Wana filamu kuandamana, kisa Kanumba ka-comediwa!

Mambo Ya Kanumba
Steven Charles Kanumba is my name, i was born in a Christian family of 2 girls and i happen to be the last born and the only boy to Mr. & Mrs. Charles Meshark Kanumba.

Mi naona kizunguzungu hapa....!!! Steven Charles Kanumba Ali-close vipi?? au aliogopa kuuliza menu akaamua kusingizia closing? Halafu siku ile pale ilikuwa usiku saa moja ya CAT, (saa 2 ha huku EAT), sasa yeye alikuwa na mpango wa ku-open muda gani?? (Usiku wa manane)??

Jamani, lazima tukubali kuwa mtu anapokataa kukosolewa basi ana mtindio wa ubongo au amefilisika kimawazo!! Nobody is perfect, cha kufanya ni kukubali mabadiliko
 

Tatizo la wasanii wetu si lugha kama wengi walivyofafanua. Maximo yes lugha inamsumbua lakini unaelewa logic yake.
wanatakiwa wajue maana ya sanaa, kama wanatengeneza movie, inapaswa ionekane kama movie. picha zao nyingi nimeziona, lakini si sanaa ile tunayoijua ni kama wanaelezea matukio ya kawaida na kwa kawaida mno bila kuonyesha ubunifu wowote utakaomfanya mtu anayetizama kuumiza kichwa kidogo kufikiri (ambapo ndiyo kwenye utamu wenyewe wa picha). Tatizo lao kubwa ni umbumbumbu. wanatakiwa wafanye kazi kubwa sana kujiendeleza ki sanaa. si wabunifu; si watunzi wazuri; hawajui ku act au wanachukua nafasi wasizostahili; wanajiinua mno kuwa kwenye level wasiyostahili; nk nk.
ushauri
1. Watafute wataalamu wa kutunga stories, UDSM, au Bagamoyo nk.
2. Watafute waongozaji wazuri (profesionals), wasiongoze wao
3. Washauriwe waigize wakiwa kwenye natural form
4. Wasilazimishe nafasi kwenye movie
5...........
6.............
 

Aaaaaaaaaaaaaggggggggggghhhhhhhhhhhhhhhhhhhhrrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!!
 

Kituko niko pamoja na wewe...hata gavana wa California Arnold Schwarzenegger...naye hivyo hivyo kama Van Dame...
 
kwa ufahamu wangu ni vigumu sana kutengeneza movie nzuri kwa kutumia vifaa vibovu.

hiki kinaharibu sana movie za kitanzania.

unakuta movie imerekodiwa na sony PD170 au Sony PD190,hizi ni amateur level cameras maalum kwa weddings and birthday parties,tena western wedding ambazo usually zina wageni 50-100.kwa maana kuwa hata hizi wedding za kitanzania zinazojaza kanisa la watu 1000 hizi camera hazifai.

ukija hizo studio zao ndio kabisa,full of pentinum 4 processor's computers with movies edited with the likes of adobe software etc,this is sad.

Elimu ya watu waliopo kwenye movie industry tanzania ni kiduchu,sasa kama sound editing inafanywa na DJ unategemea kusiwe na makelele?

hapa wakuwalaumu ni wasomi wetu ambao wakishapata vi-degree kuna baadhi ya kazi wanazipiga mstari-hawazitaki tena,sio saizi yao,mie huu naona ufinyu wa akili.

Pindi watanzania watakapoanza kwenda university kusoma vitu kama sound engineering na video editing as well as convesion etc ndipo mtakapoanza kuona movie zenye quality nzuri.

actors wetu wanajitahidi ila ukosefu wa exposure na muongozo vinawaangusha.wale wenzao wa hollywood sio ma-genius kiasi hicho sema they have the right people running their brands.PR Managers should ring a bell here..,

kuhusu lugha ni vizuri wakatumia kiswahili,ili wawe huru zaidi na wawe natural zaidi,movie nzuri hata usipoongea maneno ya kiingereza hata oscar itashinda.art has a way of talking to people.si mnakubuka "memoirs of geisha" and many other movies that won the best foreign movie award?!

hii tabia yao ya kukopi movie za ki-nigeria inakera sana watu-especially the educated segment of tanzanians..,which is growing rapidly.Lakini kwa asilimia kubwa ya watanzania ambao nao kingereza ni mtego,hizi movie zina wapenzi wengi tu wakutosha,so i guess this is marketing forces speaking here.so sa,it kills creativity.
But we should expect this from form 4 leavers right?
 
Kineno kipya cha mtaani ni UKANUMBA,ukikosea lugha hapo ujue umekanumba na utaambiwa acha ukanumba!
 
Kineno kipya cha mtaani ni UKANUMBA,ukikosea lugha hapo ujue umekanumba na utaambiwa acha ukanumba!

Tatizo wengi wanaomuua Kanumba hata wao Kiingereza kinawapiga chenga. Watu bana...
 
Wadau!! Waacheni hii mijamaa iyandamane ili jamii na watazania wote wajue huo upuuzi, ujinga na umbumbu wao.
 
unachokisema kuhusu Kiiingereza uko sawa, lakini acha kumtetea kanumba kwasababu ki ukweli kaboronga , na kumbuka kanumba hakwenda pale kama mshiriki kaenda kama celebrity tena kwa kujigamba msanii anayetaka kwenda kimataifa, sasa jiulize swali moja wangapi wameenda Hollywood ambapo hawajui Kiingereza?
swala la msingi yeye kanumba anajua kabisa kwamba BBA lugha inayotumika kuwasiliana ni Kiingereza na si nyingine yeyote , alikubali vipi kwenda kuliwakilisha taifa wakati hata msingi wa kiingereza hana? na si hilo tu nadhani utakubaliana na mimi jinsi upeo wake wa akili wa kujibu maswali ulivyokuwa mdogo ,
na tafadhali acha kusingizia shule za serikali ndo kisa cha kanumba kutojua kingereza , kwasababu majority tumesoma kwenye shule hizohizo lakini tumefanya juhudi binafsi kujaribu kujifunza hicho kiinegereza, yuko kwenye uigizaji kwa miaka mingapi amejishindwa kujifunza hata kiingereza cha kuombea maji? wakati alipokuwa anapanga kuigiza movie na wanigeria si ndo ilikuwa changamoto kubwa ya kwenda kozi ya kiingereza?
mbona mnaacha kuongea ukweli na kutetea vitu visivyo na msingi, Je unataka kuniambia kisa tumesoma shule za serikali na sio English Medium basi tusijiendeleze tukapata kazi kwenye mashirika ya kimataifa kisa nadumisha kiswahili changu? weee bwana acha hizoooo,
hawa wasaniiii ukweli wanalewa na sifa huko mitaani tunaonana nao kila siku maringo ulevi na uzinzi ndo wao wanaona ndo maisha wameyapatia lakini ukweli mie ningekuwa wao ndo kwanza maisha yanakuwa yanaanza kwa kujipanga na kujiendeleza zaidi, afadhali hata hawa wasaniii wa muziki naona siku hizi wamezinduka wanaingia shule na kujiendelza.
wasaniii wanatakiwa wasome waongeze upeo wao wa uelewa na ufanisi, na waache blah blah blah za akina kanumba na rey
 
Swala hapa sio kuongea kiingereza...swala ni wasanii wanataka kuandamani kisa kukomediwa....sasa kama unasoma between lines utaona point!

Kukomediwa ni muhimu watake wasitake maana kazi ya sanaa ni nini? kukosolewa pia ni kazi ya sanaa,sasa kama hawataki kukosolewa wahamie sayari nyingine ambayo hawatakutana na mambo ya kukosolewa.

kama mtu hataki kukosolewa lazima atakuwa na matatizo ya kumtosha,kwanza ukiona unakosolewa jua hiyo ni changamoto kwako na pia itakuweka mahali pazuri pa kurekebisha yale ambayo hayajakaa sawa.
 

a free advuce kanumba , ur still young why dont u go to school now?
 
Sio Kanumba tuuu!!!!! wako wengi lakini wamejificha!!!siku yao ipo!!!!!hasa hao wanajiita masuper star!!!!
 
Bwana Gwiji wewe unamwambie mwenzio aende shule wakati wewe hata spelling za english zinakushinda advice inaandikwa hivi sio (advuce) taratibu wabongo andika kiswahili lugha yako!!!!!!!!
 
Bwana Gwiji wewe unamwambie mwenzio aende shule wakati wewe hata spelling za english zinakushinda advice inaandikwa hivi sio (advuce) taratibu wabongo andika kiswahili lugha yako!!!!!!!!

mh! sasa nani anayejua lugha? huyu naye kiswahili kimemshinda? au ni taiping era tu? kw ujumla wetu wabongo wachache sana wenye kuongea kiingereza fasaha! na hasa ni wachache zaidi wenye kuongea kiingereza cha ukweli....kwa kuangalia matamshi na matumizi ya misamiati mballimbali katika mazingira tofauti. Kutojua kiingereza siyo ishu sana kama mtu ni msanii asilia mwenye kujituma...tunaona wahindi na wachina wanajipenyeza mpaka hollywood kwa kiingereza cha kuungaunga. Nikirudi kwenye mada yetu, Kanumba anajifunza kiingereza jamani, kujua lugha kwa urahisi zaidi ni kuitumia, unakosea watu wanacheka unajirekebisha, siyo kwenda twisheni halafu unatoka bila lolote. Tufanyeni kazi kwa bidii jamani, wengine wanaongea kiingereza kizuri tu mtaani lakin wamefulia sana tu, na wengine hawajui kiingereza vizuri lakini wanafanya biashara za mamilioni ya dola na waingereza.

karagabaho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…