Ila faraja yangu zaidi ni kuwa treni yetu itatumia umeme tofauti nanya Kenya ambayo nadhani inatumia diesel, hii maana yake ni kwamba gesi yetu ya Songosongo inayotumika kuzalisha umeme pale Kinyerezi itapata soko zaidi na kupunguza fedha za kigeni matrillion kwa matrillion zinazotumika kuagiza mafuta ya diesel kuendeshea malori, hii itaimarisha sana shillingi. Ila wasiwasi wangu upo kwa hawa waarabu koko wenye malori, je, wataiacha salama SGR au wataifanyia hujuma na kuiulia mbali kama walivyoihujuma na kuiua kwa makusudi TAZARA cape gauge railway? Tumejipanga vipi? Maana hawashindwi kupigisha shoti transformer zote za hiyo treni ili ife kabisa!