Wana CCM tuambieni Tanzania ilipata uhuru tarehe, mwezi na mwaka gani?

Sasa ndio naelewa kwa nini Laurent Kabila baada ya kuufurumusha utawala wa Mobutu alilifuta jina la zaire na kuriludisha jina la zamani Congo.

Ipo siku tu Tanganyika ni lazima irudi.
 
Huyu Pascal Mayalla sina hakika kama alikuwa serious. Possibly hoja yake ilikuwa ni some sort of jokes...

Kama ataitikia wito wa kuja kujibu maswali hayo, hebu tumwongezee na haya;

1. Baada ya muungano wa 26/4/1964 kati nchi mbili huru Tanganyika na Zanzibar, Tanganyika alibadilisha jina na kuanza kuitwa "TANZANIA BARA". Zanzibar mpaka leo hawakubali identity mpya ya kuitwa " TANZANIA VISIWANI" Bali siku zote wabebaki na original identity ya nchi yao yaani "ZANZIBAR" na watu wao wanajulikana kama "WAZANZIBARI" na kamwe siyo "WATANZANIA".

Unadhani ni kwanini hali hii iko hivi bwana Pascal Mayalla..?

2. Tunafahamu kuwa nchi ya TANGANYIKA ilipata uhuru wake wa bendera toka kwa waingereza tarehe 9/12/1961. Na vivyo hivyo tunafahamu kuwa nchi ya ZANZIBAR ilipata uhuru wake 12/2/1964. Na siku zote kwa Wazanzibari inapofika tarehe hii, husherekea kumbuizi la uhuru wao iitwayo " SIKU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR"

Mbona sisi tunasherekea kumbuizi ya Uhuru wa nchi ambayo haikuwahi kuwepo inagalau kabla ya 1964..? Unadhani ni kwanini tunajirisha uongo na uzandiki...?
 
Tunaishi kiujanjaujanja tu
 
Hakika ni upotoshaji kiwango Cha lami.
 
Nadhani hizi ni mathematics za ^proportionality & infinitesimals:^

T + Z = T (given Z B]
Kwa tafsiri kwamba;
Tanganyika jumlisha Zanzibar jibu ni Tanzania. Ila zingatia kwamba Zanzibar ni kinchi kidooogo sana kilichomezwa na Tanganyika kuuuubwa. Kwahiyo zanzibar ni kama haipo tena kwa maana ya kujitegemea kama inchi
 
Tar 12/01/1964
 
Ngoja Paskali aje 🤣🤣🤣
 
Wanapotosha UMMA mwaka 1961 hakukuwa na Nchi inayoitwa TANZANIA
 
Hili suala la Uhuru wa Tanganyika au Tanzania limetrend sanaaa hebu nielekezeni Kwanza inakuajeee hapo
 
Wajameni ni katika kukumbushana tuu kuwa maadhimisho ya leo ni ya Uhuru wa Tanzania, na sio wa Tanganyika!.

Nawatakia sikukuu njema ya Uhuru na Jamhuri.

Paskali

Nawatakia maadhimisho mema ya siku ya Uhuru na Jamhuri, nikiendelea kusisitiza, kumbukumbu ndio kumbukumbu za uhuru wa Tanganyika, lakini maadhimisho ni maadhimmisho ya uhuru wa Tanzania. Darsa: Maadhimisho ya Leo, ni ya Uhuru wa Tanzania, yaani, Tanzania National Day, ila Kumbukumbu Ndio ya Uhuru wa Tanganyika!
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…