Wana vipaji ila nidhamu na dharau vinawarudisha nyuma

Wana vipaji ila nidhamu na dharau vinawarudisha nyuma

Mbona wote hao umewahusisha na kujiunga usafini?
Ndo sababu ya kupotea kwao uki base upande mmoja upande mwingine wanakupotezea mwisho wa siku wote wanakuacha dilema unaanza upya
 
1.BARAKAH DA PRINCE

ni moja kati ya msanii aliyekuwa anakuja vizuri sana katika tasnia ya bongo fleva mpaka kuna kipindi alikuwa anahofiwa na wasanii wakubwa nchini lakini huyu jamaa ana jeuri kupitiliza, alishawahi kuandikiwa nyimbo na goodluck gozbert na akakana hamjui alipoulizwa.

Goodluck alishawahi kuthibitisha alipohojiwa kwenye kipindi na salama kwamba kuna wasanii aliwaandikia nyimbo ila wakihojiwa wanasema hawamjui mwisho wa siku akaja kupotea baada ya kuingia kwenye vita ya wafalme wawili wa bongo fleva (diamond na alikiba),

alidanganywa ajitoe rock star atasainiwa WCB akaanza jeuri kwa viongozi wake mwisho aliishia kufanya collabo tu romy Jones mpaka leo yupo anahangaika kurudi katika peak yake ya mwanzoni ila kipaji anacho jeuri ndo zinamrudisha nyuma.

2.RUBY

Kama kuna msanii wa kike alitakiwa awe billionaire kupitia mziki basi ruby alistahili nafasi hiyo kwa kipaji alicho barikiwa na mpaka sasa hakuna msanii wa kike anayemkaribia kwa kuimba,
ila jeuri ndo inamfanya asipige hatua kuna kipindi alishawahi kukataa kushiriki FIESTA ambayo inaandaliwa na CLOUDS watu wenye mchango mkubwa kwenye safari yake ya mziki lakini aligoma kwa madai ya pesa kidogo aliyopewa.

Ruby huyu huyu alishawahi kugoma kufanya video ya SU aliyoshirikishwa na ya moto band na ndo sababu iliyomfanya mpaka leo asijiunge na WCB,
maana wakati wanatafuta msanii wa kike chaguo la kwanza la diamond lilikuwa RUBY ila viongozi walikataa kwa madai ya kwamba hana nidhamu.

3.YOUNG KILLER

kipaji cha RAP MUSIC kilichopewa kisogo na wadau wa mziki kwa jeuri na kiburi alichonacho cha kuwasema na kuwachana baadhi ya wasanii wenzake.
Huyu kijana pia alitakiwa aende WCB kipindi wasafi wapo katika harakati za kumalizana nae akaanza matusi na dharau kwa CLOUDS hatimae wakamfungia vioo akawa karibu na wasafi mwisho wa siku sio CLOUDS wala WCB wote wamemfungia vioo,
yupo anapambana peke yake kwenye kiza kinene na amepoteza mwelekeo kwa siku za karibuni anatoa nyimbo bila mpangilio kwa kukosa mtu wa kumsimamia.

4.HANSTONE

mtoto wa marehemu banza stone aliyekuwa chini ya ABBAH PROCESS pamoja na marioo wengi tulimjua kwenye IOKOTE aliyofanya na mauwa sama na chibonge aliyo shirikishwa na marioo,

Huyu bado alikuwa na safari ndefu kwenye career ya mziki na mengi ya kujifunza kutoka kwa wadau wa mziki ila alianza kuharibu safari yake mapema baada ya kukataa kutoa ushirikiano kwenye video ya chibonge badala yake wakaifanyia remix na kuondoa sauti yake kwenye video.

Taarifa zilidai anaelekea wasafi ila mpaka leo haijulikani yupo chini ya nani na anafanya nini kuendeleza kipaji chake alicho nacho.
Ukifanya jeuri na clouds umeishAa
 
Nnachojua kutoka kwa baraka hana kiburi ila n mkweli na anamsimamo katka anachokiamini that's y anaonekana anakiburi🚮
 
ALIKIBA ANA SHIDA GANI WAKATI TAYARI NI SUPERSTAR HUWA ANAAMUA TU KUPOTEA MWENYEWE MUDA WOWOTE ANAOTAKA KUTOKANA NA UBIZE WA BIASHARA ZAKE ZINGINE NA KURUDI KWENYE GAME MUDA ANAOTAKA.
TOFAUTISHA ALIKIBA NA HAO CHIPUKIZI WALIOTAJWA KWENYE UZI,ALIKIBA HAFANYI MUZIKI KWA SHIDA ANAPENDA KUBALANCE MAISHA.
LAITI KAMA ANGEAMUA KUTUMIA MIGUVU KAMA WANAYOTUMIA WASANII WENGINE HAKUNA MSANII YEYOTE WA BONGO ANGEMKARIBIA.
Hatusomagi magazeti we endelea kukaza fuvu ila kibamia ni utopolo Tena grade one[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wewe mleta mada umefanya makusudi au ndo bahati mbaya tu umejisahau??
Mbona hujamtaja RICH MAVOKO?
Huyu jamaa namjua personally yaani ana nyodo na jeuri Kama JIWE.
 
ALIKIBA ANA SHIDA GANI WAKATI TAYARI NI SUPERSTAR HUWA ANAAMUA TU KUPOTEA MWENYEWE MUDA WOWOTE ANAOTAKA KUTOKANA NA UBIZE WA BIASHARA ZAKE ZINGINE NA KURUDI KWENYE GAME MUDA ANAOTAKA.
TOFAUTISHA ALIKIBA NA HAO CHIPUKIZI WALIOTAJWA KWENYE UZI,ALIKIBA HAFANYI MUZIKI KWA SHIDA ANAPENDA KUBALANCE MAISHA.
LAITI KAMA ANGEAMUA KUTUMIA MIGUVU KAMA WANAYOTUMIA WASANII WENGINE HAKUNA MSANII YEYOTE WA BONGO ANGEMKARIBIA.
Ni miongoni mwa Wasanii wenye kiburi na majivuno.
 
Hapana sio kiburi umeshindwa kumsoma tu.
Alikiba ni mtu wa imani sasa ukitaka akunyenyekee au akutukuze au akupigie magoti na kumuonesha kwamba bila wewe hawezi kuishi hapo hamuwezi kuelewana.
Ukitaka kufanya naye kazi uwe wazi majukumu yako sio unataka uwe dalali au kishoka halafu umnyonye hamtaelewana

Huyo ana imani gani? Wakati anatomba Sana dada zetu na kuzalisha wanawake ovyo bila ndoa
 
[emoji3][emoji3][emoji3] Hata Mimi nilitaka kuuliza , mana kuna wasanii Wana biashara kubwa na hzo biashara ni Pasua kichwa Sana kuziendesha zinahtaj uwe busy Zaid ya maelezo lakn still wanagonga hits back to back ..... Sasa hzi za Alli Kiba duuh....
ndio maana anaishi mjini bila kuimba imba kila wakati.

au ulitaka kusikia anauza alkasusi.
 
Back
Top Bottom