Kuna siku moja tuko na pikipiki nimempakia mshkji tunaelekea majengo..
Tumefika mataa pale ngarenaro nikaanza kusikia ukunga(nduru)jamaa anapiga kelele kuita wenzake..
Ilikuwa ni kelele kubwa akisema YULE ANAEMTTOOOMB SHEMEJI YULE PALE"
yaani jamaa alikuwa kama kapandisha kichaa..sisi kugeuka km hatuelewi kitu kwamba huyu jamaa anaesema hivyo anamlenga nani..
Kidogo zikatoka ndani baa soja km 3 hivi wakaanza kuja tulipokuwa tumesimama pale kwenye mataa..
Kuja kuangalia vizuri kidole anatuonyeshea sisi..kubabakeee
Nikawasha pikipiki ondoka pikipiki ikazima ilikuwa gia namb 4 nikapangua washa ikawaka.
Jamaa hawa hapa niliondoka pale hadi tairi ya mbele ikanyanyuka..yule soja mmoja alikuwa kavaa kombat akamdaka jamaa koti mshkaji wangu niliempakia..
Kama yule soja angekuwa hajalewa alikuwa anamchomoa mshkaji pale nyuma..
Yaani spidi tulitoka nayo hapo breki ilikuwa duka bovu..
Tulikaa kule hadi usiku ndo tukarudi mshkaji namuuliza anasema yeye hajui chochote hajawai kuwa na mke wa mwanjeshi.