Wana Simba SC hali si nzuri kwa Kesho ila Babu yangu yule wa Pemba Zanzibar kaniambia hili lifanyike haraka ili Nkana FC ' Afe ' kwa Mchina

Nitarudi katika Uzi huu SAA moja jion kesho ,napata uoga sana juu ya wachezaji wetu ..hawajitumi sana
 
Kwenye mpira hakuna uchawi ndg yangu ingekua ivo sumbawanga kungekua Ata na timu ligi kuu au kigoma ipandisha timu na kuchukua kombe kabisa
 
Kumbe kwenye mpira pia wanarogana? Hatari sana hii inanikumbusha ile cartoon fulani inaitwa EARLY MAN wachezaji wanafanya mawasiliano na Ancestors kabla ya mechi na mechi ilipoanza kunasehem golikipa alipelekewa shoot la kichawi kabisa maana mpira ulikwenda ukiwa unawaka moto kipa alipokinga mikono akapitiwa na lile shoot hata hadi kwenye nyavu na ushindi ukapatikana. Nadhani ile movie ya katuni inafanana na hii mikakati
 

Ungekuwa umecheza mpira wowote wa ngazi za ' Mashindano ' kama UMISETA au UMISHUMTA au Timu za Mtaani za Ligi Daraja la Nne hadi la Tatu hapo usingeshangaa hiki ambacho unakishangaa sasa. Tuliocheza mpira tunajua linaloendelea / kinachoendelea.
 
Babu yako hakukwambia lolote kilichotokea kitwe Mkuu?
 
Ungekuwa umecheza mpira wowote wa ngazi za ' Mashindano ' kama UMISETA au UMISHUMTA au Timu za Mtaani za Ligi Daraja la Nne hadi la Tatu hapo usingeshangaa hiki ambacho unakishangaa sasa. Tuliocheza mpira tunajua linaloendelea / kinachoendelea.
UMISETA na UMITASHUMTA nimeshiriki lakini sikuona hayo mambo labda kwakua sikutilia maanani sana japo kunakipindi wachezaji wanaotakiwa kwenda kucheza walikua wakienda mtoni kuoga maji ya moto ambayo yalikua yanatoka pangoni, nadhani kulikua na maana yake
 

Sasa umekataa nini na umekubali nini?
 
hahahahahaha! nasikitika kuwajulisha kuwa it is too late! ungesema mapema ili tuwape mganga wetu kwa muda apindue matokeo! anyway tusubiri matokeo, mpira ni dk 90
 
Mkuu gentamicin unajua kweli haya mambo maana mkude Jana nyota yake ilikua juu kawasumbua sana na kawapiga bonge la kamba, haya mambo ya ndani unayajuaje? Af wakati wanaingia nkana waliingia na ile staili yao kama wanapaka mafuta kichwani mkude akawaiga, je ilikua na mana yoyote?

Ni kweli mpira wa tz hua wanachanganya na ushirikina nilikua kiongozi timu moja ya ndondo mkoa flan kuna mechi mnaweza msiroge ila nusu au fainali yenyewe lazma kuroga. Kuna mwaka nilienda umiseta nikiwa nafundisha mchezo tofauti na soka, makocha wa timu ya mpira wa miguu ya mkoa wetu walikua wanavuka maji kwenda ukerewe kuchukua dawa. Madhindano yalifanyikia mwanza hivyo haikua mbali sana watu walienda asubuhi na meli ya saa mbili na kurudi saa tisa. Kilichonikera ni kuwapaka watoto madawa na kuwapa kubeba. Kwanza ukibeba mikoba ya timu unaweza kuumia vibaya au kufa kbs kama utagongana ama kugusana na mpinzani mwenye dawa ilozidi nguvu. Pili sipendi watoto wajifunze mpira na ushirikina labda waje wajifunze wakiwa watu wazima sio vzr mzazi kutoa mtoto wake kwenda kucheza af anarudi mshirikina. Niliwaambiwa wale makocha kama wanataka waroge ila wasiwahusishe kbs wanafunzi na nikawaita wanafunzi baadh nikawakataza kufanya lolote la kiganga watakaloambiwa. Nilisemewa kwa afsa michezo wa mkoa nikaambiwa ndio mwisho na mwanzo kupewa timu kwenda taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…