Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Viongozi na wanachama 6 wa CHADEMA Ngazi ya Kata ya Muganza akiwemo Tumain Petro, Mwenyekiti BAVICHA wa Sasa wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi wakati wa tafrija ya Kusherehekea kukamirika kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyamagoma.
Sherehe hiyo ilidhaminiwa na Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara ambaye alichangia Shilingi 5,600,000, Kilo 100 za Mchele pamoja na wananchi waliochangia kilo 650 za Mchele, Maji, Kuni na kutoa eneo la kufanyia Sherehe hiyo. Aidha Ng’ombe 4 zilichinjwa hivyo kufanikisha kulisha wananchi zaidi ya 2,300 wa Kata ya Nyamagoma.
Wakiongea na vyombo vya habari, wananchama hao walieleza sababu mbalimbali za kuihama CHADEMA na kujiunga na CCM ikiwemo kuvutiwa na kazi na viwango vya uongozi Bora wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro ambaye ametekeleza ahadi zake alizozitoa kwa wananchi wakati alilokuwa akiomba kura mwaka 2020.
Miongoni mwa ahadi zake Mbunge Ndaisaba George Ruhoro ilikuwa ni kujenga Sekondari, kujenga Minara miwili ya Mawasiliano na kufikisha umeme kwenye Kata hiyo ahadi ambazo zimetekekezwa kwa asilimia mia moja.
Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amewaomba wanachama wengine wa CHADEMA kuendelea kujiunga na Chama Tawala CCM ambacho ndicho Chama sahihi chenye Sera, Ilani inayotekelezeka na viongozi wenye weledi, utashi na uwezo wa kutatua matatizo ya wananchi ikiwemo kuleta maendeleo ya vitu na watu.
Naye, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ngara Ndugu Vitalis Misago Ndailagije amewapongeza wanachama wa CHADEMA kwa kufanya uamuzi sahihi wa kujiunga na CCM Chama Tawala na kuwahakikishia kuwapa malezi bora na ushirikiano wa kutosha wakiwa wanachama wa CCM.