Uchaguzi 2020 Wana CCM wanaotaja Membe kuteuliwa na CHADEMA bila kumtaja Lissu, ni propaganda chafu. Membe hawezi kuteuliwa bila ridhaa ya Lissu!

Uchaguzi 2020 Wana CCM wanaotaja Membe kuteuliwa na CHADEMA bila kumtaja Lissu, ni propaganda chafu. Membe hawezi kuteuliwa bila ridhaa ya Lissu!

jmushi1

Platinum Member
Joined
Nov 2, 2007
Posts
26,329
Reaction score
25,263
Wanajamvi,

Naona kama kuna panic ya hali ya juu humu jamvini, ya members wengi maarufu humu mfano Troll JF johnthebaptist, wakidai kuwepo na kikao cha mwenyekiti wa CHADEMA na Membe kuhusu nafasi ya kuiwakilisha chadema kwenye uchaguzi mkuu wa rais mwaka huu Oktoba.

Lakini kwa uelewa wangu, sidhani hata kama wanachosema ni kweli hata kidogo. Kwa vyovyote vile, wana nia ya kuanza kuweka mianya kwa upinzani. Lissu mwenyewe ni mtu anayekipenda chama chake. Hata kwenye issue ya Lowassa kuja, hakujiondoa kwenye chama kama alivyofanya Slaa. Nadhani hata Lissu angejitoa, badala ya risasi, angepewa cheo. Lakini yeye ni muumini wa mabadiliko ya kuiondoa ccm madarakani.

Kwa wale waelewa, tunasubiri kauli ya Tundu Lissu kabla ya kusema mengi ambayo yanaweza kupanda mbegu mbaya itakayoweza kusambaratisha upinzani zaidi.
 
Kwani lisu ni Nani? Mwenye uamuzi ni(mwenye chama Chake) MBOWE tu, lisu Hana jeuri yeyote kwa mwenye Sacco's yake!!!
 
Kwani lisu ni Nani? Mwenye uamuzi ni(mwenye chama Chake) MBOWE tu, lisu Hana jeuri yeyote kwa mwenye Sacco's yake!!!
Hiyo ndiyo propaganda mnayoilazimishia. Hicho kikao mnaripoti nyie mmekidukua au?
 
Safari hii ccm wanahangaika kumtuma kachero mzoefu aende upinzani kugombea urais.Upinzani kuweni makini
 
Biashara ya kuuza nafasi indelee.
 
Tuwe watulivu mambo yanaandaliwa vyema mtajulishwa tuwe pamoja.
 
Inasubiriwa sauti ya Tundu Lisu badala ya Mwenyekiti?
 
Back
Top Bottom