Engine za GDI zinatengeneza uchafu sana aina ya carbon kwenye engine. Na hii ikizidi engine inakosa power, gari kuwa na miss na kuzima zima na baadae inaweza engine inaweza kuharibika kabisa.
Chukua tahadhari: mwenye GDI iliyofika mileage 100000km au zaidi, nunua dawa "complete fuel system cleaner" na umwagilie kwenye tenki lako la petroli halafu jaza mafuta (FUATA MAELEKEZO YALIYOKO KWENYE CHUPA YA DAWA HIYO".
Ukirudia kufanya hivi kama marambili kwa kila kabla ya oil service (yaani 5000km) sio mbaya.
Dawa utazipata kwenye maduka ya oil za gari kama lumumba na livingstone.
Angalizo:natoa ujuzi tu na siko kwa ajili ya matangazo ya kibiashara