Wana CCM wenzangu tukiendelea kuwa na kiburi cha uzima na madaraka Taifa litapasuka vipande

Wana CCM wenzangu tukiendelea kuwa na kiburi cha uzima na madaraka Taifa litapasuka vipande

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Wengi wetu niwaumini wa dini mbalimbali na tumefikia hatua kila jambo baya au zuri tunamtaja Mwenyenzi Mungu, nipongeze kwa ilo.

Lakini ni ukweli usiopingika kwamba tunamkosea sana Mwenyenzi Mungu na tunaweza tukawa tunamkasirisha sana kwa matendo tunayoyafanya hasa kwakuyafanya maisha yetu yategemee siasa za chama tawala kuliko taifa kuishi maisha yanayompendeza Mungu.

Yapo mapokeo yakiimani yameibuka hivi katlribuni ambayo hayaendani na vitabu vitakatifu vinavyosema. Viongozi wetu wa dini wamekuwa watu wamataifa kuliko watu wakuingoza nchi kwenye toba.

Msiba wa mpendwa wetu umetuonyesha wazi kwamba Taifa limegawanyika, Wapo wanaosema ukweli na Wapo wanaosema uongo kila mmoja akiwa na malengo yake. Ila kama Taifa mfumo wa usiri, watu wasiojulikana, kusudio la watu wote kuwa chama Tawala na kufanya ukosoaji kwa viongozi kuwa jinai kumedumaza uwezo wetu Wana CCM kufikiri na kutuweka mbali na ibada ya kweli ambayo ni matendo yampendezayo Mwenyenzi Mungu.

Naomba kusema, kwa namna wazee walivyosema katika maeneo tofauti, kwa namna viongozi wa dini walivyohubiri bila kukemea maovu yaliyopita, kwa namna viongozi wetu wa serikali walivyojipambanua na kwa namna Marais wastaafu na Mawaziri wakuu walivyojipambanua tukubali kwamba Taifa limepoteza dira na mwelekeo kwa siku za usoni. Maadili nakusema kweli vimeondoka kuwa tunu zetu na kusema uongo kumegeuka kuwa nguzo kuu za Taifa.

Lini tutasema ukweli kwamba Taifa letu linafaa kufanya maridhiano? Lini tutakubali kwamba damu zilizomwagika kwa awamu ya nne na tano zimesimama upande wakuligawa Taifa? Lini tutakubali kwamba wananchi wameondoa kuwa walinzi namba moja wa Tqifa letu kwa sababu tu hakuna usawa na haki?

Mhe. Rais , unalo jukumu lakuweka chama pembeni nakuliongoza Taifa, unalojukumu lakupambana na mfumo wa wasiojulikana, unalojukumu lakupambana na unafiki uliojengeka miyoyoni mwa watawala na unalojukumu yakuliponya Taifa.

Naomba niseme, Miradi mingi ya maendeleo si kipimo cha maendeleo katika ulumwengu wa sasa, maendeleo ya kweli ni furaha, amani, utu na haki kwa wananchi. Taifa linalomwaga damu kwa ajili yakufungua milango ya maendeleo nitaifa linalotengeneza njia yakukua kiuchumi kwa haraka lakini kuporomoka kwa kasi pale wanaoumia watakapoacha kuandamana miyoyoni nakujitokeza adharani.

Niwaombe viongozi wa dini wasiombe sana bali wajiombee wawe na ujasiri wakutoka adharani nakukemea maovu. Kuendelea kuomba huku wakishindwa kukemea maovu nikujitengenezea miyoyo isiyojiamini mbele za Mwenyenzi Mungu. Kweli siku zote ukuza imani lakini uwoga na unafiki uzalisha uasi.
 
Lissu si ana furaha na sherehe kubwa ya kifo cha JPM, CDM si mna furaha , sasa mnachohangaika ni nini? Huwezi kukaa chini na mshenzi kama Lissu mkaongea chochote, kila mtu atapata stahili yake tu .
 
Lissu si ana furaha na sherehe kubwa ya kifo cha JPM, CDM si mna furaha , sasa mnachohangaika ni nini? Huwezi kukaa chini na mshenzi kama Lissu mkaongea chochote, kila mtu atapata stahili yake tu .
Huuu si wakati wa kumtukana huyo unayemtaja vinginevyo utakuwa punguwani kichwani
 
Una akili kubwa sana,tunza hiyo isije haribiwa na hao JK alowaita waganga njaa,

Umeongea jambo sahihi kwa manufaa ya nchi siyo siasa
 
Lissu si ana furaha na sherehe kubwa ya kifo cha JPM, CDM si mna furaha , sasa mnachohangaika ni nini? Huwezi kukaa chini na mshenzi kama Lissu mkaongea chochote, kila mtu atapata stahili yake tu .
Pole sana. mkuki kwa nguruwe......kwa ninadamu mtamu sana.
 
Lissu si ana furaha na sherehe kubwa ya kifo cha JPM, CDM si mna furaha , sasa mnachohangaika ni nini? Huwezi kukaa chini na mshenzi kama Lissu mkaongea chochote, kila mtu atapata stahili yake tu .
out of topic. hata uzi hujasoma
 
Who is "wenzangu", kwa nini unajidanganya? Wewe siyo CCM. Hoja yako siyo mbaya lakini unapoinafiki unatibua kila kitu watu hawataamini ni lini utasema nini. Kwa urongo huu sasa hata jina lako nadhani si lako na hilo kabila na hata dini naona vyote ni vya kubuni tu. Jipime.
 
Kwa hakika wewe ni mtu wa Mungu , mtu akitazama ulichokiandika hapa ni ushahidi tosha kuwa wewe una hofu ya Mungu hasa na unalitazama taifa sio raha za muda muda mfupi zinazoandaa
 
....Kwanini kuugua ilikuwa siri....mpaka dhihaka...PM..."Rais ni Mzima"...mimbarini/msikitini_Njombe hapo..."Rais anamenituma niwasalimie"..VP..Lushoto ..hadharani?
 
Lissu si ana furaha na sherehe kubwa ya kifo cha JPM, CDM si mna furaha , sasa mnachohangaika ni nini? Huwezi kukaa chini na mshenzi kama Lissu mkaongea chochote, kila mtu atapata stahili yake tu .
Ok, well noted. We'll see who'll be the looser.
 
Back
Top Bottom