Wana CCM tuambieni Tanzania ilipata uhuru tarehe, mwezi na mwaka gani?

Wana CCM tuambieni Tanzania ilipata uhuru tarehe, mwezi na mwaka gani?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Imekuwa kawaida viongozi wa CCM kupotosha ukweli kuhusu hoja ya Uhuru. Kwenye hotuba zao nyingi wamekuwa wakiiambia Dunia kwamba Tanzania ilipata uhuru tarehe 09/12/1961. Na hata tunaposherekea sikukuu ya Uhuru Naamini tutegemee kuendelea kusikia upotoshaji ukifantywa na wasomi wa Nchi hili.

Tarehe 9/12/1961 ninavyofahamu mimi hakukuwa na Tanzania. Tanzania ni matokeo ya muungano wa Nchi mbili huru ambazo ni Tanganyika iliyopata Uhuru 09/12/1961 pamoja na Zanzibar.

Kwa muktadha huo ni vyema Wana CCM watakupa ushahidi wa Tanzania kupata Uhuru au waamue kutubu na kutamka ukweli kwamba Tarehe 09/12/1961 ni Siku ya Tanganyika kupata Uhuru. Tuache ujanja ujanja wakijinga unaodumaza fikra zetu Kwa kivuli Cha uzalendo
 
Hivi Zanzibar wanaikumbuka siku yao kama siku ya Mapinduzi Tanzania au Zanzibar ni fundo tu.
 
Wanabodi, leo ni tunasherehekea miaka 60 ya uhuru wa Tanzania na sio Tanganyika, kwa sababu maandimisho ni present, kilichopo sasa!, japo ni kweli iliyopata uhuru ni Tanganyika, which doesn't exist any more, kilichopo sasa ni Tanzania, tunasherehekea uhuru wa Tanzania.

Jee wewe mkuu usomae hapa, ile siku ulipozaliwa, jee unajua ulizaliwa bila jina?, unaposherehekea siku yako ya kuzaliwa, jee unasherehekea siku ya kuzaliwa yule mtoto aliyezaliwa siku ile bila jina, au huyu aliyepo mwenye jina?!.

Na kama ni mwanamke, anakuwa na Maiden Name, akiolewa ana change name, kuasume jina la mumewe, tuseme umeolewa na Pasco, hiyo, sasa ameolewa anaitwa Mrs. Pasco, siku ya kuadhimisha birthday yako tutaadhimisha siku ya kuzaliwa ya Mrs. Pasco, sio binti fulani wala ya yule mtoto asiye na jina!.

Tanganyika was an area with a Name Tanganyika. Now that name doesn't exist any more, kilichopo sasa ni Tanzania Bara, na eneo la ilipokuwa Tanganyika ndio eneo la Tanzania bara!.

Hivyo leo kumbukumbu ni ya uhuru wa Tanganyika, lakini maadhimisho na kusherehekea ni uhuru wa Tanzania Bara kwa kifupi Tanzania

Pasco.
Wajameni ni katika kukumbushana tuu kuwa maadhimisho ya leo ni ya Uhuru wa Tanzania, na sio wa Tanganyika!.

Nawatakia sikukuu njema ya Uhuru na Jamhuri.

Paskali
 
Tarehe 6 mwezi wa 12 wakati huo Machaga wa Ufipa wakiwa wanawinda kuiba mbege. Mpaka kiongozi waoachagga akamwagiwa mbege iliyochacha akawa ma makengeza usoni.
If you have nothing to comment, you better keep quiet rather than writing nonsenses
 
Wajameni ni katika kukumbushana tuu kuwa maadhimisho ya leo ni ya Uhuru wa Tanzania, na sio wa Tanganyika!.
Nawatakia sikukuu njema ya Uhuru na Jamhuri.
Paskali
Mdogo wangu Paschal nimeona unaungana na hoja ya Uhuru wa Tanzania SIYO Tanganyika. Naomba utusaidie kujua mambo yafutayo;
1. 9/12/1961 kulikuwepo na Tanzania?
2. Je Tanganyika au Tanzania Bara imewahi kubadili jina ikajiita Tanzania? If yes,lini na kwa hati gani?
3. Tukisema Uhuru wa Tanzania tunamaanisha hata Zanzibar walipata Uhuru wao 9/12/1961?
4. Kama Zanzibar inatarehe yake yakupata Uhuru ambayo naamini ni siku ya Mapinduzi, tunasemaje Tanzania ilipata Uhuru mwaka 1961 tukijua kilichopata Uhuru ni sehemu tu ya Tanzania ambayo ni Tanganyika?
5. Kwa uelewa wako Mapinduzi ya Zanzibar yanaweza kutambua kama siku ya Uhuru ya Zanzibar?
6. Hoja Yako ya kusherekea ya Sasa ( present) umeitoa kwenye nyaraka gani?

Nauliza haya baada ya kuona mada zako zote zimeacha lakuna kwenye maeneo hayo: Nikutakie siku njema ya Uhuru wa Watanganyika
 
Kikubwa kuondoa utata..ni kwenda kwenye katiba kubadili..Penye Tanganyika..pasomeke Tanzania bara. Si ndyo furaha yao? Mana neno Tanganyika panawapa kichefuchefu
 
Imekuwa kawaida viongozi wa CCM kupotosha ukweli kuhusu hoja ya Uhuru. Kwenye hotuba zao nyingi wamekuwa wakiiambia Dunia kwamba Tanzania ilipata uhuru tarehe 09/12/1961. Na hata tunaposherekea sikukuu ya Uhuru Naamini tutegemee kuendelea kusikia upotoshaji ukifantywa na wasomi wa Nchi hili.

Tarehe 9/12/1961 ninavyofahamu mimi hakukuwa na Tanzania. Tanzania ni matokeo ya muungano wa Nchi mbili huru ambazo ni Tanganyika iliyopata Uhuru 09/12/1961 pamoja na Zanzibar.

Kwa muktadha huo ni vyema Wana CCM watakupa ushahidi wa Tanzania kupata Uhuru au waamue kutubu na kutamka ukweli kwamba Tarehe 09/12/1961 ni Siku ya Tanganyika kupata Uhuru. Tuache ujanja ujanja wakijinga unaodumaza fikra zetu Kwa kivuli Cha uzalendo
Tulishapigwa na kitu kizito toka Lumumba. Tuwe wapole tu.
 
Hao unaowauliza sijui kama wameelewa swali. Hawakawii kuporomosha matusi na kejeli. 😄😄😄
 
Imekuwa kawaida viongozi wa CCM kupotosha ukweli kuhusu hoja ya Uhuru. Kwenye hotuba zao nyingi wamekuwa wakiiambia Dunia kwamba Tanzania ilipata uhuru tarehe 09/12/1961. Na hata tunaposherekea sikukuu ya Uhuru Naamini tutegemee kuendelea kusikia upotoshaji ukifantywa na wasomi wa Nchi hili.

Tarehe 9/12/1961 ninavyofahamu mimi hakukuwa na Tanzania. Tanzania ni matokeo ya muungano wa Nchi mbili huru ambazo ni Tanganyika iliyopata Uhuru 09/12/1961 pamoja na Zanzibar.

Kwa muktadha huo ni vyema Wana CCM watakupa ushahidi wa Tanzania kupata Uhuru au waamue kutubu na kutamka ukweli kwamba Tarehe 09/12/1961 ni Siku ya Tanganyika kupata Uhuru. Tuache ujanja ujanja wakijinga unaodumaza fikra zetu Kwa kivuli Cha uzalendo
kwa kweli jambo nalojiuliza kila siku hivi ni kweli tanzania ilipata uhuru? ama tanganyika ndio iliyopata uhuru jamani ukweli usemwe kua hakuna nchi duniani iliyopata uhuru inayoitwa wa tanzania au tanzania bara...kwani tukisema tanganyika ni dhambi?
 
Back
Top Bottom