Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwanza nianze kwa kukupongeza mleta swali hili zuri sana na majibu yake ni kama ifuatavyo:-
kwanza naomba niweke fungu lote hapa kwa ushahidi zaidi (6 Sasa ikawa kwamba hesabu ya wanadamu ilipoanza kuongezeka usoni pa nchi nao wakazaa mabinti,+ 2 ndipo wana wa Mungu wa kweli+ wakaanza kuwaona+ mabinti wa wanadamu, kwamba ni wenye sura ya kupendeza; nao wakajichukulia wake, yaani, wote waliowachagua. 3 Baada ya hapo Yehova akasema: “Roho yangu+ haitavumiliana sikuzote+ na mwanadamu kwa kuwa yeye pia ni mwili.+ Kwa hiyo siku zake zitakuwa miaka 120.”+ 4 Wanefili walikuwa duniani siku hizo, na pia baada ya hapo, wakati wana wa Mungu wa kweli walipoendelea kulala na binti za wanadamu nao wakawazalia wana, hao ndio waliokuwa watu wenye nguvu wa kale, wanaume wenye sifa. 5 Basi Yehova akaona kuwa ubaya wa mwanadamu ulikuwa mwingi duniani na kila mwelekeo+ wa fikira za moyo wake ulikuwa mbaya tu wakati wote.+ 6 Yehova akajuta+ kwamba amewafanya wanadamu duniani, naye akaumia moyoni+ mwake. 7 Kwa hiyo Yehova akasema: “Nitawafutilia mbali kutoka usoni pa nchi wanadamu ambao nimeumba,+ mwanadamu na mnyama wa kufugwa, na mnyama anayetembea na kiumbe kinachoruka cha mbinguni,+ kwa sababu ninajuta kwamba nimevifanya.”+ 8 Lakini Noa akapata kibali machoni pa Yehova.)
hao waliozungumzwa kuwa wana wakweli walikuwa ni malaika walioasi kutoka mbinguni na kuja duniani ona vifungu vya ushahidi kuhusu hilo (yuda 1:6 > 6 Na malaika ambao hawakubaki mahali pao pa kwanza bali wakayaacha makao yao wenyewe yanayofaa+ amewaweka akiba wakiwa na vifungo vya milele+ chini ya giza zito kwa ajili ya hukumu ya ile siku kuu.+)
kuhusu swali la pili kuwa hawa wanefili walionekana kwenye nchi ya kaanani majibu ya swali hili ni kuwa si kweli bali kilichokuwa kinazungumzwa zilikuwa ni ripoti za watu waliotumwa kwenda kuipeleza nchi ya kaanani sasa wakati wa kuleta ripoti hawa wapelelezi kati ya kalebu na wale wnegine walitofautiana kuwasilisha ripoti yao ambapo kalebu alisema nchi ile yafaa sana kwenda kuishi na ndiyo ilikuwa ripoti sahihi lakini hawa wapepelezi wengine wakasema kuwa nchi ile haifai kuishi kwakua kuna wanefili na haya yalikuwa maneno ya kuwaogopesha na kuwatisha waisraeli. sasa nikuombe mpendwa usome kifungu chote cha hesabu 13 utapata ukweli wa haya. soma hapa (13 Sasa Yehova akasema na Musa, na kumwambia: 2 “Tuma watu kwa ajili yako wapate kuipeleleza nchi ya Kanaani, ninayowapa wana wa Israeli.+ Mtamtuma mtu mmoja kwa ajili ya kila kabila la baba yake, kila mmoja wao mkuu+ kati yao.” 3 Basi Musa akawatuma kutoka katika nyika ya Parani+ kwa agizo la Yehova. Wanaume wote hao walikuwa vichwa vya wana wa Israeli. 4 Na haya ndiyo majina yao: Wa kabila la Rubeni, Shamua mwana wa Zakuri; 5 wa kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori; 6 wa kabila la Yuda, Kalebu+ mwana wa Yefune; 7 wa kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu; 8 wa kabila la Efraimu, Hoshea+ mwana wa Nuni; 9 wa kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu; 10 wa kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi; 11 wa kabila la Yosefu,+ kwa ajili ya kabila la Manase,+ Gadi mwana wa Susi; 12 wa kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali; 13 wa kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli; 14 wa kabila la Naftali, Nabi mwana wa Vofsi; 15 wa kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki. 16 Hayo ndiyo majina ya wanaume ambao Musa aliwatuma wakaipeleleze nchi. Na huyo Hoshea mwana wa Nuni, Musa akamwita Yehoshua.+ 17 Musa alipokuwa akiwatuma kuipeleleza nchi ya Kanaani, aliwaambia: “Pandeni hapa na kuingia Negebu,+ nanyi mtapanda na kuingia katika eneo lenye milima.+ 18 Nanyi mtaona jinsi nchi ilivyo+ na watu wanaokaa humo, ikiwa wana nguvu au ni dhaifu, ikiwa ni wachache au ni wengi; 19 na jinsi nchi wanayokaa ndani yake ilivyo, iwapo ni nzuri au ni mbaya, na jinsi majiji wanayokaa ndani yake yalivyo, iwapo ni katika kambi au ni katika ngome; 20 Na jinsi nchi ilivyo, iwapo ni nono au imekonda,+ iwapo kuna miti ndani yake au hakuna. Nanyi mjionyeshe kuwa hodari+ na kuchukua baadhi ya matunda ya nchi hiyo.” Sasa siku hizo zilikuwa siku za matunda yaliyoiva ya kwanza ya zabibu.+ 21 Basi wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka katika nyika ya Zini+ mpaka Rehobu+ mpaka mahali pa kuingilia pa Hamathi.+ 22 Walipopanda kuingia Negebu,+ ndipo wakafika Hebroni.+ Sasa Ahimani, Sheshai na Talmai,+ wale waliozaliwa kwa Anaki+ walikuwa huko. Hebroni+ lilikuwa limejengwa miaka saba kabla ya Soani+ la Misri. 23 Walipofika kwenye bonde la mto la Eshkoli,+ wakakata chipukizi lenye kishada kimoja cha zabibu.+ Na wawili kati ya wanaume hao wakalichukua kwa ufito, na pia baadhi ya makomamanga+ na baadhi ya tini. 24 Wakapaita mahali hapo bonde la mto la Eshkoli,+ kwa sababu ya kile kishada ambacho wana wa Israeli walikata kutoka huko. 25 Mwishowe, mwishoni mwa siku 40+ wakarudi kutoka kuipeleleza nchi. 26 Basi wakatembea na kuja kwa Musa na Haruni na kusanyiko lote la wana wa Israeli katika nyika ya Parani, huko Kadeshi.+ Nao wakaleta neno kwao na kwa kusanyiko lote na kuwaonyesha matunda ya nchi. 27 Nao wakampa habari na kusema: “Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo kwa kweli inatiririka maziwa na asali,+ na haya ni matunda yake.+ 28 Hata hivyo, mambo ya hakika ni kwamba watu wanaokaa katika nchi hiyo ni wenye nguvu, na majiji yenye ngome ni makubwa sana;+ na, pia, wazao wa Anaki tuliwaona huko.+ 29 Waamaleki+ wanakaa katika nchi ya Negebu,+ na Wahiti na Wayebusi+ na Waamori+ wanakaa katika eneo lenye milima, na Wakanaani+ wanakaa kando ya bahari na kando ya ukingo wa Yordani.” 30 Ndipo Kalebu+ akajaribu kuwatuliza watu mbele ya Musa naye akasema: “Na tupande moja kwa moja, nasi tutaimiliki, kwa sababu kwa hakika tunaweza kuishinda.”+ 31 Lakini wale watu waliopanda pamoja naye wakasema: “Hatuwezi kupanda kupigana na watu hao, kwa sababu ni wenye nguvu kuliko sisi.”+ 32 Nao wakazidi kuwaletea wana wa Israeli habari mbaya+ juu ya nchi waliyokuwa wameipeleleza, na kusema: “Ile nchi, tuliyoipitia ili kuipeleleza, ni nchi ambayo inakula wakaaji wake; na watu wote tuliowaona katikati yake ni watu wenye ukubwa usio wa kawaida.+ 33 Na humo tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki,+ waliotoka kwa Wanefili; hivi kwamba sisi tukawa machoni petu wenyewe kama panzi, na machoni pao sisi tukawa vivyo hivyo.”+
Wasalaam wanaJf. Naomba msaada juu ya Mwanzo 6:1-4. Ukisoma hii andiko unakutana na wanadamu, wana wa Mungu na Wanafili. Biblia inasema wana wa Mungu waliwaoa binti za binadamu na wakazaa nao. Muunganiko huu ulizaa majitu makubwa sana tena hodari walioitwa Wanefili.Suali langu ni kuwa hawa wana wa Mungu ni nani hasa, ni malaika au?
Mungu alichukizwa na matendo ya binadamu na akaamua kugharikisha watu wote isipokuwa familia moja watu wanane. Cha ajabu haya majitu makubwa wanaonekana kuwepo hata baada ya gharika. Ushahidi upo Hesabu 13:31-33. Hawa wana wa Anaki waliponaje kwenye gharika?
inasemekana kulikuwa na old bible, old bible ilikuwa imetokana na masimulizi ya wazee wa kiafrika.Hayo majitu inasemekana uzao wake ndio wazungu.Hiyo old bible iliharibiwa na wazungu,mikaka kama kumi kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusiana na old bible na kwanini wazungu walihiharibu mjadala huu ulifanywa na tv ya cnn ila maelezo ya wazee wa kiafrika yalikuwa straight tofauti na haya maelezo ambayo hayaelezi hao watu waliishia wapi.Kwa kifupi old bible ilimzungumzia zaidi mwafrikaWasalaam wanaJf. Naomba msaada juu ya Mwanzo 6:1-4. Ukisoma hii andiko unakutana na wanadamu, wana wa Mungu na Wanafili. Biblia inasema wana wa Mungu waliwaoa binti za binadamu na wakazaa nao. Muunganiko huu ulizaa majitu makubwa sana tena hodari walioitwa Wanefili.Suali langu ni kuwa hawa wana wa Mungu ni nani hasa, ni malaika au?
Mungu alichukizwa na matendo ya binadamu na akaamua kugharikisha watu wote isipokuwa familia moja watu wanane. Cha ajabu haya majitu makubwa wanaonekana kuwepo hata baada ya gharika. Ushahidi upo Hesabu 13:31-33. Hawa wana wa Anaki waliponaje kwenye gharika?
kati ya watu ambao sitaki kushilikiana nao ni wewe kumbuka comment yako hii "Maelezo mengi alafu yote pumu"Hiv Mkuu unabshana na maandiko? Andiko lnasema kabsa walioneka we unàpindsha maana
Mkuu tafuta kitabu cha Ennoch ' The book of Ennoch. au documentary zake. kinaeleza kwa kina kuhusu hii story.
Kiukweli nami nisomapo hiyo verse ya kitabu cha mwanzo kuhusu hayo majitu huwa napata maswali mengi.
Kikawaida kabisa walipoona duniani kuna wanawake wazuri wakaja na kuzaa nao inamaana huko mbinguni walikuwa wanaishije!? Je, waliishi na wake zao au walikuwa ni watumishi wa mwenyezi MUNGU na hawakuruhusiwa kuoa kabisa.
Walishukaje, shukaje huku ulimwenguni walikuja in form of spirit then baadaye wakaanza kuonekana physically! reaction ya wanadamu ilikuwaje baada ya kuwaona watu waajabu waliotofauti na wao kimaumbo maana wanatajwa kwamba walikuwa warefu sana na miili yao ilikuwa mikubwa pia. Hawakuwa na chimbuko lolote hapa ulimwenguni yaani Hawakuwa na wazazi, bali waliumbwa na MUNGU ili wamtumikie yy huko walipo.
Maisha ya dunia huku walipokuwa wanaishi waliyazoea tofauti na kule walipotoka, sabu mbinguni ni sehemu inayotajwa kuendelea sana kwa kila kitu na hivyo ndivyo tunavyojuzwa kwenye nyumba za ibada ss kama walikuja na kuishi huku iliwawia vigumu kukopi mazingira ya kizamani au walikuwa radhi kuishi hivyo hivyo tu ili mradi wamefanikiwa azma. Pia walipokuwa wanaishi huku duniani walikuwa na uwezo wa kwenda kuondoka kwenda mbinguni na kurudi tena ulimwenguni. Yaani nina maswali mengi!? Wataalamu nasubiri majibu yenu plz
kati ya watu ambao sitaki kushilikiana nao ni wewe kumbuka comment yako hii "Maelezo mengi alafu yote pumu"
Asante Mkuu. Nimepata hiki kitabu kutoka Google, kinaeleza mambo magumu sana isee. Kitabu kinaelezea mpaka mambo ya kuzaliwa kwa Yesu na mpaka ufunuo. Very interesting.
Hao "watu" mnaowazungumzia walikuwa malaika wa mbinguni.
Walipokuwa dunia (katika hali ya umalaika), waliwaka tamaa juu ya mabinti za dunia.
Wakajibadili na kuchukua mwili wa binadamu (ingawa walikuwa tofauti nasi kimaumbo)
Wakazaa na mabinti wa hapa duniani (ndio hao manefili).
Sasa baada ya hapo wakataka kujibadili tena kurudi kwenye hali ya umalaika. Jeshi la mbinguni likiongozwa na malaika mkuu Mikael likapigana nao vita na likawakamata na likawapeleka kuzimu.
Hao "malaika" wamefungiwa kuzimu, na wapo huko mpaka siku ya hukumu.
Kuzimu ni paala pabaya sana, na ndio maana ukiwa unatoa pepo na kumuamuru aende kuzimu, litapiga kalele sana ya kukataa kwenda huko. Mapepo yanatoa ushuhuda kuwa kuzimu kupo na watu huko wanaunguzwa vibaya mno na wamekuwa kama mkaa hivi, wana ulimi mrefuuu, ulimi unatafuta hata tone la maji lakini haupati.
Kuzimu kupo kwa asiyeamini. Lakini kama unataka kuamini Mimi naweza Ku prove.
Ndio maana sitaki kujihusisha na hizi dini maana ukisoma unaweza changanyikiwa.
Malaika walioasi! Malaika anamatamanio? Je huko mbinguni walikokua walikua wana mademu? Na kama hawakua na mademu na wala hawana matamanio ilikuaje wakawatamani binadamu? Na kama waliweza kuwalala wanawake Je wanamaumbile kama ya binadamu yaani wanaume?Aksante kwa majibu mzuri hasa suali la kwanza. Mpendwa naomba kutofautiana na wewe kuhusu suali la pili. Sioni kama wapelelezi 10 walikuwa na lengo la kuogopesha wana Waisraeli kwa kusema uwongo. Naamini hawa wapelelezi waliwakuta/ kuwaona wanefili walikotumwa. Kumbukumbu la Torati 3:11 inamrekodi Ogu mfalme wa Beshani kama mtu wa mwisho kwenye uzao as Wanefili. Hii inathibitisha kuwa haya majitu yaliendelea kuwepo mpaka baada ya Gharika. Hili unalizungumziaje mtumishi.
Hao "watu" mnaowazungumzia walikuwa malaika wa mbinguni.
Walipokuwa dunia (katika hali ya umalaika), waliwaka tamaa juu ya mabinti za dunia.
Wakajibadili na kuchukua mwili wa binadamu (ingawa walikuwa tofauti nasi kimaumbo)
Wakazaa na mabinti wa hapa duniani (ndio hao manefili).
Sasa baada ya hapo wakataka kujibadili tena kurudi kwenye hali ya umalaika. Jeshi la mbinguni likiongozwa na malaika mkuu Mikael likapigana nao vita na likawakamata na likawapeleka kuzimu.
Hao "malaika" wamefungiwa kuzimu, na wapo huko mpaka siku ya hukumu.
Kuzimu ni paala pabaya sana, na ndio maana ukiwa unatoa pepo na kumuamuru aende kuzimu, litapiga kalele sana ya kukataa kwenda huko. Mapepo yanatoa ushuhuda kuwa kuzimu kupo na watu huko wanaunguzwa vibaya mno na wamekuwa kama mkaa hivi, wana ulimi mrefuuu, ulimi unatafuta hata tone la maji lakini haupati.
Kuzimu kupo kwa asiyeamini. Lakini kama unataka kuamini Mimi naweza Ku prove.