Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Nchini Tanzania (TATOA), Elius Lukumay, amesema wamiliki wa malori wako tayari kuyapaki magari yao endapo mamlaka zitaendelea kuwachukulia hatua wasafirishaji bila kuwashirikisha katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 18, 2026, Lukumay amesema TATOA haipingi taratibu za maegesho, bali inapinga utekelezaji unaofanyika kwa kuwanyang’anya madereva vibao vya namba za magari barabarani, akisisitiza kuwa suala hilo linapaswa kutatuliwa kupitia mazungumzo kati ya Serikali na wadau.
“Tuko tayari kuyapaki malori. Kauli ambayo mimi sijawahi kupenda kuitumia katika muda wangu wote wa uongozi, lakini kama inatufikisha hapo, tuko tayari kuyapaki tuzungumze,” amesema.
Amesema sekta ya usafirishaji imewekeza fedha nyingi na ina mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania, ikiwemo kuhakikisha mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam inafikishwa ndani ya nchi na katika mataifa jirani yanayotegemea bandari hiyo.
Lukumay amewataka viongozi wa Serikali katika maeneo yanayohusika na shughuli za usafirishaji kutumia vyama vya wamiliki wa malori kama sehemu ya majadiliano kabla ya kuchukua hatua dhidi ya wasafirishaji.
Amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kuepusha migogoro na kuhakikisha sekta ya usafirishaji inaendelea kuchangia ukuaji wa uchumi pamoja na ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.