Wana CCM wamshukia Dk. Slaa

Ama kweli waTZ bado tuko mbali sana na kuelewa usanii wa JK. Kama walivyosema wengi, umaskini unatuponza wengi na tunakubali hata 5000 ili unyeshewe na mvua!!. aibu sana. Hivi mwanaCCM anayeandamana, anapongeza nini hasa? Kufichwa mafisadi wa EPA?, kusema kuna nchi ya Tanganyika? au kuambiwa sasa deni la nchi lemepungua?. Hata mtoto wa STD VI hawezi kukubaliana na aliyosema JK akiagalia hali .halisi mitaan
Shame wana CCM!!!!!!i
 

Tatizo letu sisi wadanganyika ni kwamba CCM imetuweka mfukioni.Imagine tunaumizwa wote na wanaofaidi ni wachache hao hao wenye nafasi lakini sisi tunaumia jua kuandamana kuwaunga mkono na kuwatetea.

Kikwete ni mjanja na ile ni ajenda ya CCM kuwapumbaza watanzania kwa kuwaambia fedha zinapelekwa kwenye kilimo lakini in reality ishu ya EPA inawahusu CCM kwa kiwangi kikubwa.

Alichisema Slaa ni ukweli mtupu kuwa bunge ndilo lilistahili kutoa maamuzi juu ya fedha za EPA na siyo Kikwete.Kampeni za kusafisha chama zimeanza kwa kasi ya kutisha.Juzi CCM wamewagharamia wanachama wa upinzani waliohamia CCM wakaletwa Dar kuja kuoneshwa kwenye TVs kuwa wamerudi CCM.Hiyo nayo ni kampeni ya kujisafisha na uvundo wa EPA na madudu mengine.

Tusipoangalia tutasahau tulipoumwa na nge tukabaki tunachekelea.KWELI TUMELISHWA UNGA WA NDERE, MWE WAJAMENI!
 

kweli-Fedha ya kilimo inatakiwa iwe halali- screw CCM...
JK kua na akili timamu!!...
 
Spika wa Bunge Samuel Sitta amesema Rais Jakaya Kikwete hakukiuka sheria wala taratibu zo zote za fedha, kwa kuamuru baadhi ya fedha zilizokuwa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) zitumike kwa ajili ya ruzuku ya mbolea na mikopo ya kilimo katika Benki ya TIB.

Kwa mujibu wa Spika, taarifa kuhusu kupatikana na kutumika kwa fedha hizo inaweza kuletwa bungeni. “Ni utaratibu sahihi kabisa,” alisema Spika Sitta. Alitoa ufafanuzi huo baada ya Suzan Lyimo (Viti Maalumu - Chadema) kutaka ufafanuzi huo kutoka kwa Spika kama ilikuwa sahihi kwa Rais kugawa fedha hizo.

Kauli kama hiyo pia iliwahi kutolewa katika vyombo vya habari na wabunge wengine wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa (Karatu) na Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini), ambao walijenga hoja kwamba Bunge ndilo lenye jukumu la kugawa fedha za matumizi kwa serikali.

Spika, ambaye alimwambia Lyimo kwamba ‘amechomekea’ swali kwake, alisema kazi ya Bunge ni kuridhia na si kupanga matumizi ya serikali. Aliwataarifu wabunge kwamba mara kadhaa, mara baada ya kikao cha Bajeti, hupatikana fedha kutoka vyanzo mbalimbali, wakiwamo nchi wafadhili au watu binafsi kama bilionea Bill Gates wa Marekani. “Zinaletwa wakati bajeti imepita na serikali haiwezi kuzikataa. Baadaye inaleta taarifa bungeni,” alisema Spika.

Wakati akilihutubia Bunge wiki iliyopita, Rais Kikwete alitangaza kutwaa mabilioni hayo ya EPA, ambayo sehemu yake yalikuwa yamekwapuliwa, na kuyaelekeza katika mfuko wa ruzuku na Benki ya TIB. Ingawa hatua hiyo ilishangiliwa na wananchi, wabunge wa Chadema wanaendesha kampeni ya kueleza kuwa alikosea taratibu, kwani fedha hizo zilipaswa kufikishwa bungeni na lenyewe ndilo lingeweza kuamua zipelekwe wapi.

Source: HabariLeo
 
Ni hatari sana mambo wakati mambo muhimu ya taifa yanapogeuzwa kuwa ya kisiasa , wakati inajulikana wazi wazi kuwa siasa ni PROPOGANDA namsikitikia sana na pia namuonea huruma jk kwa kushindwa kuongoza nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…