Tabia mbaya kula kwa watu, hujakatazwa na mzazi wako wa kike?
Asante bibie kwa maelezo yako. Maana yake mimi nimezaliwa na kukulia Tanga na nilikuwa najiuliza hii stima ni nini. Je ni tsima (ugali - kidigo/kirabai), au steamer (mvuke), upishi unaotumiwa kupikia samaki, wali, hata nyama. Vitunguu vingi ni muhimu kwenye nyama, maembe mabichi kwenye samaki.
Nikipita mitaa ya kwenu nikaribishe dada naona nitabweda.
Steamed fish inategemea unapika local ama kama una steamer.
1. Unaandaa samaki kwa kusafisha kabisa, pakaa chumvi, ndimu, pilipili, tangawizi na vitunguu swaumu. Acha kama nusu saa viungo vikolee.
2. Katakata karoti, hoho na vitunguu kwa size kubwa kubwa, itapendeza shape ikifanana. Unaweza kukata na mboga za majani kama kabichi ama chinese cabbage
3. weka kwenye foil nusu ya mboga mboga na kisha weka samaki kwenye foil juu ya mboga mboga na umalizie nusu ya mboga kumfunika samaki wote. Funika foil vizuri makange
4. Unaweza kumuweka samaki ndani ya sufuria yenye mfuniko. Na sufuria ikatumbukizwa ndani ya sufuria yenye maji yanayochemka na kufunikwa tena. Hii ni local steaming. Kuna microwave zina steamer, unatumbukiza ndani ya na kuweka dakika kama 20 hivi. Unaweza pia kumchoma kwa moto mdogo na mkaa ama oven na samaki ataiva kwa mvuke wa ndani ya foil.
Makange ya samaki unakaanga ama kuchoma samaki. Then kaanga vitunguu vingi, ikifuatiwa na nyanya chache. Kaanga hadi nyanya zikauke maji kabisa. Then weka hoho na carrots vinegar/ndimu (apple cider vinegar ina faida zaidi, google it) na immediately weka samaki. Pika kwa muda mfupi then geuza kupata ladha pande zote. Pika ugali na mboga za majani halafu unipigie nije kukagua
King'asti ya fish inakuwaje?plizz