100 badala ya 80

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
20230724_150539.jpg

Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) mkoani Mwanza kimetaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), kubadili ruksa ya spidi barabarani kutoka kilomita 80 kwa saa hadi 100 kutokana na maboresho makubwa yaliyopo barabarani.

Akizungumza leo Katibu wa Taboa mkoani Mwanza, Anwar Said amesema barabara kwa sasa ni nzuri na pana hivyo kwa kuzingatia uwezo wa mashine za sasa ni vyema spidi ikabadilishwa na kuwa 100.

Aidha, amesema kuna haja ya kuweka vyombo vya kupunguza mwendo badala ya vinavyotumiwa kwa sasa ambavyo haviwezeshi kupunguza mwendo magari hayo bali humsaidia dereva kubaini kazi yake.

“Tunaomba tupate vidhibiti mwendo siyo vidhibiti dereva ili kuimarisha usalama kwa wasafiri wawapo safarini,” amesema Said.
 
Naunga mkono hoja, speed 80 Ilikuwa ni enzi ya barabara mbovu na hata aina ya magari kama kina Leyland. Leo hii barabara zimeboreka na gari ni more sophisticated, kwanini tusiongeze hicho kiwango?
 
Ipunguzwe iwe 60. Kama mtu ana haraka asafiri jana yake.
 
Ikiwa ruhusa itatolewa, basi iwe ni kwa mabasi yanayosafiri umbali wa kuanzia 1,000 km kwa safari moja (Mf Mwanza - Dar, Mbeya- Arusha).
Mtu wa kutoka Iringa -Dar au Dar- Dodoma, hawezi kuwa na haraka kiasi cha kuhitaji bus liruhusiwe kutembea zaidi ya km 80 kwa saa.
Madereva mimi nawajua. Nimesoma nao NIT! Ukiruhusu mabasi yote kwenda mwendo mkali, tutazua majanga.

Kuhusu vidhibiti mwendo, kuna Coaster moja niliendesha, chini ya accelerator kuna kibati chenye screw ya ku adjust kuzuia dereva asichochee sana. Hicho hata wenye kampuni wanaweza kufanya: kuchomelea vibati chini ya accelerator.
 
View attachment 2697833
Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) mkoani Mwanza kimetaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), kubadili ruksa ya spidi barabarani kutoka kilomita 80 kwa saa hadi 100 kutokana na maboresho makubwa yaliyopo barabarani.

Akizungumza leo Katibu wa Taboa mkoani Mwanza, Anwar Said amesema barabara kwa sasa ni nzuri na pana hivyo kwa kuzingatia uwezo wa mashine za sasa ni vyema spidi ikabadilishwa na kuwa 100.

Aidha, amesema kuna haja ya kuweka vyombo vya kupunguza mwendo badala ya vinavyotumiwa kwa sasa ambavyo haviwezeshi kupunguza mwendo magari hayo bali humsaidia dereva kubaini kazi yake.

“Tunaomba tupate vidhibiti mwendo siyo vidhibiti dereva ili kuimarisha usalama kwa wasafiri wawapo safarini,” amesema Said.
Hii ni speed ya kawaida kabisa kwa barabara za lami na pia kwenye yale maeneo ya speed 50 yafanywe soeed 60/khr.
Hizi speed ndogo ndio zinaletaga uchovu kwa dereva kusinzia hasa wale wa long journey.
 
Mtu mweusi kichwa chake hakipo vizuri ndio maana anawekewa matuta barabarani Acha waende speed 80km/h kuwapa hii 100 ni kutafuta ajali mbaya.
 
Hiyo speed yenyewe waliyowekewa hawaitekelezi, wanakwenda over 90/hr. Waendelee kudhibitiwa tu kwani miundombinu yetu bado hairuhusu kuendesha over 80/hr
 
View attachment 2697833
Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) mkoani Mwanza kimetaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), kubadili ruksa ya spidi barabarani kutoka kilomita 80 kwa saa hadi 100 kutokana na maboresho makubwa yaliyopo barabarani.

Akizungumza leo Katibu wa Taboa mkoani Mwanza, Anwar Said amesema barabara kwa sasa ni nzuri na pana hivyo kwa kuzingatia uwezo wa mashine za sasa ni vyema spidi ikabadilishwa na kuwa 100.

Aidha, amesema kuna haja ya kuweka vyombo vya kupunguza mwendo badala ya vinavyotumiwa kwa sasa ambavyo haviwezeshi kupunguza mwendo magari hayo bali humsaidia dereva kubaini kazi yake.

“Tunaomba tupate vidhibiti mwendo siyo vidhibiti dereva ili kuimarisha usalama kwa wasafiri wawapo safarini,” amesema Said.
Wehu hao, kwa barabara zipi? Zingekuwa four ways kidogo ningewaelewa. Nimekaa Uingereza, pamoja na barabara zao nzuri, mabasi hayazidishi spidi 80.
 
Back
Top Bottom