Wanabodi
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa, Chadema ni chama cha Kitaifa hivyo haya yanayoendelea ndani ya Chadema katika huu mgogoro wake na wabunge wake 19 wa viti maalum, una athari za Kitaifa zenye maslahi kwa taifa. Hoja yangu ya leo ni hii ,"kuna watu wana macho lakini hawaoni!, na wana masikio lakini hawasikii!". Swali ni je Chadema wana macho na yanaona?. Je wana masikio na yanasikia?. Kwenye hili la Wabunge 19, je Chadema wawasamehe wabarikiwe, au waendelee kukomaa nao mpaka kieleweke hata kama ni kulaaniwa?.
Naomba kukiri kupandisha bandiko hili, kwa inspirational kutoka andiko la Kaka yangu/mdogo wangu na bosi wangu kule TEF, Deodatus Balile.
Balile ameandika bandiko hili akiwa safarini jijini New Delhi nchni India.
C&P ya Balile
Mwisho wa kunukuu
Chief @Balile , nikiwa New Delhi nilijifunza imani ya Hinduism kuhusu kitu kinachoitwa karma, hivyo ushauri wako kwa Chadema, utawaepushia Chadema karma ya mambo
mabaya waliowatenda hawa wadada 19 ambao mimi nawaita ni mashujaa, hivyo huu ni ushauri mzuri, wa hekima na busara sana kwa Chadema wenye maslahi kwa Chadema na maslahi kwa taifa only if Chadema wana macho ya kuona na wanaona, na wana masikio ya kusikia na wanasikia, kwasababu kuna watu wana macho lakini hawaoni, na wana masikio lakini hawasikii.
Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anakabiliwa na kesi ya ugaidi, nilipandisha makala mfufulizo za Kilio cha Haki, nikiangazia haki jinai.
Kwenye sala yetu ya Baba Yetu, kuna mstari "Utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea" hivyo tulimpongeza rais Samia kwa kauli hii baada ya Freeman Mbowe kuombewa msamaha
Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?
Baada tuu ya bandiko hili, haukupita muda hatimaye Freeman Mbowe alisamehewa na kesi ya Mbowe ilifutwa!,
Sisi wa kupongeza tukapongeza
Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
Sasa kuna ugumu gani Chadema kuwasamehe hawa wabunge wake 19?.
Hili sakata la wabunge hawa toka lilipoanza, mimi nimekuwa very open, objective and very transparent
Na nikashauri Chadema
Katika Salaam zangu kwa mwaka mpya,
Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa, wakipata vema na kupendana. Tulikotoka ni kugumu, tunakokwenda ni kurahisi, kuzuri! Heri ya Mwaka Mpya wahusika wote
Japo kwa jicho la juu juu, hao 19, wanaonekana kama wameshinda kesi yao mahakamani but in reality ni wameshindwa na hili nililisema
The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia! kwasababu katiba ya Chadema ina kipengele kilicho kinyume cha katiba, mwanachama wa Chadema akifungua shauri lolote mahakani, akishindwa kesi ni amejifukuzisha, hivyo Mahakama tayari imeishabariki kufukuzwa kwao, salama yao ni kusamehewa tuu!.
Kwa vile mimi namfahamu Freeman Mbowe kuliko Chadema wengi, Mbowe ni muungwana, Mbowe ni mtu wa shukrani, na baada ya kikao cha CC kuwatimua, Freeman Mbowe aliingia huruma na kufukuzwa kwao, akawasamehe, akawaita Nairobi, akawasamehe, akawashauri waombe msamaha, ili wayamalize, wakamgomea!.
It's high time Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Aikael Mbowe, kuitumia kofia yake ya Uenyekiti wa Chadema kwa kuitekeleza kwa vitendo sala ya Baba Yetu, kwa mtindo wa reciprocity kama yeye alivyosamehewa bila kuomba msamaha, sasa ni zamu ya na yeye kusamehe tuu bila kuombwa msamaha?., au Chadema iendelee kukomaa nao ili kuwaonyesha, kuwakomoa na kuwanyorosha?.
Tena na mimi kwa vile ubavu wangu ni pande za Kaskazi, na mimi nimeunga tela hija za migombani.
Merry Christmas
Paskali.