Waombe tu kama bado hawajaomba !!Kwani wameomba msamaha..?
Kwani wakisamehewa Chama kitakuwa kimepoteza kitu gani kikubwa ??!Ya Kaizari apewe Kaizari, bali ya Mungu apewe Mungu. Kutafuta huruma katika mchezo mchafu wa kisiasa kupitia mizania ya kiimani ni kitu ambacho kinakosa mantiki kabisa. Unawezaje kutanguliza msamaha kwa mtu ambaye hasukumwi ama kuwiwa kufanya hivyo.
Kupitia tafsiri ya mahakama, hao kina mama walikwisha vuliwa uanachama wao na KK ya CDM, ikiwa na maana kwa sasa sio wanachama tena na wamepoteza sifa ya kukiwakilisha chama kwa namna iwayo yoyote ile. Kwa tafsiri hiyo hiyo pia ni kwamba wanachokipigania ni haki yao ya kusikilizwa rufaa yao mbele ya Baraza Kuu.
Mimi natambua sina uelewa mkubwa wa mambo ya kisheria, lakini natambua mchakato wa akina mama hawa kujipatia nafasi hizo za kibunge haukuwa halali wala hakufuata utaratibu wa kisheria, hali iliyopelekea wao kuvuliwa uanachama. Na hapo walipo wao si wanachama tena wa CDM.
Na wala sidhani kama kuna tamko la mahakama ya wao "being stay away from execution" kupitia maamuzi ya KK ya CDM. Labda wajuvi wa sheria watufafanulie kuhusiana na uhalali wa uanachama kwa hivi sasa.
Mhaini hasamehewi kumsamehe ni sawa na kukaribisha uhaini zaidi au kuwambia kuna watu ni bora au wana nguvu kuliko chama. Mtu akifanya uhaini, haijalishi ni nani ni afadhali aondokeWanabodi
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa, Chadema ni chama cha Kitaifa hivyo haya yanayoendelea ndani ya Chadema katika huu mgogoro wake na wabunge wake 19 wa viti maalum, una athari za Kitaifa zenye maslahi kwa taifa. Hoja yangu ya leo ni hii ,"kuna watu wana macho lakini hawaoni!, na wana masikio lakini hawasikii!". Swali ni je Chadema wana macho na yanaona?. Je wana masikio na yanasikia?. Kwenye hili la Wabunge 19, je Chadema wawasamehe wabarikiwe, au waendelee kukomaa nao mpaka kieleweke hata kama ni kulaaniwa?.
Naomba kukiri kupandisha bandiko hili, kwa inspirational kutoka andiko la Kaka yangu/mdogo wangu na bosi wangu kule TEF, Deodatus Balile.
Balile ameandika bandiko hili akiwa safarini jijini New Delhi nchni India.
C&P ya Balile
Mwisho wa kunukuu
Chief @Balile , nikiwa New Delhi nilijifunza imani ya Hinduism kuhusu kitu kinachoitwa karma, hivyo ushauri wako kwa Chadema, utawaepushia Chadema karma ya mambo
mabaya waliowatenda hawa wadada 19 ambao mimi nawaita ni mashujaa, hivyo huu ni ushauri mzuri, wa hekima na busara sana kwa Chadema wenye maslahi kwa Chadema na maslahi kwa taifa only if Chadema wana macho ya kuona na wanaona, na wana masikio ya kusikia na wanasikia, kwasababu kuna watu wana macho lakini hawaoni, na wana masikio lakini hawasikii.
Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anakabiliwa na kesi ya ugaidi, nilipandisha makala mfufulizo za Kilio cha Haki, nikiangazia haki jinai.
Kwenye sala yetu ya Baba Yetu, kuna mstari "Utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea" hivyo tulimpongeza rais Samia kwa kauli hii baada ya Freeman Mbowe kuombewa msamaha
Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?
Baada tuu ya bandiko hili, haukupita muda hatimaye Freeman Mbowe alisamehewa na kesi ya Mbowe ilifutwa!,
Sisi wa kupongeza tukapongeza
Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
Sasa kuna ugumu gani Chadema kuwasamehe hawa wabunge wake 19?.
Hili sakata la wabunge hawa toka lilipoanza, mimi nimekuwa very open, objective and very transparent
Na nikashauri Chadema
Katika Salaam zangu kwa mwaka mpya, Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa, wakipata vema na kupendana. Tulikotoka ni kugumu, tunakokwenda ni kurahisi, kuzuri! Heri ya Mwaka Mpya wahusika wote
Japo kwa jicho la juu juu, hao 19, wanaonekana kama wameshinda kesi yao mahakamani but in reality ni wameshindwa na hili nililisema The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia! kwasababu katiba ya Chadema ina kipengele kilicho kinyume cha katiba, mwanachama wa Chadema akifungua shauri lolote mahakani, akishindwa kesi ni amejifukuzisha, hivyo Mahakama tayari imeishabariki kufukuzwa kwao, salama yao ni kusamehewa tuu!.
Kwa vile mimi namfahamu Freeman Mbowe kuliko Chadema wengi, Mbowe ni muungwana, Mbowe ni mtu wa shukrani, na baada ya kikao cha CC kuwatimua, Freeman Mbowe aliingia huruma na kufukuzwa kwao, akawasamehe, akawaita Nairobi, akawasamehe, akawashauri waombe msamaha, ili wayamalize, wakamgomea!.
It's high time Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Aikael Mbowe, kuitumia kofia yake ya Uenyekiti wa Chadema kwa kuitekeleza kwa vitendo sala ya Baba Yetu, kwa mtindo wa reciprocity kama yeye alivyosamehewa bila kuomba msamaha, sasa ni zamu ya na yeye kusamehe tuu bila kuombwa msamaha?., au Chadema iendelee kukomaa nao ili kuwaonyesha, kuwakomoa na kuwanyorosha?.
Tena na mimi kwa vile ubavu wangu ni pande za Kaskazi, na mimi nimeunga tela hija za migombani.
Merry Christmas
Paskali.
Kumsamehe mhaini ni kumwambia yeye ni mkubwa kuliko chama na ni untouchable. Hii itasababisha uhaini mwingine huko mbeleni. Hata CCM haiwezi kulikbali hili. Ni afadhali liwalo na liwe ila wasiwasamehe.Kwani wakisamehewa Chama kitakuwa kimepoteza kitu gani kikubwa ??!
Makamanda walikipigania sana chama chao before that evil took place !!
Duniani hakuna mkamilifu !!
Muwasamehe tu nanyi mutasamehewa na mutabarikiwa !! 🙏🙏
Anyway mimi nilikuwa rafiki wa late kaka yake Mbowe wakianzia Splendid na mzee Mbowe kabla ya kuuza eneo na kuhamia huko.Mkuu Hismastersvoice , I don't know how old you are, ila uliwahi kusikia kipindi kinaitwa Kiti Moto?, na kilikuwa kinaendeshewa wapi?.
Kwa kukusaidia wewe na wengine, kipindi cha Kiti Moto, kilikuwa kinaendeshewa Kilimanjaro hotel na Club Billicanas, mimi wakati naoa vikao vyangu, harusi yangu tumeendeshea Club Billicanas na ukumbi ni Freeman Mbowe ametupa bure!.
Hivyo Mbowe ni rafiki yangu mkubwa na tumetoka nae mbali toka enzi za Mbowe Hotels hivyo sina chuki yoyote na Mbowe, kosa langu kubwa ni kupenda haki, kosa kubwa la Chadema ni kutotenda haki.
Unaweza kuniangalia nilizungumza na Mbowe usikilize kwa makini nimesema nini kuhusu mimi na Freeman
View: https://youtu.be/fxDX_gkCE1E?si=kXh5FLNJxYynqi_gPasco
Mkuu Telesphore Magobe T, mimi niko very honest, najihesabu ni mtetezi huru wa haki, na hata kama ni wakosefu wanaostahili kuhukumiwa kufukuzwa, basi wahukumiwe kwa haki, kama ni kufukuzwa wafukuzwe kwa haki.
Sii wengi humu wanaijua na wameisoma w
katiba ya Chadema, mimi naijua katiba ya Chadema nimeisoma kinyume nyume!.
Nimeamua kujitokeza wazi sio ili kuingilia mambo ya ndani ya Chadema bali kujiridhisha kuwa katika fukuza fukuza hii ya hawa 19, jee haki imetendeka?, wanachama wale wamehukumiwa na haki kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za Katiba ya CHADEMA?.
Mamlaka binafsi ya kuingilia mambo ya ndani ya CHADEMA, ni kwa mujibu wa katiba nchi, kipengele cha uhuru wa kutoa maoni na haki ya kiraia kwa "public bodies" ambapo japo CHADEMA ni taasisi huru yenye mamlaka kamili ya kujifanyia mambo yake yenyewe, CHADEMA pia ni taasisi ya umma, public party, inayo gharimiwa na fedha za umma, public money, ambazo ni kodi yetu hivyo "the public has the right to know its public as well as its private conduct!".
Swali la kwanza la kujiuliza ni
Wito faraja kwa wadhulumiwa wote wanaonyanyaswa na kudharauliwa kwa ajili ya kupigania haki yao ndani ya Chadema hadi kufukuzwa kama mbwa!. Kama nyinyi ni watu wa haki, msihofu na kutimuliwa Chadema, Mungu yupo na ni mkubwa zaidi ya Chadema. Mungu atawasinamia na kokote muendako atawainua na kuwalipia, itakuwa ni story ya ," jiwe walilolikataa waashi litafanywa kuwa jiwe Kuu la pembeni", mnaweza kuinuliwa hadi Chadema kuja kuwapigia magoti huko mbele ya safari.
- Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa na miongoni mwake ni hizi nitakazo ziorodhesha hapa chini, jee zilifuatwa?.
- Kuandaa Hati ya Mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?.
- Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia, jee hili lilifanyika?, nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, kuna watu waliitwa kwa WhatsApp na barua zimetumwa kwa WhatsApp jee huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?.
- Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, jee hili lilifanyika?.
- Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kumpa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee kwenye huo uamuzi uliotangazwa jana na Bavicha, Jee sheria, taratibu na kanuni zilifuatwa?!.
- Kanuni ya kwanza ya haki ni "no body is condemned unheard!". Yaani hakuna yoyote atakayehukumiwa bila kusikilizwa!. Wameitwa kienyeji enyeji, wakagoma wamehukumiwa in "absentia" bila kusikikizwa, hii ni haki?.
- Nawasisitiza Chadema kutenda haki ili pia kuepuka hukumu ya kitu kinachoitwa karma isije kuwakumba kwa siku za usoni. Ukiwatendea watu uovu au ubaya kwa kuwaonea, bakora za karma ya uovu ule zitakuja kuitandika Chadema siku zijazo.
Ushauri huu lengo lake ni kutuaminisha sisi Watanzania wengine tusio wanachama wa CHADEMA, kuwa Chadema ni chama cha haki na kinafanya maamuzi yake kwa haki kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni za haki, hivyo kutupa matumaini kuwa CHADEMA inaweza kuaminiwa na kukabidhiwa nchi mwaka 2025!, vinginevyo kwa mambo haya kama yalivyo sasa, na kama CHADEMA haitabadilika, then kwa 2025 CHADEMA itakuwa bado haijakomaa kiasi cha kutosha kuaminika na kukabidhiwa nchi!, hivyo 2025 ni CCM tena.!.
P
Mkuu Hismastersvoice , I don't know how old you are, ila uliwahi kusikia kipindi kinaitwa Kiti Moto?, na kilikuwa kinaendeshewa wapi?.
Kwa kukusaidia wewe na wengine, kipindi cha Kiti Moto, kilikuwa kinaendeshewa Kilimanjaro hotel na Club Billicanas, mimi wakati naoa vikao vyangu, harusi yangu tumeendeshea Club Billicanas na ukumbi ni Freeman Mbowe ametupa bure!.
Hivyo Mbowe ni rafiki yangu mkubwa na tumetoka nae mbali toka enzi za Mbowe Hotels hivyo sina chuki yoyote na Mbowe, kosa langu kubwa ni kupenda haki, kosa kubwa la Chadema ni kutotenda haki.
Jamaa ni kada wa Ccm na mmoja wa watia nia wa ubunge na nafasi nyingine za kisiasa, hivyo lazima ajitengenezee mazingira ya kuonekana hayupo nyuma sana kwenye kuunanga Upinzani Chadema hasa hasa kama makada wenzake.Wewe mkuu una tatizo kubwa sana. Kimsingi, lengo la mfumo wa vyama vingi vya siasa ni kuwapa nguvu wananchi kuchagua viongozi wao na kuamua mustakabali wa nchi yao. Hata CHADEMA ikifa leo hii haitakuwa mwisho wa upinzani. Mapambano ya wananchi yataendelea kwa namna zozote zile.
Ni ajabu kwamba wewe unatumia nguvu nyingi sana kuandika mabandiko kadhaa yanayoishutumu (unadai unaishauri) CHADEMA kama vile ndiyo inayoharibu mustakabali wa nchi hii. Unataka CHADEMA ipokee na kukubali kila adha inayoletewa na serikali ya CCM. Eti ikubali kila “nusu shari” ili i-survive; isife kimoja! Ingekuwa wewe ni kada au mfuasi makini wa CHADEMA ingefikirisha. Ingekuwa ni ushauri wa mara moja tungesema well, huenda ni jambo la kawaida. Lakini hii toka kwa mtu mwenye mitazamo ya kijanja janja ni zaidi OBSESSION kabisa!
You’re not honest my friend. Anyone can clearly see that you’re on a one track mission to bring CHADEMA down on its knees before the might of the state. For exactly what gratification OR how many “pieces of silver”? That remains to be seen.
HapanaMkuu malantu , umeisha wahi kukisikia kitabu kinaitwa "An Enemy of the People " kilichoandikwa na Hendrix Ibsen?
P
Waombe tu kama bado hawajaomba !!
Na wakiomba wasianze kuulizwa maswali mengi kwamba ilikuwaje au nani nani alifanya nini !! Hiyo itakuwa ni sawa na kuanzisha kesi mpya !!
1. Of course, kupigania au kutetea haki za watu ni jambo muhimu kiongozi. Hata mimi napenda iwe hivyo. In fact, ndiyo matakwa ya kila mtu mwenye mapenzi mema - haki itendeke - kila upande utende haki na utimize wajibu wake.Mkuu Telesphore Magobe T, mimi niko very honest, najihesabu ni mtetezi huru wa haki, na hata kama ni wakosefu wanaostahili kuhukumiwa kufukuzwa, basi wahukumiwe kwa haki, kama ni kufukuzwa wafukuzwe kwa haki.
Sii wengi humu wanaijua na wameisoma w
katiba ya Chadema, mimi naijua katiba ya Chadema nimeisoma kinyume nyume!.
Nimeamua kujitokeza wazi sio ili kuingilia mambo ya ndani ya Chadema bali kujiridhisha kuwa katika fukuza fukuza hii ya hawa 19, jee haki imetendeka?, wanachama wale wamehukumiwa na haki kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za Katiba ya CHADEMA?.
Mamlaka binafsi ya kuingilia mambo ya ndani ya CHADEMA, ni kwa mujibu wa katiba nchi, kipengele cha uhuru wa kutoa maoni na haki ya kiraia kwa "public bodies" ambapo japo CHADEMA ni taasisi huru yenye mamlaka kamili ya kujifanyia mambo yake yenyewe, CHADEMA pia ni taasisi ya umma, public party, inayo gharimiwa na fedha za umma, public money, ambazo ni kodi yetu hivyo "the public has the right to know its public as well as its private conduct!".
Swali la kwanza la kujiuliza ni
Wito faraja kwa wadhulumiwa wote wanaonyanyaswa na kudharauliwa kwa ajili ya kupigania haki yao ndani ya Chadema hadi kufukuzwa kama mbwa!. Kama nyinyi ni watu wa haki, msihofu na kutimuliwa Chadema, Mungu yupo na ni mkubwa zaidi ya Chadema. Mungu atawasinamia na kokote muendako atawainua na kuwalipia, itakuwa ni story ya ," jiwe walilolikataa waashi litafanywa kuwa jiwe Kuu la pembeni", mnaweza kuinuliwa hadi Chadema kuja kuwapigia magoti huko mbele ya safari.
- Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa na miongoni mwake ni hizi nitakazo ziorodhesha hapa chini, jee zilifuatwa?.
- Kuandaa Hati ya Mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?.
- Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia, jee hili lilifanyika?, nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, kuna watu waliitwa kwa WhatsApp na barua zimetumwa kwa WhatsApp jee huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?.
- Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, jee hili lilifanyika?.
- Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kumpa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee kwenye huo uamuzi uliotangazwa jana na Bavicha, Jee sheria, taratibu na kanuni zilifuatwa?!.
- Kanuni ya kwanza ya haki ni "no body is condemned unheard!". Yaani hakuna yoyote atakayehukumiwa bila kusikilizwa!. Wameitwa kienyeji enyeji, wakagoma wamehukumiwa in "absentia" bila kusikikizwa, hii ni haki?.
- Nawasisitiza Chadema kutenda haki ili pia kuepuka hukumu ya kitu kinachoitwa karma isije kuwakumba kwa siku za usoni. Ukiwatendea watu uovu au ubaya kwa kuwaonea, bakora za karma ya uovu ule zitakuja kuitandika Chadema siku zijazo.
Ushauri huu lengo lake ni kutuaminisha sisi Watanzania wengine tusio wanachama wa CHADEMA, kuwa Chadema ni chama cha haki na kinafanya maamuzi yake kwa haki kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni za haki, hivyo kutupa matumaini kuwa CHADEMA inaweza kuaminiwa na kukabidhiwa nchi mwaka 2025!, vinginevyo kwa mambo haya kama yalivyo sasa, na kama CHADEMA haitabadilika, then kwa 2025 CHADEMA itakuwa bado haijakomaa kiasi cha kutosha kuaminika na kukabidhiwa nchi!, hivyo 2025 ni CCM tena.!.
P
Tumia uamuzi wa haki, mahakama. Tukumbuke kuna wakati baadhi yao waliomba watoke mahakamani ili wajadiliane na kuomba msamaha lakini kuna wanaojiona viongozi wao waliendelea kuwachuuza wasio na sauti.1. Of course, kupigania au kutetea haki za watu ni jambo muhimu kiongozi. Hata mimi napenda iwe hivyo. In fact, ndilo takwa la kila mtu mwenye mapenzi mema - haki itendeke - kila upande utende haki.
2. Lakini kwa hili suala la Chadema na ex-wanachama wao inabidi kuliangalia vizuri bila kuwa 'biased'.
3. Hao akina dada nilipenda sana michango yao na hata baada ya kuwa kwenye hili tatizo waliendelea kutoa michango mizuri bungeni.
4. Hata mimi nilisikitika sana nilipoona kwamba pande zote mbili zilishindwa kukutana/kupata mwafaka maana nilitamani wabaki upande huu ili serikali iendelee kupata mchango mzuri kutoka upande wao kama chama.
5. Kwa upande mwingine, kama ni kweli waligushi barua na sahihi ili waapishwe as if wamependekezwa na Chadema katika kipindi ambacho walitakiwa kusimama pamoja siwezi kuona kama kosa lao ni dogo na la Chadema kutowasamehe ndilo kubwa zaidi. Hata kama tungewapima kwa kutumia kanuni ya kusema ni upande gani tunaweza kusema walichokifanya ni 'lesser evil' sidhani kama upande wao una merit hiyo 'lesser evil' kwa sababu Chadema waliamua kama walivyoamua kutokana na kuona kwamba "wamesalitiwa" na in this case usaliti unaharibu kanuni zote (kama kweli walisaliti).
6. Kama Chadema waliwapa hizo barua na kuzisaini na kubariki uteuzi wao kama Chama na baadaye wakatudanganya kwamba hawajawahi kufanya kitu kama hicho, hapo Chadema ni wa kulaumiwa muda wote mpaka watakapokuja tena hadharani na kutuomba radhi kwamba walitudanganya.
7. Otherwise, bado kwa maoni yangu natoa the benefit of the doubt kwa pande zote, ila kama kuna upande unatudanganya unatukosea sana. Kama pande zote ziko sahihi, then ni muhimu kupata reconciliation sehemu ambayo kumetokea misunderstandings.
8. Kwa vile sina chama na sina upande wa kuegemea, hata mimi nasema napenda kutetea haki ambayo pia inaambatana na wajibu.
Mbona mahakama ilisema uamuzi wa kamati kuu wa kuwafukuza ulikuwa sawa au mahakama haikuwatendea haki?Tumia uamuzi wa haki, mahakama. Tukumbuke kuna wakati baadhi yao waliomba watoke mahakamani ili wajadiliane na kuomba msamaha lakini kuna wanaojiona viongozi wao waliendelea kuwachuuza wasio na sauti.
Nimeandika hivyo kutokana na wewe kuwapa 50 50 kwenye shauri lao, mahakama ilitoa 100 kwa Chadema.Mbona mahakama ilisema uamuzi wa kamati kuu wa kuwafukuza ulikuwa sawa au mahakama haikuwatendea haki?
Mimi nimesema sina upande ninaoegemea, hivyo siwezi kuegemea upande wa X dhidi ya Y. Lakini kwa vile kuna tuhuma kwamba waligushi barua na sahihi, ndiyo maana nikasema kama hiyo ni kweli, hawawezi kustahili kanuni ya 'lesser evil' na kuona Chadema ndio hawakutenda haki. Kwa sababu tatizo la jambo hili kwa maoni yangu chanzo siyo Chadema, bali ni kuapishwa kwa hao wabunge waliodai walipata baraka zote kutoka kwa chama chao, wakati chama chao kinadai hakijawahi kufanya kitu kama hicho. So, 50:50 ni katika mkutadha kwamba kama madai ya kila upande hayajapatiwa ufumbuzi. Lakini kama kuna upande uligushi na kutuaminisha kwamba walichokifanya kilikuwa na baraka za chama wakati siyo kweli, kwa kutumia the principle of double effect, "the lesser evil" iko upande wa Chadema (kama kuna eneo Chadema walikosea). In this case, kosa lao (kama lipo) kwa maoni yangu ni dogo sana ukilinganisha na kosa la upande wa hao 'ex-members' 19 walilolifanya. Anyway, sipendi kujadili mambo ya vyama kwa sababu siyo mzoefu sana katika hayo na nimejikuta nafanya hivi baada ya kutoa maoni yangu kwa maoni aliyoyatoa ndugu Paskali Mayala. Asante.Nimeandika hivyo kutokana na wewe kuwapa 50 50 kwenye shauri lao, mahakama ilitoa 100 kwa Chadema.
Figure of speech in quotation marks. Some kind of reward au mere gratification of the soul.Mkuu Drifter, honest and genuineness ya mtu inakaa ndani yake, ila pia ni kama ilivyo justice, must not only be done, but must be seen to be done!.
Ushauri honest and bonafide genuine must be seen with naked eyes.
Kama mtu anaye toa ushauri kama huu, unauona ni ushauri wa ki Yuda Eskariote na kuniulizia how many “pieces of silver”?, then naomba niheshimu mawazo yako kwasababu watu hatufanani, and we don't think the same!.
P
Naomba uheshimu hukumu ya mahakama kwamba walifukuzwa kihalali, huo ndiyo ulikuwa mwisho wa utata wa kufukuzwa kwao.Mimi nimesema sina upande ninaoegemea, hivyo siwezi kuegemea upande wa X dhidi ya Y. Lakini kwa vile kuna tuhuma kwamba waligushi barua na sahihi, ndiyo maana nikasema kama hiyo ni kweli, hawawezi kustahili kanuni ya 'lesser evil' na kuona Chadema ndio hawakutenda haki. Kwa sababu tatizo la jambo hili kwa maoni yangu chanzo siyo Chadema, bali ni kuapishwa kwa hao wabunge waliodai walipata baraka zote kutoka kwa chama chao, wakati chama chao kinadai hakijawahi kufanya kitu kama hicho. So, 50:50 ni katika mkutadha kwamba kama madai ya kila upande hayajapatiwa ufumbuzi. Lakini kama kuna upande uligushi na kutuaminisha kwamba walichokifanya kilikuwa na baraka za chama wakati siyo kweli, kwa kutumia the principle of double effect, "the lesser evil" iko upande wa Chadema (kama kuna eneo Chadema walikosea). In this case, kosa lao (kama lipo) kwa maoni yangu ni dogo sana ukilinganisha na kosa la upande wa hao 'ex-members' 19 walilolifanya. Anyway, sipendi kujadili mambo ya vyama kwa sababu siyo mzoefu sana katika hayo na nimejikuta nafanya hivi baada ya kutoa maoni yangu kwa maoni aliyoyatoa ndugu Paskali Mayala. Asante.
Si ndivyo nilivyosema au wewe unataka nisemeje? Soma vizuri tangu nilipoanza ku'post' hii post labda hapo utaelewa ninachokisema. In fact, nilitofautiana na Paskali Mayala anayeona Chadema hawakuwatendea haki. Nikamuuliza kama anaona kugushi barua na sahihi kwamba walipendekezwa na kupewa baraka za chama ni sahihi. Hoja imeanzia hapo. Sasa unaniambia nini, mkuu? Soma tangu mwanzo utaona ninasema nini.Naomba uheshimu hukumu ya mahakama kwamba walifukuzwa kihalali, huo ndiyo ulikuwa mwisho wa utata wa kufukuzwa kwao.