Wana Simba SC, piga kura kama unataka timu ichukuliwe na Mo Dewji au la

Wana Simba SC, piga kura kama unataka timu ichukuliwe na Mo Dewji au la

Mo akiichukia Simba timu itakua nzuri na Yanga HATUTAPUMUA KWA MANENO, hivyo wazee wa Simba msimpe timu Mo. Mzuieni tu na mmwambie hii ni timu ya wananchi wote hawezi kupewa yeye
 
hatimae bwana yanga kapita kwa mbinde sana ila kapita....sasa wana simba tujiandae tu kuumizwa na maneno ya mropokaji jerry muro wakirudi........
 
NDIYO



Simba waache mambo ya kizamani. Mpira ni pesa ona Yanga, Azam

Ona Real Madrid, Man City Barcelona. Mpira ni pesa kwa sasa, mpira ni utajiri na mpira unaendeahwa na matajiri kote duniani. Ona TP Mazembe. Mpe Mo 50 hisa na 50 ziwe za hao wanaoitwa wanachama au uwiano wa hisa 51:49 (au vyovyote itajavyoonekana inafaa na wanasheria wa Simba) lakini kwa hali ya sasa ya fedha Simba iliyo nayo, itaendelea kushika namba 3 hata kwa msimu huu. Ukweli mchungu huu. Fedha ndiyo kila kitu.
Haya ni maoni yangu. Lakini maslahi ya Wanachama lazima yazingatiwe, maana huyo ni mfanyabiashara ukilemaa imekula kwenu, asije akajimilikisha jumla. Be careful!
 
Michango ya wanachama wapi? Tuelezane ukweli. We umeshachangia mara ngap?wanachama wa simba wapo wangap.?walio hai.acha mashabiki na wanachama wa msimu. Unajua gharama za kuendesha team?hizi porojo si wakat wake huu.

Hawa viongozi waliopo lazima wabadilishwe, ili uingie uongozi mwingine lakini sio timu akabidhiwe Dewji kama kampuni. Simba ni zaidi ya kampuni, inaweza kujiendesha kwa kutumia michango ya wanachama tu.

Tusijaribu kujifananisha na timu za ulaya kwani wao wana misingi ya uwazi sana kuliko sisi. Huyo Dewji atatumia simba kujinufaisha kibiashara, kama anapenda maendeleo ya simba agombee urais muda ukifika. Sio kumiliki timu na kama anapenda maendeleo ya soka, hizo bilioni 20 anaweza kuanzisha timu kama mwenzie bakhresa alivyofanya.
 
Simba timu ya upinzani hawezi kuuziwa uyo kada wa ccm mbunge mstaafu.
Boss tupo kwenye MICHEZO mbona unatupeleka kwenye SIASA ! Wewe ni mbaguzi na hiyo ni dhambi kubwa sana Umesha leta ubaguzi kwamba SIMBA ni upinzani Ushindwe kwa jina Yesu .
 
Back
Top Bottom