Mie nafikiri vitu vingine tulikuwa tuaambiwa tu lakini ukitazama kiuhalisia sioni mantiki yakukataza kuvifanya; Mfano mie kule kwetu haturuhusiwi kukata kucha usiku, mwanamke haruhusiwi kukalia "ngata", haturuhusiwi kufagia usiku, haturuhisiwi kuosha vyombo ulivyolia chakula usiku, ukiuliza sababu nini unapewa jibu lisiloeleweka. Ajabu mbona huku mijini vinafanyika na sioni kinachotokea?. Nije kwenye hicho ulichouliza, mimi nina mtoto nakumbuka nilipojifungua bibiyangu alikuwa akisisitiza sana kitovu kisiangukie kwenye uume wa mtoto nilipouliza sababu nikapewa hicho ulichoambiwa. lakini nikitazama mantiki ya kusema hivyo labda wanataka tuwe makini katika ulezi na mara nyingi kitovu cha mtoto kinahitaji usafi ulio makini sana.