Wamiliki wa Malori Kenya walia na Standard gauge railway

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Hali hii imekuja baada ya SGR ya Kenya kuanza kazi kwa ufanisi wa hali ya juu sana na gharama za chini mno ukilinganisha na malori, Video inajieleza.
Je, tumejiandaa vipi kupambana na hawa wa kwetu ili wasije kuihujumu SGR yetu kama walivyoihujumu CGR ya TAZARA?
 
Zingekuwa habari za kulawitiwa baba yake Mange Kimambi tungeshakuwa page ya 10 sasa hivi kwenye thread, stupid
Relax....
Umeweka taarifa ambayo imejitosheleza haihitaji mjadala....
JPM nia yake ya kusafirisha mizigo kupitia treni ilikua ya muda mrefu ili kuokoa fedha zinazoenda kwenye barabara... Na naamini wananchi na serikali wanaelewa hujuma za wenye malori na wamejiandaa kupambana nazo.... Kila maendeleo huja na vicheko na vilio kwa pamoja tatzo ni for how long.....
 
Mkuu umewahi kusoma huu uchambuzi wa wiki iliyopita wa The East African

Kenya’s SGR cargo volumes cast doubt on its viability

Japokuwa wenye malori wanalia lakini long run benefit za SGR ya Kenya zinaleta mashaka, hii inaweza kuwa case study kwetu pia

 
Lakini mzigo ukifika Nairobi inabidi ukodi Lori tena mpaka eneo husika,tofauti na malori.
 
Ila faraja yangu zaidi ni kuwa treni yetu itatumia umeme tofauti nanya Kenya ambayo nadhani inatumia diesel, hii maana yake ni kwamba gesi yetu ya Songosongo inayotumika kuzalisha umeme pale Kinyerezi itapata soko zaidi na kupunguza fedha za kigeni matrillion kwa matrillion zinazotumika kuagiza mafuta ya diesel kuendeshea malori, hii itaimarisha sana shillingi. Ila wasiwasi wangu upo kwa hawa waarabu koko wenye malori, je, wataiacha salama SGR au wataifanyia hujuma na kuiulia mbali kama walivyoihujuma na kuiua kwa makusudi TAZARA cape gauge railway? Tumejipanga vipi? Maana hawashindwi kupigisha shoti transformer zote za hiyo treni ili ife kabisa!
 
Kumbuka ya kwetu itatumia umeme, nimefafanua kwenye post namba 8. Na bila shaka hizo habari na tafiti ni propaganda za wenye malori.
 
Lakini mzigo ukifika Nairobi inabidi ukodi Lori tena mpaka eneo husika,tofauti na malori.
Sawa, lakini ni sawa na bandari ya nchi kavu inavyofanya kazi, ni kwamba unaondoa msongamano mjini kwa kutoingiza malori mengi mjini kufuata mzigo bandarini bila sababu za msingi, pia ni cheaper zaidi.
 
Hii itawaweka macho wamiliki wa malori tz kuanza mchakato waktafuta biashara nyingine yakufanya .

Ndio hivyo maendeleo huja na changamoto zake, lakini mwishowe watu watazoea tu hali ya madiliko
 
Haya ni mazingaombwe ndugu. Umeme hatuna wa kueleweka so turnover ya hiyo project sijui inatoka wapi mradi utageuka white elephant kama ilivyo kampuni ya ndege Tanzania. Imebaki kusifia ingali hakuna faida
 
Haya ni mazingaombwe ndugu. Umeme hatuna wa kueleweka so turnover ya hiyo project sijui inatoka wapi mradi utageuka white elephant kama ilivyo kampuni ya ndege Tanzania. Imebaki kusifia ingali hakuna faida
Nasikia hiyo treni ni hybrid, yaani unaweza ukwasha engine ya diesel pindi umeme unapoleta shida, na kuhusu umeme nasikia mradi wa Kinyerezi Phase 2 umeshakamilika kwa 90%, meaning an increase of 240MW exclusively dedicated for the SGR, in the long run tunakuwa tunaokoa fedha za kigeni zilizokuwa zitumike kuagiza diesel toka uarabuni na badala yake tuna-utilise natural gas ambayo tunayo nyingi sana! Kumbuka, we have several comfirmed Trillion Cubic Feet (TCF) of natural gas reserves.
 
Ishu ni kuwa tumejiandaa vipi kimiundombinu na swala la umeme? Is it reliable? Hivi kwa nini mvua ikinyesha na umeme unakatika? Is it coincidence au ni ubovu wa miundombinu?
 
Ishu ni kuwa tumejiandaa vipi kimiundombinu na swala la umeme? Is it reliable? Hivi kwa nini mvua ikinyesha na umeme unakatika? Is it coincidence au ni ubovu wa miundombinu?
Nadhani miundo mbinu ya SGR itakuwa madhubuti sana
 
Mimi naona kwa utawala huu ikibainika kuna MTU anahujumu miundombinu ya reli, hakuna mjadala anakamatwa na zinataifishwa Mali zote anazomiliki apo ndio mambo yataenda
Tanzania ni donar country tulitakiwa kutoa misaada nchi za ulaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…