Habari za Muda huu wana Jfs.
Ni muda sasa wa takribani mwezi kumekuwa na introduction ya kile kinachoitwa tozo ambapo kwa mujibu wa Mh Rais Samia kupitia Waziri Wake Dr Mwigulu nchemba na wabunge wake wanadai ni kwa ajili ya solidarity funds ili kusaidia miradi mbali mbali ya kijamii kama elimu na afya.
Baada ya watanzania wengi kulalamikia njia hiyo iliyokinyume na sheria za kodi Dr Mwigulu Nchemba aliwataka wananchi kuungana kwa pamoja kufanikisha jambo hili. Na kwamba yeyote anayeona kero kuchangua maendeleo ya nchi yake ni bora aanze mapema ahamie Burundi.
Haikuishia hapo zikaja tozo za simu na miamala, wanaccm wengi kwenye mitandao ya kijamii whatsapp, twitter, instagram, facebook na telegram wamelalamika sana kupita maelezo kiasi cha kuanza kutukana mamlaka zilizoko madarakani huku wakilinganisha na mamlaka ya awamu ya tano. Kilio cha kufa na kupona kimeanza baada ya kuongeza tozo kupitia mfumo wa kununua umeme wa LUKU hapa ndio wakazidi kuchanganyikiwa.
Msingi wa kuchanganyikiwa kwao ni kwa sababu
1. Moja hawakutarajia serikali yao ambayo 90% ya viongozi wao walipita bila kupingwa kuwafanyia unyama huu.
2. Waliamini Mama ni sawa na Mwendazake hivyo ataendelea kuwadekeza
3. Waliaminishwa uchumi wa nchi uko vizuri sasa wanashangaa matozo ya nini.
4. Wanaamini mfumo ulioko madarakani sasa una lengo la kurudisha ufisadi wa wazi ( ikumbukwe ufisadi wa magufuli ulikuwa mkubwa na wa kificho sana).
Wito kwa wanaccm popote mlipo badala ya kutupigia kelele sisi ambao ni wazalendi kweli kweli na tuko tayari kuchangia maendeleo ya nchi ni vema mkapinga kwa vitendo ikiwemo kuingia mabarabarani kuonesha hisia zenu Ni haki yenu kikatiba kupinga pale haki zenu mnapohisi zinavunjwa.
Ukweli daima, unafiki kwangu mwiko. Tudumishe itikadi hii.