Wamilki wa Mbwa, hivi hua mnawaza nini unaona mtu anakaribia kung'atwa na unamuambia asijali?

Wamilki wa Mbwa, hivi hua mnawaza nini unaona mtu anakaribia kung'atwa na unamuambia asijali?

Pantomath

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
842
Reaction score
3,449
Hawa watu hua najiulizaga, akili zao wote zinafanana, Mazoea yao na mbwa wao wanachukulia kila yule anayo..

Mtu dude unaona kabisa linakuja kwa kasi, unajichekesha tu "hahahaaaa usijali hang'ati" unamsemea mbwa? Hakuna mbwa anayekuja kwa Mgeni(anaamini ni adui) kwa kukukimbilia na kubweka asiwe na nia ya kung'ata, kinachosaidia wengi ni reactions tuu.

Ili mtu usionekane mwoga au umepanic,
Unamwambia mwenyeji kwa Sauti ya kawaida "Oya mzuie basi" ila kiuhalisia hio tune haijatoka ndani, halafu mbaya zaid mbwa wapo wawili, mmoja kakuzunguka, Halafu simple tuu analeta uzungu kwa ma mbwa koko eti "Tom njoo uingie bandani" ,"leo nimechelewa kuwafungia".

Dude limepaa, mdomo kama jagi, unaniambia nisiogope?, hapo hapo nikaona kuna kuku mkubwa tuu kafa manyoya nyoya yametoka na damu (nikahisi kabisa yule ni mbwa) nikauliza yule kuku pale vipi? Akazuga. Ndio najua sipaswi kukimbia, hilo kosa siwezi fanya ila tatizo nipo katikati, halafu kuna dude jingine limezunguka nyuma lenyewe halibweki, huyu wa mbele yupo serious hana mchezo.

Anyway " nilisogea kiubavu ubavu Nikaokota Chungu cha Maua nikamtandika nacho cha ubavu, Mbio zake kuelekea bandani na lile yowe Yule mwingine sikumona alipotelea wapi, na kelele za kuku bandani, Wote wakatoka nje wanauliza kuna nini? Eti kisa mbwa kalia, wakati anabweka kwa nini wasiulize?
Anyway Amani ikatoweka na biashara iliishia pale pale, wanaita sikurudi nikasepa. Potelea kote.
 
Wapuuuzi sana Mkuu, wanathamini mbwa kuliko binadamu. Biashara ya Home delivery ni ngumu dunia nzima mkuu. Hujaskia huko mambele Vampire wanavyowageuza mishikaki hasa sie ngozi nyeusi! Dog anaugulia maumivu ya chembe ya mbavu huko.
 
Waswahili kuliko kumfanyia Home Delivery, ni Bora umpunguzie bei..

Mara apotee hewani,
Akupole, umefika akuambie punguza bei,
Haya mara mbwa, mwisho wa siku akuroge wewe ndio umpe mzigo na umlipe.
😂😂😂
 
😁 unabahati walikuwa mbwa Koko og,siku ukikutana na Shepard aliyevutishwa ndumu usijaribu mkuu.
 
Ulipompiga ubavuni akabweka huo ndo uanaume. Ukiona upo hatarini kiasi kwamba usipopambana unakufa na ukipambana unajeruhiwa na kuwin game, pigana Kwa nguvu zote utashinda.
 
😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜
 
Hakuna mbwa mkali mkuu….hata nyoka hayupo mkali….kiumbe yoyote ukishaonyesha kuogopa lazima nae ajihami
Usije kujidanganya hili, ondowa hayo mawazo, tena kama ile mimbwa yenye sura mbaya bulldog yana tabia za kupoteza memory zinamshambulia na kumuuwa mmiliki wa hayo mambwa.

Kuna wengine wakicheleweshewa ratiba ya chakula ukiwapekekea chakula wanaanza na wewe.

Kwa kifupi mbwa siyo mfugo wa urembo ni kwa security purpose tu na wanatakiwa kufungiwa muda wote wote na kufunguliwa usiku tu.
 
Usije kujidanganya hili, ondowa hayo mawazo, tena kama ile mimbwa yenye sura mbaya bulldog yana tabia za kupoteza memory zinamshambulia na kumuuwa mmiliki wa hayo mambwa.

Kuna wengine wakicheleweshewa ratiba ya chakula ukiwapekekea chakula wanaanza na wewe.

Kwa kifupi mbwa siyo mfugo wa urembo ni kwa security purpose tu na wanatakiwa kufungiwa muda wote wote na kufunguliwa usiku tu.
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom