Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kwenye hotuba yake ya kutangaza kuendelea kuutaka uongozi wa CHADEMA, alisema kuwa kuna watu wanasema Mbowe amechoka, katika kulijibu hilo, akasema kuwa yeye bado ana nguvu, ana uwezo wa kufanya mikutano hadi 8 kwa siku, na kwamba, hao wanaosema amechoka, wamwambie ni nani anaweza kufanya hivyo. Ilikuwa ni kauli ya kushangaza na kuonesha kuwa kweli Mbowe, kiuwezo amechoka.
Kwanza, Mbowe yeye mikutano yake hutumia chopa, wenzake wanatumia magari, wakati wenzake wanatumia muda mwingi barabarani, ikitokea yeye amefika maeneo mengi kuwazidi wanaotumia magari, eti hicho ni kipimo cha yeye kuwa na nguvu!! Kwani anafika maeneo mengi kwa kutumia mbawe zake, hadi ajisifu ana uwezo wa kufika maeneo mengi? Unawanyima wenzako hata pesa ya mafuta, wewe unatumia usafiri wa gharama kubwa kupindukia, halafu unajisifu kuwa una nguvu! Je, hili si dhihirisho tosha kuwa Mbowe amechoka?
Kwa fikra na mtazamo wa Mbowe, tamaa yake ya uchu wa madaraka, itaisha pale mwili wake utapokuwa umegoma kabisa! Yaani asiwe na uwezo hata wa kutembea.
Mbowe amekataa kabisa kuweka muda wa ukomo kwenye uongozi, anadai kuwa ukomo ni pale wananchi watakapomkataa!! Mbowe hata baada ya kukaa kwenye madaraka kwa muda mrefu, ameshindwa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya kuelewa kuwa nchi zote, na taasisi zote zinazoweka ukomo wa madaraka, ni kwa sababu zinatambua kuwa mtu aliyepo kwenye madaraka, ana advantage kubwa au uwezo wa kumanuplate ili aendelee kuwepo madarakani. Kwa hiyo hata kama wananchi hawamtaki, lakini ni vigumu sana kumwondoa ambaye yupo madarakani.
Fikiria Mbowe ashindane na mjumbe wa kamati kuu ambaye hamiliki chochote ndani ya chama zaidi ya utu wake, wakati kwa mfumo wa CHADEMA, kila kitu, mpaka pesa za chama, ni mali ya Mwenyekiti Mbowe, watendaji wote wa chama wa ngazi ya Taifa, ni mali ta Mbowe, anayepanga mishahara yao, anayeamua nani awe mwajiriwa au kibarua wa chama, ni Mbowe; je, unadhani kunakuwa na mazingira sawia ya ushindani?
Anaweza kuondolewa, lakini lazima kuwa na nguvu kubwa ya ziada, tofauti na kwa upande wake.
Mbowe, bila shaka ni wale viongozi wa aiana ya Museveni wa Uganda, Banda wa Malawi au Mugabe wa Zimbabwe. Ni watu wanaotaka, ikiwezekana wafie madarakani, kwao hayo ndiyo mafanikio makubwa na kudhihirisha walikuwa na nguvu mpaka dakika ya mwisho.
WanaCHADEMA, waunganishe nguvu, wampumzishe Mbowe, kisha waibadilishe na kurekebisha katiba ya chama ili kuondoa hii hali mbaya ya sasa wanayokumbana nayo. Tamaa na uking'ang'anizi wa Mbowe, umewasaidia kutambua matobo ya katiba yao.