Wana JF, uandishi wa lugha mchanganyiko ni uchafu! Ni sawa na kuhifadhi sufuria kitandani (kero)

Gaddaf i06

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2022
Posts
1,770
Reaction score
2,841
Kwanza kabisa, nakutakia afya njema kama ya kwangu..

Bila kinyongo kabisa naomba niweke hapa kero yangu juu ya waandishi baadhi wa hoja hapa jf

Kama utaguswa tafadhali usikasirike wala kutukana, ni kitu ambacho kinafanywa na watu wengi, hata hvyo si kero kwa wengi/wote.

Ruksa kutoa kero yako pia ili tujifunze!

Kero yangu nambari # 1
ni habari zinazoandikwa kwa mfumo wa 'kiswanglish'
mfano:
~Before we met, nilikuwa interested sana, bt the more we got used to each other basi nilimwona wa kawaida!
~When i was fired nilipata conection kwenye institution kubwa hapa tz[emoji16][emoji16]
(ni mifano)

Binafsi napenda kuona uzi ulioandikwa Kwa kiingereza a-z
Ama kiswahili a-z
Inapendeza sana

Nina kero 3, bado 2
 
Hii inatokana na kuwa, Kiswahili chetu hakijajitosheleza kwa hakika. Si kwa maana ya misamiati, bali kwa uelewa na ujuzi wake.Kuna maneno ambayo humaanisha sana endapo utaiandika kwa lugha tofauti.

Ukitaka kuandika kwa Kiswahili nyoofu, hata hadhira yako inaweza isikuelewe barabara.

Ukikutana na maandiko ya Kiswahili yenyewe, hata wewe itakuwia ugumu mno kuelewa andiko hilo.
 
If u do nat like jus never bother your self quit the thread. Mim napenda sana so wew pambana na vile unavo penda ila usitupangie how to portray our own
Sijakupangia mkuu!
lakini ukifaanya unachopenda wewe mbele ya hadhara, sio kwamba wote watapenda
 
Hii inatokana na kuwa, Kiswahili chetu hakijajitosheleza kwa hakika. Si kwa maana ya misamiati, bali kwa uelewa na ujuzi wake.Kuna maneno ambayo humaanisha sana endapo utaiandika kwa lugha tofauti.

Ukitaka kuandika kwa Kiswahili nyoofu, hata hadhira yako inaweza isikuelewe barabara.

Ukikutana na maandiko ya Kiswahili yenyewe, hata wewe itakuwia ugumu mno kuelewa andiko hilo.
haya maoni yako ni mfano mzuri sana!
 
Ni lini,wapi,kwa maneno yepi kiswahili hakijajitosheleza?Kuna changamoto kubwa sana kwa waandishi wanaochanganya lugha mbili au tatu.
-kutopenda kujifunza misamiati mipya,
-kukosa misamiati mingi vichwani mwao,
-kujionesha kwa ujuaji tu kwamba anayo mengi bichwani,
-uzembe tu na kutojali anawasiliana na hadhira ipi,
-kuficha au kupunguza ukali wa maneno kwa kutumia lugha ya pili au ya tatu,
-kuishi kwa kudhania tu kwamba anaeleweka,
-kukataa kuwa hajui na kutumia lugha ngeni/ya pili kujijumuisha kundini,
-ni njia ya kujifunza na kuzoea matumizi ya maneno ya lugha nyingine,
-uhuniuhuni tu,
-kuandika wakati hayupo sawa kifikra aidha kwa kutumia vilevi,msongo wa mawazo au kukurupuka,
-kujipima kama masomo yake ya ziada kuhusu lugha yanafanya kazi au amehitimu,
-usumbufu aidha wa kirika au kutenga wengine wasielewe akijidai anaweka mafumbo.
NB:Yapo mengi sana.Kwa hayo "machache",unaweza kuongeza mengine.
 
hakika hujabahatisha!
 
Sure kabisa i think ni cause ya kukosa uelewa tu,wanafikiri wakiandika hivo comminity itawaona ni watu intelligent
🤣🤣🤣🙌🏽 i see what you did there ... i like it and ...
OP hebu punguza makasiriko kwanza
 
Back
Top Bottom