Samahani mie nitapingana kidogo na wachangiaji hapo juu, Hvi ni Watanzania wangapi wanaweza kuongea sentensi 5 kwa kiingereza bila kuboronga?? Ni wachache ambao wamepata bahati ya kusoma shule za English Medium na wengine wengi ambao wazazi wao walikuwa na uwezo wa kuwapeleka ulaya wakasome. Sisi wengine tuliosoma shule zetu za kina Kanumba hatuwezi. Na hata ukienda kujiendeleza kusoma kiingereza kuflow inakuwa ni ngumu sana. Mie nafikiri badala ya kumcheka na kum-critisize labda tungetafuta namna ya kumshauri.
Kama mnaangalia Big Brother kuna Mshiriki wa kiume kutoka Msumbiji anaitwa Lionel hajui kabisa Kiingereza na anachapia ile mbaya, Tujiulize kitu kimoja kwani Kiingereza ni lugha yetu??? Watu mmeifanya issue sana, Na wala sio suala la shule kwani ni wangapi wamesoma mpaka Chuo Kikuu na Degree zao lakini hawawezi ku-flow kiingereza? Sio tu wasanii wenzake hata sisi tupo wengine wengi ambao hatukupendezewa na namna watu walivyoli-handle suala la Kanumba akiwa BBA
Tuache Kasumba ya kikoloni lugha yetu ni kiswahili na ndio 'Communication Language yetu Watanzania.
unachokisema kuhusu Kiiingereza uko sawa, lakini acha kumtetea kanumba kwasababu ki ukweli kaboronga , na kumbuka kanumba hakwenda pale kama mshiriki kaenda kama celebrity tena kwa kujigamba msanii anayetaka kwenda kimataifa, sasa jiulize swali moja wangapi wameenda Hollywood ambapo hawajui Kiingereza?
swala la msingi yeye kanumba anajua kabisa kwamba BBA lugha inayotumika kuwasiliana ni Kiingereza na si nyingine yeyote , alikubali vipi kwenda kuliwakilisha taifa wakati hata msingi wa kiingereza hana? na si hilo tu nadhani utakubaliana na mimi jinsi upeo wake wa akili wa kujibu maswali ulivyokuwa mdogo ,
na tafadhali acha kusingizia shule za serikali ndo kisa cha kanumba kutojua kingereza , kwasababu majority tumesoma kwenye shule hizohizo lakini tumefanya juhudi binafsi kujaribu kujifunza hicho kiinegereza, yuko kwenye uigizaji kwa miaka mingapi amejishindwa kujifunza hata kiingereza cha kuombea maji? wakati alipokuwa anapanga kuigiza movie na wanigeria si ndo ilikuwa changamoto kubwa ya kwenda kozi ya kiingereza?
mbona mnaacha kuongea ukweli na kutetea vitu visivyo na msingi, Je unataka kuniambia kisa tumesoma shule za serikali na sio English Medium basi tusijiendeleze tukapata kazi kwenye mashirika ya kimataifa kisa nadumisha kiswahili changu? weee bwana acha hizoooo,
hawa wasaniiii ukweli wanalewa na sifa huko mitaani tunaonana nao kila siku maringo ulevi na uzinzi ndo wao wanaona ndo maisha wameyapatia lakini ukweli mie ningekuwa wao ndo kwanza maisha yanakuwa yanaanza kwa kujipanga na kujiendeleza zaidi, afadhali hata hawa wasaniii wa muziki naona siku hizi wamezinduka wanaingia shule na kujiendelza.
wasaniii wanatakiwa wasome waongeze upeo wao wa uelewa na ufanisi, na waache blah blah blah za akina kanumba na rey