Nyie watu:
Mmeangalia vizuri kichwa cha habari? Ngoja niwakumbusheni, hiki hapa:
Wana JF ARUSHA Mliokwisha Kuoa/kuolewa; Ombi Langu la dhati kwenu.
Sasa kama hujakidhi hivyo vigezo usichangie. Cha ajabu walio mstari wa mbele kuchangia ni wale ambao hawajaoa/kuolewa, tena wengi wenu hampo Arusha. Halafu mnamwambia atafute solution ya haraka, ama! hiyo solution ya haraka ndiyo anayoiomba...msimrudishie tena hicho hicho alichokiomba.
Ushauri wangu sasa kwa mleta mada:
Inategemea na dhehebu ulilopo lakini nijuavyo mimi haijalazimishwa kuwa wasimamizi ni lazima wawe mke na mume. Wanaweza kuwa ni watu wenye ndoa lakini si mke na mume....unajua kazi yao wale ni mashahidi tu kuwa ndoa hiyo ilifungwa na waliishuhudia, kwisha.
"In a worst cenerio" inaruhusiwa kusimamiwa na hata mtu asiye na ndoa ama wa dini tofauti (hata muislamu). Inapendekezwa kuchukua watu wa dini yako na wenye ndoa ili wasiwe wageni wa taratibu za pale kanisani na taratibu za dini yenu kiujumla...vile vile ni rahisi kwao kuwa na ufahamu mkubwa juu ya masuala ya ndoa.
Faida ya kusimamiwa na mtu na mkewe si zaidi ya hii kuwa endapo mtapata matatizo ya kindoa basi ni rahisi kuomba ushauri kwa wasimamizi wenu ambao mnaweza kuwapata kirahisi kwa pamoja. Yaliyobaki huwa ni "SHOW"
Mkeshaji naomba nitofautiane na wewe kidogo
Msimamizi wa ndoa sio show off wala sio suala la kuchukua mtu ambaye hajaoa au hajaolewa
Sio suala la kwenda kuchukua mtu ambaye haijui ndoa wala hajawahi kuwemo kwenye ndoa kuwa msimamizi wa ndoa yako
Sio suala la kuchukua mtu ni mtu hata mnayetofautiana madhehebu kuwa msimamizi wa ndoa
Msimamizi sio anatakiwa tuu asimame pale mbele aonekane kwa kuvaa suti na gauni zuri kwa kuwa ni mpambe wa bwana na bibi arusi
Nenda kwa watu wanaojua thamani na kazi za msimamizi wa ndoa watakuambia ni nini kazi na thamani ya msimamizi wako wa ndoa
Ana majukumu zaidi ya unavyofikiria na sio kusimama pale mbele ya wafunga ndoa tuu kushuhudia ndoa yako ila ni zaidi ya hapo
Ana jukumu kwanza la kuw amsiri maana yeye ndie atakayepelekewa matatizo yote ya ndoa iwapo yatatokea. Atakuwa msuluhishi wa migogoro yote ya ndoa yenu. Kuna mambo ambayo yakitokea ndani ya nyumba mke anaweza kwenda kumweleza mzimamizi wake wa ndoa au mume kwenda kumweleza msimamizi wake wa ndoa sasa kama hata hawaishi pamoja au haawajui hata ndoa ni nini hapo watakupa ushauri gani
Mnasema wasimamizi wawe hata hawajaoa sasa watu ambao hawajaoa unategemea wawashauri nini watu ambao wanaingia kwenye ndoa
Sipingi kwamba ambao hawajaoa wanaweza kutoa ushauri ila tuangalie na taasisi ya ndoa ina mambo mengi ambayo yanatakiwa yasuluhishwe na watu ambao washaingia kwenye ndoa
Na inashauriwa hata wasimamizi wa ndoa wawe ni watu ambao wamefunga ndoa muda mrefu kiasi sio wale ambao ndoa zao ni changa