Mabadiliko Lazima
Member
- Nov 12, 2012
- 7
- 0
Mimi nimezaliwa Tanzania Dar Es Salaam, asili yangu ni Mkoa waKilimanjaro. Nimesomea na kukulia Dar,kwenye miaka ya 1998 nilienda chuo nchini Uingereza. Nikiwa nchini humo nilisoma nakufanikiwa kupata shahada ya kwanza 2002.
Baada ya kumaliza masomo nikashawishika kuendelea kukaa nakufanya vibarua. Siku zikapita na visa yangu ikaisha malengo yangu kimaisha bado, 2006 nikajilipua KIRUNDI ili niendelee kuishi Uingereza na kufanikisha malengo yangu. Nilifanikiwa na kupewa miaka minne kuishi na kupewa hati ya kusafiria inayonitambulisha kama Mrundi.
Miaka minne ikaisha na kwa kuwa malengo yangu niliyokuwanayataka nimefanikiwa, nikaamua nirudi nyumbani Tanzania 2010 na kuanzisha shughuli zangu binafsi. Kwa sasa nimefungua kampuni yangu nafanya shughuli binafsi na nimeajiri vijana kumi.
Sehemu ambayo nimefungua shughuli zangu za biashara nafahamika vizuri sana na wananchi wananikubali. Mimi ni mwananchama hai wa chama kimoja kikubwa nchini. Wananchi wa sehemu hiyo wananishauri nigombee nafasi ya Ubunge 2015 kwenye jimbo hilo maana aliyepo hakubaliki sana.
Najiuliza, Je kisheria naweza gombea nafasi ya Ubunge bila kupata matatizo yeyote kutokana na background yangu ya kujilipua Uingereza?
Je nifanye nini ili niweke sawa mambo kabla ya kipindi kijachocha uchaguzi ili nisije pata matatizo baadaye?Naomba ushauri wa kisheria kwa wenye utaalamu wa mambo ya Uhamiaji na Uraia.
Hili jambo linanisumbua sana, najua nilifanya makosa hayo kwasababu ya mahangaiko ya kimaisha na hata bila hiyo sababu ya kugombea Ubunge, bado nahisi uraia wangu uko na mashaka.
Kwa nina Mke na watoto wawili.