Wana Simba SC tutaje wachezaji tunaoona hawatufai msimu ujao

Kweli na ukizingatia wengi wanaiona mara moja kwa mwaka..
 
49 kwa 51 inawezekana mkuu?.. Hapa sijaelewa
 
Vipi wa dar wanashindwa nini kujazana kwa sababu timu inafanya vizuri??wenyewe ndo hawataki kuwaona wachezaji wanaosababisha timu ifanye vizuri...tatizo linalosababisha mechi zikose watu wengi hapo dar ni kuwa watu wa dar kwa kuwa simba ndo uwanja wake wa nyumbani na wanaiona inacheza kila siku basi hata hamu inapungua
 
Huyu jamaa kesha uteka nyara uzi na kuubadili kabisa
 
Simba hadi sasa imefikia ukomo wa kusajiri wachezaji wa njee..so timu ikitaka kusajiri pro ni lazima waachwe wengine kama kina kwasi..
 
point less ..shame on you..ingekuwa hivyo Old traford ,anfiled ,zisingekuwa vinajaa...jamani si mnaona aina ya wanaojiita mashabiki tulio nao...yani anawaza na kuwazua ujinga tuuu..hapo ndipo akili yako ilipoishia,,yani kweli kisa eti timu iko dar..mashabiki wanaiona kila siku hivyo hamu inapungua,,kweli we juha aiseee....ndio maana nasema kwa ushabiki wa namna hii uliokuwa nao wewe iwe Yanga au Simba mashabiki tuitafakari sana...kwa mantiki hiyo unataka timu mechi zote 38 iwe inacheza miko tofauti tofauti ili watu wawe na hamu ya kuiona ..kudadadeki
 
Wewe ndo sio mzima...tena mgonjwa wa akili 😂 😂 😂 😂 😂 ....yaani unakaa kabisa unapoteza mda wako unafanya comparison ya Mpira wetu na Mpira wa ulaya....Ulaya wametuzidi kila kitu kuanzia level ya uchumi na karibia kila kitu...kule wenzio hata level ya uchumi wapo juu ndo maana unakuta kiingilio mechi gharama ni kubwa weka kiingilio hata milioni moja uwanja utajaa sasa hapa bongo ukiweka milioni moja si uwanjani ataenda Mo peke yake...kule Arsenal na Manchester wanaweza kutoka kwenda kucheza mechi hata nje ya nchi na mashabiki watajaa watasafiri wengine....sasa chukua simba na yanga wakacheze mechi hapo tu Zambia uone uwanja kama utafikisha hata mashabiki mia...kwanza wenye uwezo wa kusafiri ni wachache sana uchumi zero....sasa wewe leo hii unataka kuchambua soccer la africa unatumia reference za ulaya...kule washatuzidi kila kitu....mwisho utaanza kutaka kulinganisha hospitali za bongo na ulaya...bara bara za bongo na ulaya kitu ambacho hakipo sawa...sisi washabiki wa hapa bongo tunajitahidi tu kutokana na hali na level yetu but usitake kufanya comparison na ulaya
 
Oky.. you know every thing bro

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
unajua unapojitoa ufahamu ndio napozidi kukushangaa...kwa hiyo unataka kusema kiingilio cha tsh 2000 - 5000 kwa wiki kinakuwa kikubwa hadi kupepelekea uwanja kukosa walau watu 25000 tu ?yani hao tu kweli inashindikana kweli?

na labda tu nikwambie kitu..hata wale kule ulaya sio kwamba wanaumauwezoo sanaa kulingana na uchumi zao..wale kule uwezo wao wa kawaida tu...(linapokuja suala la uchumi..mwananchi kawaid wa USA anaweza akawa na uwezo kawaiad lakini akija TZ ataonekana kidogo anauwezo ) kulingana na mifumo...sasa hapa kwetu na mfumo wetu wa maisha sitaki kuamini kuwa wadau tunakusa tsh 3000 watu 25000 kwenda kutazama game taifa
 
Mzamiru yupo vizuri ila ndemla sina uhakika nae sana....simba inahitaji marekebisho sehemu chache but marekebisho yawe makubwa sana ya wachezaji wakubwa wa kimataifa....sehemu ya ulinzi na kiungo zipewe kipaumbele
Kiungo waje Sure boy Na muda WA azam
 
Wakuachwa: Zana,. Kwasi, juuko, bukaba, mbonde, mzamiru, mo Ibrahim, ndemla, salamba, mkude, kotei, Simba kwa Sasa imeyumba Sana kwenye eneo la kiungo,. Kotei na akina mkude wamefeli kabisa.
Kotei yupo vizuri mkude Hamna kitu
 
Mzee Mimi sio kama nyie baadhi yenu hapa hata hamuichangii timu yenu..katika orodha ya wanchama 1000 wa kwanza wa SSC Mimi nipo..kadi yangu ya uanachama nalipia kila mwaka ..na sidaiwi mpka miaka mitano mbele...shame on you shabiki maandazi
Kuna hisa asilimia 51 za wanachama umeshanunua au unajiita mwanachama tu, kumbuka sasa hivi sio elfu 2 tena kwa mwaka
 
Hivi wewe unajua kama kununua jezi tu ni moja ya chanzo cha mapato kutoka kwa fans!! Achilia mbali fans kujaa uwanjani, hata ulaya pesa huwa inarudi kwa kuuza jezi za team achilia mbali vitega uchumi vingine
 
Simba haina mfumo wa kadi sasa hivi , wanauza hisa je wewe umenunua hisa na jua hisa moja kwa sasa inagonga mpaka hata 500,000 kwa mtu mmoja hununui hisa wewe sio mwanachama wa simba
 
Wangapi hawana kadi na uwanjani wanaenda? Acha kujidhalilisha
 
We una matatizo wewe, hivi unafikiri kama Uganda angekuwa anahitaji point sisi tungeshinda ile match pamoja na nyomi la watu!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…