Wana JamiiForums wote ' tuliokwazika ' na Bondia Hassan Mwakinyo ' tumsamehe ' kwani hatimaye amemuomba Radhi ' Legend ' Rashid Matumla

Wana JamiiForums wote ' tuliokwazika ' na Bondia Hassan Mwakinyo ' tumsamehe ' kwani hatimaye amemuomba Radhi ' Legend ' Rashid Matumla

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nikiwa kama Mmoja wa Watu niliochukizwa kama siyo kukasirishwa na Kitendo Bondia Mwakinyo cha Kumdhihaki Bondia mwenye Historia iliyotukuka hapa Tanzania Rashid Matumla hadi GENTAMYCINE nikaanzisha Uzi wa Kumsema ambao uliibua Hasira Kali za Watanzania zilizosambaa sehemu mbalimbali hatimaye leo hii kupita Azam Tv Bondia Mwakinyo amemuomba Radhi Matumla na Watanzania wote kwa ujumla tukiwemo Mimi na Wewe.

Hivyo nasi hatuna budi Kiungwana kabisa Kumsamehe na Kuanzia sasa tuweke Silaha zetu chini na tumsaidie akue Kimchezo.

Kwa wale wenye Kumiliki Visimbusi / Vingamuzi vya Azam Tv leo Saa 3 na Nusu msikae mbali na Runinga zenu kwani kutakuwa na marudio yote ya tukio zima ambapo Bondia Mwakinyo alionyesha Heshima ya juu kwa ' The Legend 'Rashid Matumla huku Rashid Matumla nae akionyesha kuwa kweli Yeye ni Mkongwe na amekomaa katika Tasnia hiyo ya Ndondi nchini ambapo nae hakuonyesha ' Kinyongo ' na muda wote alikuwa akimkumbatia Kiupendo na Kumtia Moyo Bondia Mwakinyo hali ambayo inaonyesha kuwa Bondia Mwakinyo amejutia lakini pia amejifunza Kitu na sasa atabadilika.

Kwa wale ambao mlikuwa mnaudharau huu Mtandao wa JamiiForums fikirieni upya kwani kama hamjui na kwa taarifa yenu tu ni kwamba hakuna Mtandao wa Kijamii nchini Tanzania ambao unaibua mambo mengi na una ' Influence ' kubwa ndani ya Jamii ya Watanzania kama huu. Ni Maudhui na Maoni ya huu Mtandao hasa juu ya Uzi niliouanzisha na ambao wengi wenu mlichangia ndiyo umeweza Kuamsha ari kwa Watanzania wengi hadi Kupelekea na Waandishi wa Habari za Michezo nao Kufuata mtiririko na Uzi mzima hadi leo Mwakinyo ameamua Kusalimu Amri na Kuomba Radhi.

Katika hili kila mwana JamiiForums ni Mshindi hivyo unapokuwa hapa jione kuwa Wewe ni sehemu Kuu ya Mabadiliko Kijamii.
 
Ameshaomba msamaha tayari sasa hivi wako wote Live UFM.
 
kijana amesifiwa kukimbia amepitiliza mlango

ajifunze kuwaheshimu waliomtangulia kumfungulia njia

ni sawa na Messix amtukane maradona kisa ana ballon d'or 6
 
Ameonyesha ukomavu na waliokuwa wanatetea ule utoto sijui wako wapi muda huu
FB_IMG_1575535428553.jpg
FB_IMG_1575535407736.jpg
 
Uungwana ni vitendo,alichokifanya mwakinyo huo ndio ukomavu,amekiri wazi kwamba alikuwa fustrated na makonde ya mfilipino.
 
Angekuwa mada mahugo au cheka. Watu mngekaa kimya .nauona ubaguzi hapa
 
Mimi simsamehe mpaka nione akipigwa vitasa na kulambishwa sakafu katika pambano lake moja ili ajifunze kuwa kushindwa au kuzomewa ni sehemu muhimu ya mchezo pu..mbavu sana.. unatujaza taifa halafu unapigwa kibwege? Yaani unapigwa unaambiwa ukweli unabisha?.. mimi bado sijamsamehe kbs
 
Mimi simsamehe mpaka nione akipigwa vitasa na kulambishwa sakafu katika pambano lake moja ili ajifunze kuwa kushindwa au kuzomewa ni sehemu muhimu ya mchezo pu..mbavu sana.. unatujaza taifa halafu unapigwa kibwege? Yaani unapigwa unaambiwa ukweli unabisha?.. mimi bado sijamsamehe kbs
Kupigwa kashawahi kupigwa TENA BILA hata kufurukuta LABDA apigwe Mara ya pili
 
Back
Top Bottom