Wana Msimbazi wenzangu Kagere anaweza kuondoka simba muda wowote kama mipango ikienda sawia.

kibol

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
4,521
Reaction score
2,747
Klabu za As Vita ya DRC Congo na zamalek ya misri zipo tayari kumnunua kwa Dola 200,000 ( ambazo ni sawa na Sh460 milioni),.

Meneja wake alisema fedha hizo zitakagawanywa mara tatu, Simba itaambulia chao kwa kuvunjwa mkataba huku meneja na mchezaji nao watapata chao.

Simba walimsajili Kagere kwa Dola 60,000( zaidi ya Sh120 milioni), huku ikimpa mshahara wa Dola 6000 (zaidi ya Sh12 milioni kwa mwezi.

“Kagere yupo tayari kuondoka Simba, kwani haya ni maisha na soka ndio ajira yake pekee, hizo timu ziliwasiliana nami ila niliwaeleza ukweli, ana mkataba wa miaka miwili japo ameshatumikia miezi sita Simba, wameonyesha utayari wa kuvunja mkataba huo.

Kwa upande wa Kagere alisema; “Ni kweli kuna ofa nyingi lakini kila kitu kipo chini ya meneja wangu, hivyo wakikubaliana mimi sina tatizo nitakwenda.”

Source mwanaspoti.
 
Sura haidanganyi...Kagere grandpa
Ngasa ndio grandpa ndio maana kiwango kimeisha kabisa, kagere mtoto wa juzi juzi tu ndio maana vilabu vikubwa vinamng'ang'ania unlike Ngasa aliyetoka ndanda na kuja yanga baada ya yanga kufulia na kukosa hela za usajili.
 
Kagere ni sawa na Mzee wa Kiminyio
Naona mmekosa hoja na kuingia kwenye issue ya umri, mwaka jana mlikuwa mnamuita Okwi mhenga ila mziki wake mliuona kwenye ligi kuu msimu uliopita, hivyo jifunzeni kujenga hoja za kueleweka na sio hivi viroja mnavyoleta hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…