Wamiliki wa maduka ya uwakala wa mabenki na chuma ulete

Wamiliki wa maduka ya uwakala wa mabenki na chuma ulete

Kwamba chuma ulete ndiye aliyesababisha uandike 200k badala ya 20k??.
Kuwa makini.
Alafu inavoonekana tayari unaamini katika uchawi so endelea kuamini katika uchawi huo huo.
 
Unahitaji kuwa Mpumbavu kuamini kwenye huo ujinga.

Sidhani hata kama wewe Mwenyewe unaweza kufafanua maana ya huo ujinga unaoitwa chuma ulete.

Biashara yoyote ina sheria na kanuni zake...ndio maana tumekuta Watu wanapewa elimu ya kutunza vitabu.

Laiti kama Biashara ingekuwa ni suala tu la kutoa na kupokea pesa sidhani kama Watu wangeumiza vichwa kutengeneza kanuni na sheria za kihesabu kusimamia hayo mambo yanayohusiana na kutoa na kupokea pesa.

Mangi Mwenye mafanikio pale Mtaani huenda hajamaliza hata Darasa la saba na hana Elimu rasmi ya kutunza Vitabu, lakini ukichunguza utagundua kuwa ana 'practice' kanuni hizo hizo ila kwa namna yake mwenyewe...tofauti tu ni huenda ya kwake ikawa inahitaji nguvu nyingi kuliko kama angekuwa anafuata kanuni za kufundishwa darasani...ingawa huenda naye anapata matokeo chanya kama ya yule anayetumia kanuni za darasani.

Msingi wowote wa Shughuli unayoifanya ni kuzijua kanuni zake vizuri...kinyume cha hapo hata kama ugekuwa unasonga ugali ukikosa matokeo uliyotarajia utaishia kusingizia umelogwa.

Tafuta Watu wakuelekeze namna ya kuendesha hizo shughuli...tuache ujinga.
 
Back
Top Bottom