MBUNGE WETU MOSHI VIJIJINI ACHA KUOGOPA KIVULI CHAKO
Mh. Sana, Daktari Cyril chami, mbunge mtukufu wa jimbo la moshi vijijini, nakuandikia waraka huu nikiwa na matumaini kuwa utausoma kwa makini na kuulewa badala ya kukurupuka na kumwagiza anayeitwa msaidiizi wako maalumu kunijibu.
Ninakuandikia kukuonya mapema kuwa mwaka 2010, siyo mbali, kama ukilinganisha na safari ya kutoka moshi kwenda dare s salam mlioianza mwaka 2005, sasa mmeshafika njia panda ya segera. Hivyyo kujidanganya kuwa bado upo muda ni sawa na kumdanganya mt0to kwa pipi ili alale.
Ninakuandikia nikikkukumbusha kuwa mwaka 2005, ilibidi uongozi wote kitaiifa uhamie moshi vijijini kukunusuru, wananchi waliamua kukupa kura za huruma na kwa bahati mbaya, umeligawa jimbo kwa misingi ya ukabila.
Wakati wananchi wa uru mawela , wakilalamika kwa ngazi zote kuhusu kudhulumiwa kwa ardhi yao , na majengo waliompangisha mwekezaji aitwaye laitolya tours, kiasi kwamba mwekezaji huyu hataki kulipa kodi ya pango kwa miaka 12 sasa, huku akisaidiwa na baadhi ya viongozi kutengeneza hati miliki hivyo kuwadhulumu wananchi hawa, wewe umekaa kimyaa kabisa, na wala hutaki kujiingiza kwenye mgogoro, labda unafaidi toka kwa mwekezaji au kwako matatizo ya wananchi wa uru hayana nafasi. Huko kibosho unakotoka mgogoro mdogo wa ardhi kati ya wananchi na chuo kule mweka uliufungia safari toka dar es alam ukautatua kwa muda mfupi sana. Mweka ni kama nusu kilomita toka uru mahali ambako wananchi wanavutana na kutishiwa kuuawa na mwekezaji. Nawe ukekaa kimya hali ukijua kama mwekezaji yule angebanwa akalipa kodi anayodaiwa kama 467m, pesa hizo zingetosha kufanya maajabu kieleimu na afya kwa tarafa zima ya uru. Mwekezaji yule anavuna mamilioni kila kukicha na ukweli ni kuwa anao uwezo wa kulipa kiasi hiki, ila kiburi unampa wewe na wenzako huko serikalini.
Mwaka juzi, uliahidi wananchi wa uru mawela kuwa utamleta balozi wa japan, ambaye angesaidiana kiufadhili na wanachi kujenga kidato cha tano na sita katika shule yetu ya mawela. Kwa masikitiko makubwa ukampeleka kwako kibosho, wakati kule mawela wananchi walikuwa wanakusubiri hadi giza hukutokea! Badala yake baadaye ukawajibu kuwa eti serikali ina mpango wa kujenga shule za kidato cha tano na sita hivyo wasubiri. Ni nani asiyejua kuwa mipango ya serikali inachukua muda mrefu? Kwa nini balozi aende kujenga shule kibosho, na uru wa subiri serikali?
Mheshimiwa , labda nikukumbushe tu kuwa, barabara ya uru iliahidiwa kuwekewa lami, barabara ile ina urefu wa kilomita 20. naona utapeli umeanza wa kuweka mita 300 kila mwaka, na sasa wako pale rau kama mita 700 toka mjini, hii danganya toto haitawafanya wananchi wa uru waamini kuwa eti unatimiza ahadi. Tunachotaka ni barabara ijengwe yote kilomita 25 kabla ya mwaka 2010, la sivyo hakuna cha ngawaiya kuzunguka na wewe au yeyote kukuombea kura. Mambo ya kudanganywa na rangi za bendera za vyama vya siasa sio uru, mkajaribu mahali pengine.
Mheshimiwa sana mbunge na waziri. Wananchi wa moshi vijijini hatutaelewa somo lolote kama ahadi zako hazitatimia kuhusu hasa elimu, majji, ajira nakadhalika. Kamwe usihangaike kuandika litania za mambo uliyofanya ukidanganywa na wasaidizi wako, wananchi hawataangalia makaratasi, bali kama ni lami ionekane barabarani, na kama ni maji yaonekane yanatiririka. Ngonjera tulishazichoka
Mwisho, ni vema nikakuonya mapema, kwani kuna watu wananyemelea jimbo la moshi vijijini. Yeyote aliye tayari kufanya kazi na sisi tunamkaribisha. Hatujali wadhifa ulio nao au kipaji chako cha kufaulu darasani, tunachotaka ni maendeleo na wala siyo litania za sifa.tunazo taarifa kuwa badala ya kukazania kutimiza ahadi unatumia rasilimali ulizo nazo kupambana na wote wanaojitokeza kuwania jimbo hili. Hii haitakusadia sana, san asana itazidi kutuongezea wasiwasi tulio nao dhiidi yako, na uwezo wako wa kujibadilisha kwa siku chache zilizobaki, Ni matumaini yangu kuwa utasoma barua hii kwa makini kwani bado hujachelewa
Ahsante sana
Mwikimbi mwitori
moshi