Wana jf nisaidieni elimu ya tanzania imeingia kirusi gani!


sasa waulize darasani walifundishwa kifaransa na wanaweza kuelezea wanayoyajua kifaransa au wanjing'atang'ata kama hawa wetu apa!
 

wewe ni mzalendo mkuu na unaujua ukweli! safi sana
 
kwa nini hujui swahili is becoming the world language.
Angalia Media mbalimbali zinatangaza kiswahili nadhani hata software za computer zimeanza kuwa za kiswahili.wanyarwanda na warundi wanajifunza kiswahili
SHTUKIA!

Safi kabisa mkuu, ila wewe chuoni umefunzwa kwa kiingereza, unataka interview ya kazi ujibu kwa kimatumbi!??
 

kinacholalamikiwa ni kushindwa kujielezea kwa kingereza na sio kuelezea utaalamu walionao.kama wasahiliwa walishindwa kuongea kingereza angewapa wajieleze kwa lugha wanayoiweza ilimradi atambue weledi waliokua nao wangeshindwa hapa ndio tungehitimisha kwamba hawajui kazi.
Kama anataka waongeaji wazuri wa kingereza nadhani tunafahamu pa kuwapata -aende england sio Tz wala Ke.
 
sasa waulize darasani walifundishwa kifaransa na wanaweza kuelezea wanayoyajua kifaransa au wanjing'atang'ata kama hawa wetu apa!

kwa hiyo unahisi vyuo vyote walivyotoka vinafundisha kwa kifaransa?
 
Safi kabisa mkuu, ila wewe chuoni umefunzwa kwa kiingereza, unataka interview ya kazi ujibu kwa kimatumbi!??
sio kimatumbi,nataka nijibu kwa kiswahili ambayo ni lugha rasmi Tanzania.
 
Naanza na wewe kwanza, kanuni za HR nikutunza siri, kwa sababu hr ni kudili na watu wa aina mbalimbali wakiwemo na hao pia. Ndio maana si kila mtu anaweza ku muintavyu mtu, iweje wewe ufanyie watu usaili then utoke uanze kutangazia watu. HR hayuko hivyo wewe mwenyewe uchunguzwe kwanza umepewaje kazi hiyo, Kitu kingine ndio maana ikawekwa intavyuu ili kupima uwezo wa watu na uelewa wao, kwa kitu kile kile ili upate ambae anaelewa zaidi na kutenda pia, wangekua wote wanalingana uelewa na kufam basi kusingekua na haja ya kuwa fanyia usaili, hata waswahili wanasema kwenye safari ya mamba hata kenge wapo, sasa ungejuaje yupi ni bora kama hao wasingekuwepo? acha kua unatoa siri za watu na za ofisi sio poa ili na wewe uwe bora:blabla::blabla:.
 
Ndugu zangu tusiwalaumu waitimu,mfumo wetu wa elimu ndo umetufikisha hapa tulipo

Na hili ndo linalolifanya taifa letu liendelee kuwa na maskini wengi wasio na kazi,wenzetu wachina,warusi n.k wameweza kutumia lugha zao na kuwapima vijana wao kwa kutumia lugha zao,vijana wanajieleza na wanapewa kazi ili kufaidi stadi zao,

sasa kwa vile sisi hatuwezi kujitegemea ndo maana hata lugha yetu haina mchango katika kuonyesha mtu anaelewa nini na anaweza kufanya nini mwishowe wanaachwa wanaendelea kuwa maskini,siamini kama mtu anamaliza chuo akiwa hajuhi kitu,mie nafikiri tungepima yote katka njia tofauti,apewe kazi ademonstrate na pili apimwa uwezo wa kuwasiliana

kazi za kijamii asilimia kubwa iwe kuwasiliana alafu zile physical wapime matendo zaidi kuliko mawasiliano,lakini hata vyuoni kwenyewe fields zimekuwa ni sehemu ya kutengeneza pesa na kufifisha maana halisi ya field,

lakini kuna sehemu ya uzoefu nayo ni lazima izingatiwe,ni wachache wanaokuwa na uwezo wa kumaster yote mwanzoni,ila kadri mda unavyoenda uweza kumshape mhusika,tusiwaache watanzania wenzetu hawa ndo kwanza wanapata exposure,baadae anaweza kumaster na akapafomu wonders
 
Ndugu zangu tusiwalaumu waitimu,mfumo wetu wa elimu ndo umetufikisha hapa tulipo

Na hili ndo linalolifanya taifa letu liendelee kuwa na maskini wengi wasio na kazi,wenzetu wachina,warusi n.k wameweza kutumia lugha zao na kuwapima vijana wao kwa kutumia lugha zao,vijana wanajieleza na wanapewa kazi ili kufaidi stadi zao,

sasa kwa vile sisi hatuwezi kujitegemea ndo maana hata lugha yetu haina mchango katika kuonyesha mtu anaelewa nini na anaweza kufanya nini mwishowe wanaachwa wanaendelea kuwa maskini na kuwa hasara kwa taifa,siamini kama mtu anamaliza chuo akiwa hajuhi kitu,mie nafikiri tungepima yote katka njia tofauti,apewe kazi ademonstrate na pili apimwa uwezo wa kuwasiliana

kazi za kijamii asilimia kubwa iwe kuwasiliana alafu zile physical wapime matendo zaidi kuliko mawasiliano,lakini hata vyuoni kwenyewe fields zimekuwa ni sehemu ya kutengeneza pesa na kufifisha maana halisi ya field,

lakini kuna sehemu ya uzoefu nayo ni lazima izingatiwe,ni wachache wanaokuwa na uwezo wa kumaster yote mwanzoni,ila kadri mda unavyoenda uweza kumshape mhusika,tusiwaache watanzania wenzetu hawa ndo kwanza wanapata exposure,baadae anaweza kumaster na akapafomu wonders
 

mkuu sikutaja jina la mtu! au na kama mtu haelewi mada ischangie mimi kwenye original post sikuwalaumu hawa vijana ila nilitoa options kama tatu ili nipate chacho halisi cha haya.
 


kaka wenzetu wa kenya hawana ile knowledge tuliyo nayo sisi ila wanajua kujieleza na kama huamini mimi najua kampuni zaidi ya kumi kati ya chache tulizo nazo ma c.e.o wake ni wakenya na mwanzoni anajieleza vizuri akipewa kazi anaanza kusema naomba training nipate japo kauzoef ka mazingira ya kazi kwani sisi tunashindwa ua ni uvivu!
 
mlichokuwa mnaangalia ni uelewa wa hao uliowainterview wa kazi wanayoiombea au ni kiingereza chao na je kiingereza kilikuwa ni moja ya qualification za kuomba kazi katika kampuni yako na je wanaenda kufanya kazi ya kuongea kiingerez aau taaluma yao

Ukweli unabaki pale pale kwamba sisi wa-TZ Kiingereza chetu ni cha kubahatisha. Ila tusiwahukumu huko chuo kikuu, tatizo liko huku kwenye msingi yaani Primary, Sekondari (yaani O-Level na A-Level). Kwa wenzetu kitoto cha primary kinaweza kukutoa jasho, hebu angalia Kenya, Rwanda na Burundi (hawa wawili kwa Kifaransa) wako vizuri.

Kwenye kampuni nyingi Kiingereza ni lazima bwana huwezi kuwekwa pale hata kama una taaluma ya kitu fulani lakini eti Kiingereza huwezi! Sasa ukitembelewa na wageni kutoka nje tuende kuazima tena makarimani? Wewe vipi wewe!!! Hivyo vijana wetu kazi bado wanayo, hata kama kichwani ni wazuri lazima wafanye jitihada na mikakati ya ziada kuweza kujua Kiingereza cha kuongea, vingeinevyo watabaki wasindikizaji na walalamikaji tu, ngoja shirikisho lije bila lugha ya wenzetu mtabaki na vyeti vyenu bila kazi!!

Hata kama una shahada yako kama hakipandi ni veyma ukaenda english course mkuu!! Shauri yenu!!!
 
Mkuu hapo umenena jambo, kwani ni lazima tukubali mapungufu tuliyonayo wa tz.
 
mkuu tembelea hapa arusha AICC ukutane na wanyarwanda,wasenegali,wacameroun e t c walivyojazana.hawajui kingereza!

Hao unaowataja walau wanajua lugha nyingine ya Umoja wa Mataifa (Maana huko kuna lugha zinazotambuliwa na kukubaliwa). Hapo sikubaliani na wewe kabisaaaa! Maana hao utakuta ni wazuri kwa Kifaransa, nenda uchunguze utatujuza!!

Maana kwenye UN system unaweza kupata kazi hata kama hujui kiingereza mradi tu unajua ama Kifaransa au Ki-Italiano n.k na siyo Kiswahili peke yake.
 

Na wewe acha uzezeta hapa!! Mbona unataka kumlazimisha jamaa aajiri watu wasioweza Kiingereza kwenye kazi inayodai kujua Lugha? Ni wa-TZ wanagapi hata kujieleza kwa Kiswahili kwenyewe ni ngoma? Tatizo hapa ni mfumo wetu wa elimu hatujajengewa mazingira ya kujieleza bwana!! Si Sekondari wala Chuo Kikuu, wote hoi!!
 

haya sasa,wale wa udsm,sua na mzumbe mnaojiitaga bora.
 
huwezi kuwekwa pale hata kama una taaluma ya kitu fulani lakini eti Kiingereza huwezi! Sasa ukitembelewa na wageni kutoka nje tuende kuazima tena makarimani? Wewe vipi wewe!!!
hopeless kabisa kwa hiyo ulitaka pasiwepo na wakalimani?kwa hiyo ukitembelewa na wachina utalazimisha kuongea kingereza hata kama hamuelewani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…