Elections 2010 Wana JF Tumeiangusha CHADEMA, tumewaangusha watanzania, tumemsaliti Dr Slaa

Elections 2010 Wana JF Tumeiangusha CHADEMA, tumewaangusha watanzania, tumemsaliti Dr Slaa

CHADEMA,CUF havina udini hata kidogo,wala udini haupo kwenye mawazo ya wa tz, bali hiyo ni mbinu chafu ya ccm ya kushadadia udini ili kuimaliza CHADEMA na CUF, tuelimishane hizi mbinu chafu zisitumalize.
 
Ili tuungane inabidi Chadema kwanza wajitoe katika sera za udini,ukabila na ujimbo ndio tuanza mapambano ya kweli kuing'oa ccm.

Wewe ndiye unaye ona sera za udini ndani ya CHADEMA. Yeyote mwenye uelewa mpana anaelewa kwamba hizo ni propaganda za kuichafua CHADEMA.
 
Nchi hii ilitawaliwa miaka ipatayo 60 na wakoloni,wakoloni ni nini mfano wake ni CCM ni watu waliotawala miundombinu na democrasia ya Watanzania lakini mnamo 9th Dec 1961 yote yalipita. Achana na hiyo South Africa walitawaliwa na makaburu yapata miaka 300 ila 1994 waliandika historia mpya, 65years baada ya Martin Luther kuanzisha black revolution movement 2008 Barack Obama became the 1st Black man to manifest the revolution. I tell you my Brother Dr. Slaa is our Mandela, our Luther King. Dr. Slaa ameonyesha kuwa na uchungu wa hii nchi. A true patriot na kama wewe ni mfuatiliaji mzuri ni kwa sababu yake vijana wengi wamejitoa kuandikisha kupiga kura, na wameongeza idadi kubwa ya voice of revolution bungeni. Beautiful Tanzania is coming, BUT it begins with YOU. Usimuangalie Slaa angalia Tanzania mpya. Slaa alikuwa haubiri kwenda kujaza parking ya ikulu magari ya Ujerumani Slaa alikuwa anaangalia kwa mtazamo wa Mao (Ruler wa China) Kama China iliwezekana kwa nini hapa ishindikane? Wachina walikuwa masikini kama sisi ila iliwachukua miaka 30 kuhama kutoka poor developing country to kati ya mataifa ya G7 ambayo ndo matajiri zaidi duniani. Dr. Slaa alikuwa anatupa mtazamo wa namna ya kutengeneza maisha bora ya kweli. Usikute na yeye angeenda kujaza tumbo lake ikulu lakini at least alionyesha kuwa na mtazamo ambao wewe kwa bahati mbaya huuoni. Anza kubadilika, kwa sisi tuliompigia kura Dr. Slaa hatukumpigia yeye individually au Chadema kama chama bali tulipigia kura mitazamo ya ke na uchungu wake kwa nchi hii. Ambao hata wewe unatakiwa badala ya kuwaza kukimbia nchi na kwenda kujilipua nje utafakari namna ya kubadilisha mtazamo na kuanza kujenga nchi upya. Kumbuka hii ndo chi pekee aliyokupa Mwenyezi Mungu kuwa nchi yako bila kujilipua. Tengeneza kesho acha kuwa Myopic.
 
we have to make changes ,na watakaomake changes ni sisi watanzania hasa kizazi hiki cha vijana. inabidi tufike mahali tusijiangalie sisi tu,ila tuangalie wale babu zetu,bibi zetu,dada zetu,kaka zetu ,baba zetu wanaolala kwenye mbavu za mbwa,wanaokufa kwa kukosa dawa,eti hata panado hakuna hospitali. angalia kizazi cha shule za kata jinsi kitakavyoangamia hii ni serikali inayoweka tabaka la wenye nacho na wale masikini zaidi. tubadilike na tuwaoneshe kuwa tunaweza. 2015 we can
 
alikufa akiitaja chadema na watanzania. Sasa sema alikuwa wapi! Maana si unajua alishaikana ccm kwa kusema si baba yake wala mama yake?

mbona ktk mazishi yake ni vigogo wa ccm ndio walikuwa wakisimamia? Na hatukumuona mbowe wala slaa wakisimamia mazishi! Na hata tangazo la kifo lilitangazwa na mwenyekiti wa ccm! Sasa mwalimu alikuwa vipi mpenzi au mshabiki wa chadema? Nadhani mnataka kutuchezea akili zetu!!!
 
hebu nipeni tathmini ya malipo pamoja na marupurupu ya diwani nione kama naweza shawishika kushiriki, nipo kikazi zaidi :wave: ........................

kwa kauli yako hii haufai kwa kuwa umetanguliza maslahi binafsi badala ya utumishi kwa wananchi.
 
nchi hii ilitawaliwa miaka ipatayo 60 na wakoloni,wakoloni ni nini mfano wake ni ccm ni watu waliotawala miundombinu na democrasia ya watanzania lakini mnamo 9th dec 1961 yote yalipita. Achana na hiyo south africa walitawaliwa na makaburu yapata miaka 300 ila 1994 waliandika historia mpya, 65years baada ya martin luther kuanzisha black revolution movement 2008 barack obama became the 1st black man to manifest the revolution. I tell you my brother dr. Slaa is our mandela, our luther king. Dr. Slaa ameonyesha kuwa na uchungu wa hii nchi. A true patriot na kama wewe ni mfuatiliaji mzuri ni kwa sababu yake vijana wengi wamejitoa kuandikisha kupiga kura, na wameongeza idadi kubwa ya voice of revolution bungeni. Beautiful tanzania is coming, but it begins with you. Usimuangalie slaa angalia tanzania mpya. Slaa alikuwa haubiri kwenda kujaza parking ya ikulu magari ya ujerumani slaa alikuwa anaangalia kwa mtazamo wa mao (ruler wa china) kama china iliwezekana kwa nini hapa ishindikane? Wachina walikuwa masikini kama sisi ila iliwachukua miaka 30 kuhama kutoka poor developing country to kati ya mataifa ya g7 ambayo ndo matajiri zaidi duniani. Dr. Slaa alikuwa anatupa mtazamo wa namna ya kutengeneza maisha bora ya kweli. Usikute na yeye angeenda kujaza tumbo lake ikulu lakini at least alionyesha kuwa na mtazamo ambao wewe kwa bahati mbaya huuoni. Anza kubadilika, kwa sisi tuliompigia kura dr. Slaa hatukumpigia yeye individually au chadema kama chama bali tulipigia kura mitazamo ya ke na uchungu wake kwa nchi hii. Ambao hata wewe unatakiwa badala ya kuwaza kukimbia nchi na kwenda kujilipua nje utafakari namna ya kubadilisha mtazamo na kuanza kujenga nchi upya. Kumbuka hii ndo chi pekee aliyokupa mwenyezi mungu kuwa nchi yako bila kujilipua. Tengeneza kesho acha kuwa myopic.
sasa tufanye nini?
 
Tathmini yangu fupi ya mwenendo wa uchaguzi inaonesha kuwa kila sehemu ambayo Chadema iliweka mgombea makini, msomi, Kijana na mpiganaji wa ukweli katika Ngazi za Ubunge na Udiwani Chadema iliongoza kwa kura.

Dr Slaa alipata kura kiduchu sana maeneo ambayo chadema iliweka mgombea dhaifu ngazi ya Ubunge

Hali ilikuwa mbaya zaidi maeneo ambayo Chadema iliweka wagombea dhaifu wa Ubunge na Udiwani ni kukosa timu sahihi ya kampeni.

Wagombea Ubunge kama Thomas Nyimbo, Shitambala, Regia nk licha ya uwezo wao lakini katika baadhi ya kata waliangushwa na wagombea wasiouzika na wasiona hoja wa Udiwani.

Baada ya kutafakari kwa kina nimegundua kuwa sisi wana JF tunahusika kwani wengi wetu tungeweza kujitokeza kwenda kugombea na kuongeza kura kwa Chadema. badala ya kushabikia humu JF

Ni wakati wa kuamua sasa, Mshawishi na mwenzako tujitokeze. tutengeneze network, tufanye training za stage performance za kutosha, Tuandae wagombea serekali za mitaa na Udiwani kwenye kata zetu ili uchaguzi ujao tuweze kusaidia harakati.

Suala la kuiangamiza CCM haiwezi kufanya na Mbowe peke yake au Dr Slaa pekee, ni kazi yetu sote hasa vijana

Hima tuamke, tushikamane, tutambue wajibu wetu kwa Taifa hili

Mimi nimetangaza nia Isimani Iringa na naanza maandalizi mapemaaaaaa

2015 peopleeeeeeeezzzzzzzzz

NAKUBALIANA NA HOJA ZA MTOA MADA 100%, LAKINI HALI HII ILICHANGIWA NA CHADEMA KUMTAMKA MGOMBEA URAIS DR SLAA BAADA YA MUDA WA WAGOMBEA WA NAFASI MBALI MBALI KUCHUKUA FOMU NA KUOMBA UTEUZI. HIVYO MOTO ALIOUWASHA DR SLAAA HAUKUISAIDIA SANA CHADEMA KUPATA WAGOMBEA BORA ZAIDI YA HAO WALIOKUWA WAMEJITOKEZA AWALI. KWA MANENO MENGINE HAO WALIOJITOKEZA NDIO WAGOMBEA HALISI WALIOKUWA TAYARI KUFA NA CHADEMA GOI GOI AU IMARA KAMA ILIVYO SASA. HIVYO HAKUNA LILILOHARIBIKA SANA.

NIMESOMA MAONI YA WACHANGIAJI WENGI HUMU NDANI KUHUSU KUJIANDAA KUGOMBEA UCHAGUZI MKUU WA 2015. NAFIKIRI APPROACH SAHIHI NI TUJITAYARISHE KUSHIKA UENYEKITI NA UJUMBE WA SERIKALI ZA VIJIJI, VOTONGOJI NA MITAA YA MIJINI MWAKA 2014.

HALAFU NDIPO TUINGIE KATIKA UCHUGUZI MKUU WA 2015 TUKIWA NA NGUVU MPYA.

NAMNA BORA ZAIDI YA KUJITAYARISHA NI KUANZA UTUMISHI KWA WANANCHI HIVI SASA NA SIO KUSUBIRI MIEZI MICHACHE KABLA YA UCHAGUZI 2014 NA 2015. KATIKA KATA NA MAJIMBO AMBAPO MADIWANI NA WABUNGE WA CHADEMA WALISHINDA TUNAWEZA KUUNGANA NA WATEULE WETU KATIKA KUIBUA KERO ZA WANANCHI; KUBUNI MIKAKATI YA KUTATUA KERO HUSIKA KWA KUSHIRIKISHA WANANCHI NA HATIMAYE KUSHIRIKI KATIKA UTATUZI WAKE. KWA NAMNA HIYO TUTAKUWA TUMEJITAMBAULISHA MBELE YA WANANCHI KAMA WATUMISHI BORA KUTOKA CHAEMA NA HIVYO KAUFANYA KAMPENI ZETU KUWA RAHISI ZAIDI. iKUMBUKWE KUWA KAMA ILIVYO CCM, MWAKA 2014 NA 2015 CHADEMA NAYO ITAKUWA NA WAGOMBEA WENGI KATIKA VINYANG'ANYIRO VYA KURA ZA MAONI KUWAPATA WAGOMBEA WAKE WA VIJIJI, VITONGOIJI,NA MITAA MWAKA 2014; NA UDIWANI NA UBUNGE 2015. HIVYO KAMA TUTAANZA UTUMISHI KWA WANANCHI HIVI SASA TUTAFANIKIWA KUPITA KATIKA KURA ZA MAONI KIRAHISI NA HATIMAYE KUWA WAGOMBEA BORA WA CHADEMA
.


KATIKA MAENEO AMBAOPO HAKUNA MADIWANI NA WABUNGE WA CHADEMA WAGOMBEA WATARAJIWA WANAWEZA PIA KUANZISHA KAZI NILIZOZITAJA HAPO JUU KWA NIA YA KUJITAMBULISHA MBELE YA WANANCHI PIA


USHAURI KWA CHADEMA WALE WATAKAOPITISHWA KUGOMBEA WAWE NI WALE AMBAO KATIKA KIPINDI HIKI WALIJITUMA KUFUNGUA MATAWI, MISINGI NA KUITAFUTIA CHADEMA WANANCHAMA WA KUDUMU.
.
 
Back
Top Bottom