Mechi iyo unayosema mpaka half time ilikua 0-0 Refa alikua yule jamaa anaitwa Abdul Kadri ana Asili ya kisomali. Kocha wa Yanga Alikua marehemu Mziray.
Wakati timu zinaingia uwanjani kabla ya kuanza mpira Mziray aliwaonyesha alama ya vidole viwili mashabiki wa Simba akimaanisha watakufa goli 2.
Alikua Akicheza na saikolojia ya Simba na kweli kipindi Cha pili Wakati wachezaji wanatoka vyumbani wachezaji wengine waliingia uwanjani wengine walielekea kule usawa wa vyooni walipo paki basi lao.
Inaonekana ata viongozi waligawanyika juu ya kutoa timu uwanjani.
Mwishowake wakaweka mpira kwapani.