Wana CCM tuambieni Tanzania ilipata uhuru tarehe, mwezi na mwaka gani?

Imekuwa kawaida viongozi wamekuwa wakiiambia Dunia kwamba Tanzania ilipata uhuru tarehe 09/12/1961.
Tarehe 9/12/1961

Kwa muktadha huo ni ukweli kwamba Tarehe 09/12/1961 ni Siku ya Tanganyika kupata Uhuru.
Nawatakia mapumziko mema ya kumbukumbu ya siku uhuru na jamhuri ya nchi iliyokuwa Tanganyika sasa Tanzania。Tarehe 9 Desemba 1961 Tanganyika ilipata uhuru toka kwa mkoloni Mwingereza,9 Desemba 1962 ikawa jamhuri。 Tarehe 26 April 1964 ikaungana na Zanzibar na kubadili jina na kuwa Tanzania,hivyo leo tunapoadhimisha siku hii,ile Tanganyika iliyopata uhuru wake siku hii sasa haipo tena,iliyopo ni Tanzania hivyo kumbukumbu ndio ya Tanganyika lakini maadhimisho ni ya Tanzania。
Heri ya Uhuru na Jamhuri。
P。
 
Mbona Zanzibar mapinduzi day haiitwi "Mapinduzi ya Tanzania Visiwani"!? Tanganyika ipo ( ambayo ni Tanzania isiyo na Zanzibar) na Zanzibar ipo ( ambayo ni Tanzania isiyo na Tanganyika) . Ccm jaribuni kuachana na huu upumbavu wa kujifanya kuwa Tanganyika haipo. Tanganyika hakuna sehemu iliwahi badili jina. Hakuna. Sema TU Kuna nchi ambayo inaitwa Tanzania ambayo ni Muungano wa Tanganyika Na Zanzibar.
 
Haya maswali atayajibu kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…