The secretary
JF-Expert Member
- Jan 14, 2012
- 4,148
- 2,542
Ni faraja iliyoje kukuta uzi huu wa ladyfurahia na wadau waliochangia kwa kuguswa.inanikumbusha maana halisi ya kujiunga jf ni kujifunza.kuhabarishana..kujenga mahusiano.kusaidiana..kufanikisha biadhara ns malengo..kupeana ushauri.. nasaha..faraja na masuluhisho kwa ushirikiano
mbarikiwe nyote kwa mashirikiano haya
Nashukuru kwa nasaha njema Lady doctorHakika Mungu ataweka mikono yake juu ya madaktari wako uweze pata tiba na uponaji wa haraka na urejee kama awali!
Nashukuru kwa nasaha njema Lady doctor
Ushauri wangu kwa wanaJF wote especially wasio katika ajira za serikalini ambazo wengi wao wameingizwa Bima afya nibora kama kampuni yako au taasisi haijakupa bima afya ama AAR au STRATEGY ni vema kujiunga kwani linapotokea janga la kiafya ni msaada mkubwa wa matibabu hapa nchini na nje kama kenya..south africa na india.pia ni suluhisho kwa gharama kubwa za tiba kama hapa MOI chumba tu ni 50-75,000 kwa siku ikiwa haijumuishi gharama za tiba..madawa..upasuaji..xray..ct scan..maabara..ushauri na huduma nyingine
Mimi ni shuhuda wa kasoro hiyo nimeona madhara yake hivyo nisingependa iwayokee wengine
Pole sana Mkuu Mwenyezi Mungu akujalie afya njema.
ladyfurahia tuwasiliane hata kama nikishindwa kuja angalau nikupe supu ya kongoro ili mifupa iunge mapema
So sad kwa mdau Inkoskaz kweli muda mrefu nilikuwa sijamsoma hapa JF.
ladyfurahia hebu nipe mwongozo tunakwenda kama group au kila mmoja kivyake? hebu nifahamishe utaratibu kama ni kila mtu kivyake yuko wodi namba ngapi?
ladyfurahia nitaomba updates zaidi ili mimi na wake zangu tukamwone mwenzetu huyu.
Sad news, ladyfurahia napendekeza wewe mwenyewe chukua usukani wa ku organise tunaoweza kufika huko twende, Napendekeza iwekesho jioni. tukutane pale pale MOI
pole sana mwana jf mwenzetu. ladyfurahia tujuze namna ya kumpata hapo naweza pitia pale ili nikamwone.
Allah akbar... mola Ndio muweza wakila kitu, taratibu zikoje....?
Mimi sipo Dar ila nitatoa mchango wangu ambao utawakilisha nafsi yangu. Cha muhimu tu mtoa mada dada ladyfurahia weka utaratibu wa wazi kwa jinsi ya kutoa michango kwa wale watakaoshindwa kwenda. Nawahimiza wanaJF hata kama sio wa Dar kumsaidia mwenzetu. Hakika utabarikiwa kiafya, kimali, kielimu, kifamilia etc
Mkuu monaco asante sana..ukifika moi private ward ulizia chumba I ukiingia kitanda cha kwanza kabisa mlangonipole sana sana sana Mkuu,tuko pamoja,bado upo pale MOI? Unaweza kutoa Mwongozo kidogo?
Mimi nina Imani utapona,Kwa Imani utapona.
Shukuru Mungu kwa Kuwa ni Mwema.
Pole sana.
Asante sana MamndenyiPole sana mwana jf mwenzetu. ladyfurahia tujuze namna ya kumpata hapo naweza pitia pale Ili nikamwone.
Asante sana Mamndenyi
View attachment 114639
Hiyo ni picha yangu halisi siku chache kabla ya ajali japokuwa sasa Sipo hivyo
Ni kawaida na hulka ya binadamu uwapo mzima kujisahau.Nguvu..uwezo namengineyo hutufanya tuhadaike na kujisahau
Kuwa kuna wakati wa mitihani tunahitaji kudra ns rehema zake mola muumba tu.pia pamoja na yote aliyotujalia lakini kuna wakati we need people to assist and SAVE
Nikitafakari kama mimi baada ya ajali nilipoteza fahamu kwa almost 4 days lakini watu waliniokoa na kunifikisha hospitali..madaktari wakawajibika na wauguxi pia.wanafamilia na marafiki nao wakaendelea na huduma kama kunilisha..kuninywesha..kunisponge..kunisetiri nk Hivyo kila binadamu anayekuzunguka ana nafasi yake kwani hujui ni lini atakuwa msaada kwako hata kama una mapesa bado hayatapatikana kwa wakati unayohitaji wala kukutendea unavyotendewa na binadamu wengine
tuthaminiane na kujaribu kujiweka katika nafasi zao je ingekuwaje?