Unachotakiwa pia ufahamu kwa mtu kama MO mpaka afikie maamuzi ya kuweka 20 billion simba hajakurupuka, ameshafanya feasibility study ya kutosha akaona kuna possibility ya yeye kupata na Simba kuzidi kuwa imara yaani win win situation, kingine unachotakiwa ukifahamu pia ni kuwa MO anamiliki 49% tu ya klabu yetu nyingine ni sie wanachama wa simba hivyo simba haimtegemei MO kujiendesha kwa kila kitu kwani kabla hajaweka fedha zake simba tulikuwa tunajiendeshaje? Ulishawahi kuona tunatembeza bakuli? Nyuma ya simba kuna watu wana akili na uelewa wa namna ya uendeshaji wa klabu kubwa kama simba, zipo brains za kutosha mkuu.