Wanabodi,
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa, Chadema ni chama cha Kitaifa hivyo haya yanayoendelea ndani ya Chadema katika huu mgogoro wake na wabunge wake 19 wa viti maalum, una athari za Kitaifa zenye maslahi kwa taifa.
Hoja yangu ya leo ni hii ,"kuna watu wana macho lakini hawaoni!, na wana masikio lakini hawasikii!". Swali ni je Chadema wana macho na yanaona?. Je wana masikio na yanasikia?
Kwenye hili la Wabunge 19, je Chadema wawasamehe wabarikiwe, au waendelee kukomaa nao mpaka kieleweke hata kama ni kulaaniwa?
Naomba kukiri kupandisha bandiko hili, kwa inspirational kutoka andiko la Kaka yangu/mdogo wangu na bosi wangu kule TEF, Deodatus Balile.
Balile ameandika bandiko hili akiwa safarini jijini New Delhi nchni India.
C&P ya Balile.
Mwisho wa kunukuu
Chief @Balile , nikiwa New Delhi nilijifunza imani ya Hinduism kuhusu kitu kinachoitwa karma, hivyo ushauri wako kwa Chadema, utawaepushia Chadema karma ya mambo
mabaya waliowatenda hawa wadada 19 ambao mimi nawaita ni mashujaa, hivyo huu ni ushauri mzuri, wa hekima na busara sana kwa Chadema wenye maslahi kwa Chadema na maslahi kwa taifa only if Chadema wana macho ya kuona na wanaona, na wana masikio ya kusikia na wanasikia, kwasababu kuna watu wana macho lakini hawaoni, na wana masikio lakini hawasikii.
Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anakabiliwa na kesi ya ugaidi, nilipandisha makala mfufulizo za Kilio cha Haki, nikiangazia haki jinai.
Kwenye sala yetu ya Baba Yetu, kuna mstari "Utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea" hivyo tulimpongeza rais Samia kwa kauli hii baada ya Freeman Mbowe kuombewa msamaha
Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?
Baada tuu ya bandiko hili, haukupita muda hatimaye Freeman Mbowe alisamehewa na kesi ya Mbowe ilifutwa!,
Sisi wa kupongeza tukapongeza
Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
Sasa kuna ugumu gani Chadema kuwasamehe hawa wabunge wake 19?.
Hili sakata la wabunge hawa toka lilipoanza, mimi nimekuwa very open, objective and very transparent
Na nikashauri Chadema
Katika Salaam zangu kwa mwaka mpya,
Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa, wakipata vema na kupendana. Tulikotoka ni kugumu, tunakokwenda ni kurahisi, kuzuri! Heri ya Mwaka Mpya wahusika wote
Japo kwa jicho la juu juu, hao 19, wanaonekana kama wameshinda kesi yao mahakamani but in reality ni wameshindwa na hili nililisema
The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia! kwasababu katiba ya Chadema ina kipengele kilicho kinyume cha katiba, mwanachama wa Chadema akifungua shauri lolote mahakani, akishindwa kesi ni amejifukuzisha, hivyo Mahakama tayari imeishabariki kufukuzwa kwao, salama yao ni kusamehewa tuu!.
Kwa vile mimi namfahamu Freeman Mbowe kuliko Chadema wengi, Mbowe ni muungwana, Mbowe ni mtu wa shukrani, na baada ya kikao cha CC kuwatimua, Freeman Mbowe aliingia huruma na kufukuzwa kwao, akawasamehe, akawaita Nairobi, akawasamehe, akawashauri waombe msamaha, ili wayamalize, wakamgomea!.
It's high time Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Aikael Mbowe, kuitumia kofia yake ya Uenyekiti wa Chadema kwa kuitekeleza kwa vitendo sala ya Baba Yetu, kwa mtindo wa reciprocity kama yeye alivyosamehewa bila kuomba msamaha, sasa ni zamu ya na yeye kusamehe tuu bila kuombwa msamaha?., au Chadema iendelee kukomaa nao ili kuwaonyesha, kuwakomoa na kuwanyorosha?.
Tena na mimi kwa vile ubavu wangu ni pande za Kaskazi, na mimi nimeunga tela hija za migombani.
Merry Christmas
Paskali.
Update swali very objective
Mkuu
Bulesi , there you are.
Katiba ya Chadema imeweka utaratibu wa kuwatimua wanachama wake, nimekuwekea katiba ya Chadema ya 2006, hapo chini , kwanini CC ya Chadema imewatimua kinyume cha utaratibu wa kwenye katiba yao?.
Kuwatimua kwa haki ni kuwatimua kwa mujibu wa katiba ya Chadema.
Hata mtu anayehukumiwa kunyonywa, adhabu hiyo inatekelezwa kwa utaratibu.
- Baada ya hukumu ya kunyongwa, mtuhumiwa atahamishiwa gereza la kunyongea kwa Tanzania ni Gereza la Isanga.
- Huko gerezani, huwekwa chumba cha peke yake, na hafanyi kazi yoyote zaidi ya kula na kulala.
- Mfungwa huyo hupatiwa huduma za ushauri nasaha kumuandaa kwa kifo.
- Pia hupatiwa huduma za kiroho kwa mujibu wa imani ya dini yake ili kumuandaa kwenda kukutana na muumba wake.
- Nakala ya hukumu hupelekwa Ikulu kutayarishiwa Death Warrant ambayo lazima Rais wa nchi aisaini ndipo adhabu hiyo hutekelezwa.
- Rais akiisha saini death warrant, itaonyesha mfungwa huyo atanyongwa lini, wapi na saa ngapi.
- Ndugu wa mfungwa huarifiwa, kuwapa fursa ya kuja kumuaga kabla ya kunyongwa.
- Ndugu wa aliyemua hujulishwa kama watapenda kushuhudia.
- Siku ya kunyongwa hufanyiwa usafi, shaving, new dress, heavy breakfast.
- Kabla ya kunyongwa daktari humpima kujiridhisha yuko fit kiafya, akikutwa na ugonjwa wowote, hata homa tuu, au mafua, adhabu haitekelezwi, anapaswa kutibiwa kwanza apone ndipo anyongwe.
- Akikutwa fit, hupewa fursa ya kuaga ndugu zake na kutoa neno lolote la mwisho.
- Viongozi wa dini yake humsalia sala ya mwisho, kama ni Mkristo Mkatoliki hupakwa mafuta ya krisma.
- Ndipo hunyongwa na kama ni Muislamu hunyongwa kwa kutizamishwa kibla.
- Baada ya kunyongwa, daktari hiitwa kuthibitisha amekufa.
- Familia hukabidhiwa mwili kwenda kuuzika.
Huo ni utaratibu.
Kumfutia mwanachama uanachama wake ndio capital punishment kwenye chama lazima ufunyike kwa uangalifu na umakini kwa mujibu wa katiba ya Chadema. Kwanini haukufanyika?.
Kwa faida ya wasio na uwezo wa kuisoma katiba, nimewawekea hivyo vifungu hapa
Kwa Vile Kamati Kuu ya Chadema Imewaita Kina Halima Mdee ili Iwahoji, na Wamegomea Mwito, Naomba Kuwaletea Vifungu vya Mamlaka ya Nidhamu Kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema.
6.5 Taratibu zifuatazo lazima zizingatiwe katika kuchukua hatua za kinidhamu:-
6.5.1 Kila tawi litaweka kumbukumbu/orodha ya wanachama wanaokoma kuwa wanachama Uongozi na Vikao vya Tawi. Kumbukumbu itaonyesha jina kamili la mwanachama katika rejista ya wanachama tarehe aliyokoma kuwa mwanachama wa Tawi na sababu za kukoma kuwa mwanachama.
6.5.2 Kwa mujibu wa Ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza: (haya ni masherti ya vikao vya nidhamu)
(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu ya maandishi katika muda usiopungua wiki mbili. (Mashitaka ni kwa maandishi na Majibu ni kwa maandishi na sio kuitana kienyeji enyeji)
(b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
(c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
(d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu wa kifungu (a) na (b) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa ( kwenye issue ya kina Halima Mdee, kulikuwa na uharaka huu?.) isipokuwa mwachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.
6.5.3 Mtu yeyote aliyepoteza uanachama wake kwa mujibu wa Ibara ya 5.4 ya Katiba atapoteza haki zake zote za uanachama na hatarudishiwa ada, zawadi au ruzuku yeyote aliyokwishaitoa kabla ya kupoteza uanachama wake.
6.5.4 Mwanachama aliyepewa adhabu na kikao kimoja cha kikatiba atakuwa na haki ya kukata rufani kwa kikao cha ngazi ya juu ya kile kilichompa adhabu.
6.5.5 Mwanachama aliyewahi kuachishwa ama kufukuzwa uanachama anaweza kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu za kutaka kurejea. Maombi yake yatachunguzwa kwenye ngazi hiyo na kutolewa maamuzi na vikao vya ngazi moja ya juu inayofuata. Aliyesimamishwa au kufukuzwa na Kamati Kuu ataweza tu kurejeshwa na Baraza Kuu. Watakaofukuzwa na Mkutano Mkuu hawatakuwa na chombo kingine chochote kitakachotengua uamuzi huo.
6.5.6 Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.
6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kukata rufani au
6.5.9 Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu.
6.5.10 Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya kikao cha maamuzi.
Sasa kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa kama nilivyo zianisha hapo juu, jee zilifuatwa?
- Kwa nini CC ya Chadema, inawaita watu kihuni huni tuu, bila kuandaa hati ya mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?.
- Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia. Je, hili lilifanyika? Nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, je huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?
- Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, je hili litafanyika?
- Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee this time Chadema itafuata taratibu?
Halima na genge lake they are very right, kugomea wito huo wa kienyeji wa kufika mbele ya Kangaroo court iitwayo CC ya Chadema ambapo CC hiyo inapokaa kama a Kangaroo court, kazi yake huwa ni moja tuu, kuchinja bila kueleleza Kibla!. Ukichinja bila kuelekeza Kibla, kunahesabika ni kunyonga. Chadema ilizoea kufanya mambo kienyeji, leo imekutana na kisiki cha mpingo!.
Chadema sasa lazima ijifunze kufanya mambo kwa kufuata katiba yake, sheria, taratibu na kanuni!, kufanya mambo kwa kienyeji enyeji kwa mtindo wa zimamoto, sasa basi!
Paskali