Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. CHADEMA wana macho? Je, wawasamehe Wabunge 19 wabarikiwe, au wakomae nao walaaniwe?

Very well spoken. Many thanks mkuu. Nje ya hapa ni kuhangaika na ubatili. I hope mleta mada hataendelea kupoteza muda na suala lisilo na tija.
 
Paskali naomba unifafanulie hili, mathlani Chadema wamewasamehe hao 19 je, yule aliyetolewa gerezani(nina uhakika Chadema haikuwa na mamlaka hiyo) atarudishwa gerezani?
 
Ni kweli maana naona kama anawabeba mgongoni kiaina na hataki kuona walichokifanya, bali anaona tu Chadema wanachotakiwa kufanya kuhusiana na hao 19.
Tujaribu kutafiti chuki za Paskali dhidi ya Chadema zilianza nini na nini ilikuwa chanzo na hasa dhidi ya Mbowe jambo ambalo yeye halifichi, binafsi ninaamini Mbowe akitoka Chadema Paskali atazaliwa upya, roho yake itakuwa huru.
 

Nyie wanafiki sana. CHADEMA wawasamehe akina Halima wakati hawataki msamaha.
 

Sio kweli. Kwa Sasa akina Halima na bulaya wameflop Sana. Kinachowapa relevance ni kwamba wapo bungeni
 
Naunga mkono hoja 💯 🙏
Hata Mkuu wa Nchi amepewa madaraka ya kumsamehe yeyote yule aliyefungwa na anatumikia kifungo !!
Kwanini kwa Chadema Chama makini kinashindwa kusamehe ??!!
Hata maandiko yanasema Ukisamehe nawe Utasamehewa !! 🙏🙏🙏
 
Paskali naomba unifafanulie hili, mathlani Chadema wamewasamehe hao 19 je, yule aliyetolewa gerezani(nina uhakika Chadema haikuwa na mamlaka hiyo) atarudishwa gerezani?
Rais anaruhusiwa na Katiba kumsamehe yeyote yule hata kama alihukumiwa kifungo cha maisha !!
 
Ya Kaizari apewe Kaizari, bali ya Mungu apewe Mungu. Kutafuta huruma katika mchezo mchafu wa kisiasa kupitia mizania ya kiimani ni kitu ambacho kinakosa mantiki kabisa. Unawezaje kutanguliza msamaha kwa mtu ambaye hasukumwi ama kuwiwa kufanya hivyo.

Kupitia tafsiri ya mahakama, hao kina mama walikwisha vuliwa uanachama wao na KK ya CDM, ikiwa na maana kwa sasa sio wanachama tena na wamepoteza sifa ya kukiwakilisha chama kwa namna iwayo yoyote ile. Kwa tafsiri hiyo hiyo pia ni kwamba wanachokipigania ni haki yao ya kusikilizwa rufaa yao mbele ya Baraza Kuu.

Mimi natambua sina uelewa mkubwa wa mambo ya kisheria, lakini natambua mchakato wa akina mama hawa kujipatia nafasi hizo za kibunge haukuwa halali wala hakufuata utaratibu wa kisheria, hali iliyopelekea wao kuvuliwa uanachama. Na hapo walipo wao si wanachama tena wa CDM.

Na wala sidhani kama kuna tamko la mahakama ya wao "being stay away from execution" kupitia maamuzi ya KK ya CDM. Labda wajuvi wa sheria watufafanulie kuhusiana na uhalali wa uanachama kwa hivi sasa.
 
Tujaribu kutafiti chuki za Paskali dhidi ya Chadema zilianza nini na nini ilikuwa chanzo na hasa dhidi ya Mbowe jambo ambalo yeye halifichi, binafsi ninaamini Mbowe akitoka Chadema Paskali atazaliwa upya, roho yake itakuwa huru.
Mkuu, kama umemfuatilia Mayala kwa muda mrefu ni rahisi kujua target zake nim zipi. Hana chuki na Mbowe, na hata akitoka CHADEMA (Mbowe), bado (Mayala) ataendelea kuiattack CHADEMA chini ya kivuli cha kujifanya anaishauri.

Mayala anatafuta teuzi/cheo kule CCM, na baada ya kufeli kukubalika ndani ya chama chake, ameamua kuchagua namna mpya ya kujijenga. Amechagua kuiattack CHADEMA, na hao kina Mdee ni mtaji wake. Anguko la CHADEMA ni neema kwa CCM, inaleta mashaka kuona mwanaccm anaipa ushauri CHADEMA namna gani ifanye ili kuwa Imara. Mayala amekuwa too predictable siku hizi, haihitaji akili nyingi kufahamu bandiko lake lijalo atazungumzia nini.
 
Mkuu Drifter, honest and genuineness ya mtu inakaa ndani yake, ila pia ni kama ilivyo justice, must not only be done, but must be seen to be done!.

Ushauri honest and bonafide genuine must be seen with naked eyes.
Kama mtu anaye toa ushauri kama huu, unauona ni ushauri wa ki Yuda Eskariote na kuniulizia how many “pieces of silver”?, then naomba niheshimu mawazo yako kwasababu watu hatufanani, and we don't think the same!.

P
 
CHADEMA WANAFANYA MAMBO YA KITOTO SANA....

WENZAO WANAGROUM CHIPUKIZI WAO WAMEKAZANA NA AKINA BIBI MDEE

SHENZIIIIIIII KABISA
 
Kwasasa nimeanza kupata wasiwasi kuwa hizi ni sarakasi tu za kuwazuga wanachama vichaa kama akina Boni, Mdude na Martin, ili kuvuta muda hadi 2025 ikabie. watasameheana kisha maisha ya hadaa yataendelea.

Maamuzi ya mahakama yako wazi, what needs to be done is clear, but Mnyika is bragging on the media about writing to Madam Speaker sijui to remind her to kick akina Mdee out. Isn’t that madness??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…