Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Nawatakia mapumziko mema ya kumbukumbu ya siku uhuru na jamhuri ya nchi iliyokuwa Tanganyika sasa Tanzania。Tarehe 9 Desemba 1961 Tanganyika ilipata uhuru toka kwa mkoloni Mwingereza,9 Desemba 1962 ikawa jamhuri。 Tarehe 26 April 1964 ikaungana na Zanzibar na kubadili jina na kuwa Tanzania,hivyo leo tunapoadhimisha siku hii,ile Tanganyika iliyopata uhuru wake siku hii sasa haipo tena,iliyopo ni Tanzania hivyo kumbukumbu ndio ya Tanganyika lakini maadhimisho ni ya Tanzania。Imekuwa kawaida viongozi wamekuwa wakiiambia Dunia kwamba Tanzania ilipata uhuru tarehe 09/12/1961.
Tarehe 9/12/1961
Kwa muktadha huo ni ukweli kwamba Tarehe 09/12/1961 ni Siku ya Tanganyika kupata Uhuru.
Heri ya Uhuru na Jamhuri。
P。