Wana Diaspora tukutane hapa

Joined
Aug 29, 2017
Posts
53
Reaction score
40


Mimi nilienda UK kusoma in 1991 nilifanya undergraduate kisha nikaendelea na MA huko huko. nimeishi kikazi nchi mbali mbali kama vile UAE, Singapore, South AfricaAustralia, Israel na bila kusahau Canada.

Ilipofika 2000 nikaamua kuvuka nimekuja huku Unyamwezini. Nimeishi majimbo mbali mbali hapa USA na sasa nime settle huku Houston Texas.

Kwa sasa mimi ni raia wa USA na najivunia sana uraia wangu. Hii haiondoi ukweli kuwa sijasahau asili yangu na nilikuwa na mwamko mkubwa sana wa kutaka kuendeleza Tanzania kama vile kupeleka wawekezaji nk.

Zama za JK niliingia wazimu wa kwenda kununua mashamba na viwanja Bongo na bila kusahau niiliset up makampuni mbali mbali hapo lakini naona nchi na serikali yenyewe hazina interest na sisi wana diaspora hivyo niliamua kuuza assets zangu zote Tanzania na sasa sina chochote huko kwa sababu mimi maisha yangu ni huku na kutokana na umri naona afya nayo muhim hivyo kwa kazi zangu nina better medical coverage na mambo mbali mbali.

Tanzania bado ni nyumbani na napapenda lakini sitaki kuwa mnafiki, napapaenda zaidi USA kwani ni nchi ninayothaminiwa, elimu yangu inathaminiwa, utu wagu unathaminiwa na kwa kweli sihitaji kupimwa mkojo kama nikimcriticise Mkuu wa nchi.

Naamini kuwa bado fursa zipo za kutumia wana doaspora lakini hilo halitowezekana Tanzania na naamini itachukua labda mika 50 ijayo (tena kwa kubadilisha katiba ambayo among other things itawapatia haki za kufanya mambo kadhaa wa kadhaa ya maendeleo na NK ) kama walivyofanya Nigeria, Ethiopia , Kenya , South Africa, Israel na India. Nilifunga kampuni zangu zote na niliendelea kufanya kazi nchi jirani ambazo watu na serikali zao ni progressive and they actually make things done.

Ukweli usiopingika ni kuwa serikali na watawala waliopo madarakani hawawezi kukubali hili jambo kwa sababu itabidi iondokane na katiba iliyopo sasa mimi sioni sababu ya CCM kuachana na katiba ambayo itawafanya wabaki madarakani mpaka Yesu atakaporudi.

Niko tayari kupokea maswali na nakaribisha wana diaspora wengine waje tujumuike humu na tu "chop some games."
 

Mkuu mawazo yako yanawakilisha wanadispora wote wa Tanzania. na kama wanadipora wengetakiwa kujieleza mmoja mmoja basi wengi watakua ni kama wewe wanazi penda nchi zao za pili kwa sababu ya heshima wanayopata kuliko wakiwa katika nchi zao walizozaliwa.
Na naamini serekali ikiyachukua na kuyazingatia basi itapata cha kujifunza kutoka kwako.
 
Mkuu tatuzo la wana diaspora wengi waliokuja huku nje around 15_18yrs bado wana spliting minds. Mguu ndani mguu nje. Wanashindwa kuwa kama wayahudi au wadosi au latinos ambao wao wanaishi American dream. Narudia its not perfect lakini utaishi na utaheshimiwa kama binadam.

Unakuta mtu amespend milioni 900 kujenga nyumba Tanzania ambayo anaitumia 20 days akienda holiday. Tge rest hiyo nyumba inakuwa danguro watu wana tmbea tuuu.

Sasa hebu convert hiyo 900 nto usd au Yen au pounds au euro na mtu nduo raia wa nchi hizo zilizoendelea na tayari unafamily maana yake you are set for life...mortgage down payment na bado una pesa za kukusaidia kuishi au ku invest facebook google au general electric...


Sasa hivi kila wanahangaika kuuza nyumba viwanja na mashamba yasiyouzika zama hizi za magufuli.

jf where we dare talk openly
 
je njia zipi rahisi kuinia USA na kupata makaratasi ya kubaki?
 
Bongo hakuna dili this term mkuu, nilikuwa huko majuzi tu. Invest for ur future life ya huku, una uhakika wa maisha. Na humu ukitaja (majuu), wachache wasiojiamini wanajua unajigamba. Anyways hopefully bongo will get better. Ndugu yako akipata na ww unatajirika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…