Wana CCM walioituhumu CHADEMA na Mbowe kwa ubabe waombe radhi

Wana CCM walioituhumu CHADEMA na Mbowe kwa ubabe waombe radhi

FACTSFIRST

Senior Member
Joined
Dec 6, 2019
Posts
191
Reaction score
290
Mwanzoni mwa mwaka huu kuna kundi la Wana CCM walikuwa wakiirushia madongo CHADEMA kwa kudai kinaendeshwa kibabe kwa matakwa ya mtu mmoja - yaani Mwenyekiti wake Mh Freeman Mbowe.

Of course, kila mmoja anajua wazi kuwa target siku zote huwa si chama na taratibu zake bali Mbowe na uimara wake wa kujenga chama imara, makini, na sumbufu kwa CCM.

Nakumbuka kuna wana CCM walimwita Mbowe majina mengi tu kv dikteta, anaendesha chama kwa amri zake, na maneno mengine mengi ya kijinga.

Lakini Mungu si Rajabu. Wiki hii Mwenyekiti wa CCM katoa yake ya moyoni kwa kuweka wazi tabia yake ya asili ya kidikteta na kuendesha mambo kibabe bila kufuata sheria, kanuni, au taratibu. Magufuli kawainyookea Wana CCM wenyewe kwa kuwaambia yeye (na si wapiga kura za maoni) ndiyo ataamua nani watakuwa wagombea wa ubunge na pengine udiwani katika chama chake, kumtegemea na ameamkaje!

Hii imeshtua wengi, hata Wana CCM wenyewe, kiasi cha kuwafanya wajiulize mara mbili mbili kama walichokisikia ni kweli kimetamkwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa au na kiongozi mdogo mhuni wa mtaani.

Lakini habari ndiyo hiyo. Huyo ndiyo Magufuli katika ubora wake. Hivi ndivyo amekuwa alifanya hata serikalini. Ubabe, kuvunja sheria, udikteta!

Mungu kawadhalilisha Wana CCM waliokuwa wakiinyooshea kidole CHADEMA kwa kudai hakina demokrasia. Magufuli kawakumbusha maana ya demokrasia ndani ya CCM - ni ubabe, ni maguvu, ni udikteta tulioujua siku zote.

Zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM.
 
Walishauza chama hawana Chao kwa katiba yao mbovu hata Nyerere angekuwepo asingefunua mdomo yangemkuta.
 
Kuongoza watu huyu hapana, watakuja kuelewa baadae akiwa dikteta kamili.
 
Mantiki ya Mhe. Rais ilikua ni kuelezea juu ya uhuni wa baadhi ya wagombea kutumia nguvu ya pesa kuwadondosha wengine. Hivyo ikapelekea kupigia kura mtu ambaye hana sifa ya kugombea (hakubaliki na wananchi). Sasa pamoja na kwamba unaweza ukahonga wajumbe wote lakini hutoweza mhonga Yeye (Rais) na katiba inaruhusu hilo.
 
Usimwekee maneno mdomoni Mwenyekiti na Rais wetu mpendwa? Hukusikia alivosema itategemea ameamkaje?
 
Mantiki ya Mhe. Rais ilikua ni kuelezea juu ya uhuni wa baadhi ya wagombea kutumia nguvu ya pesa kuwadondosha wengine. Hivyo ikapelekea kupigia kura mtu ambaye hana sifa ya kugombea (hakubaliki na wananchi). Sasa pamoja na kwamba unaweza ukahonga wajumbe wote lakini hutoweza mhonga Yeye (Rais) na katiba inaruhusu hilo.
Wasio na ufahamu (vilaza) hawakumuelewa Mh raisi,na mleta mada asipoelewa hii comment yako nae atakuwa Hana ufahamu (kilaza)
 
MBOWE Ni dikteta tu kila alietaka uenyekiti alifukuzwa chadema
 
Mantiki ya Mhe. Rais ilikua ni kuelezea juu ya uhuni wa baadhi ya wagombea kutumia nguvu ya pesa kuwadondosha wengine. Hivyo ikapelekea kupigia kura mtu ambaye hana sifa ya kugombea (hakubaliki na wananchi). Sasa pamoja na kwamba unaweza ukahonga wajumbe wote lakini hutoweza mhonga Yeye (Rais) na katiba inaruhusu hilo.
Kwa hiyo kuna wakati akiamka vizuri anakubali kuhongwa na kupitisha watu?
Kama swala ni watu kutumia hongo/fedha kwanini itegemee kuamka kwake?
Je? akiamka vibaya akate majina wanaokubalika na wajumbe pamoja na wapiga kura. si ndiyo kuwagawa wanachama huko?
 
MBOWE Ni dikteta tu kila alietaka uenyekiti alifukuzwa chadema
Na tunapoelekea kwenye Kampeni na Kisha uchaguzi, Mbowe awe Chini ya ulinzi wa Chama chake ili asije akarudia tena kufakamia gongo Chama chake kikasingizia kushindwa kwake kumechangiwa na M/kiti Wao Kwa sababu hakushiriki kumkampein mgombea urahisi wao
 
Back
Top Bottom